Korea Kusini yaanza kuondoa vipaza sauti kwenye mpaka na korea kaskazini

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Jeshi la Korea Kusini limesema mapema hii leo kwamba limeanza kuondoa vipaza sauti vilivyopo kwenye eneo la mpaka na jirani yake Korea Kaskazini, kama hatua ya kupunguza mvutano kati ya mahasimu hao.

Vipaza sauti hivyo vilikuwa vikitumiwa kueneza propaganda dhidi ya Korea Kaskazini, lakini serikali mpya ya kiliberali ya Korea Kusini ilisitisha matangazo hayo mwezi Juni kama ishara ya maridhiano.

Serikali hiyo inaangazia kurejesha uaminifu na mazungumzo na Pyongyang ambayo imekata mahusiano na Korea Kusini kwa kiasi kikubwa katika siku za karibuni.

Korea Kaskazini ambayo inajilinda sana dhidi ya ukosoaji wa nje kuhusiana na utawala wake wa kiimla na kiongozi wake Kim Jong Un haikusema chochote kuhusiana na hatua hiyo.
 
KOBAZI NAO WAKIFIKIRIA HILI SUALA DUNIA ITAKAA KWA AMANI SANA
Kobazi kuna maandishi yanawaongoza kua wagomvi, Korea mbili hazina maandiko ya kiimani yanayo waongoza kua na chuki, wana tofauti za kiitikadi, mfumo wa Kikoministi na Ubepari; haya ni mambo ambayo sio ya kiimani and hence is easy to reconcile
 
Sasa ni lini waliwahi kuwa marafiki na wana uhasama tokea mwaka 1948 mpaka kulitokea vita vya Korea (1950-1953) na wameendelea kuwa mahasimu mpaka leo?

Ukomunisti na ubepari sio imani? Una uhakika?

Wapigana vita wakubwa dunia hii tena zilizokuwa kubwa kubwa sio nchi za Kiislam.
 
KOBAZI NAO WAKIFIKIRIA HILI SUALA DUNIA ITAKAA KWA AMANI SANA

Ni kwa sababu wao ndio walianzisha vita za dunia na kutumia silaha za nyuklia dhidi ya wengine??

Unaweza kunitajia "Kobazi" gani walioanzisha Cold War na kuhatarisha amani ya dunia kwa zaidi ya miaka 40?

Huo mgogoro wa Korea ambao mmoja wao ana nyuklia na anapenda kumtishia tishia ndugu yake ni wa "Kobazi"? Na huo mgogoro wao ni tokea miaka ya 1940 huko.

Sio "Kobazi" wala hawakuwa "Kobazi" ni wenye tabia ya kuwafuata wenyeji makwao na kuwafukuza na kuwafanyia wenyeji genocide kudai ni wao pale ndio kwao kama walivyofanya akina fulani huko Marekani kwa "Red Indians", Canada, Australia, South Africa, New Zealand na sasa Palestine.
 
Sasa ni lini waliwahi kuwa marafiki na wana uhasama tokea mwaka 1948 mpaka kulitokea vita vya Korea (1950-1953) na wameendelea kuwa mahasimu mpaka leo?

Ukomunisti na ubepari sio imani? Una uhakika?

Wapigana vita wakubwa dunia hii tena zilizokuwa kubwa kubwa sio nchi za Kiislam.
Ukoministi na Ubepari sio imani kaka, ni mifumo ya kiuchumi. Nyerere nae aliamini katika ukoministi. Hi ni mifumo ya kuwaletea watu maendeleo ambayo wachumi wa nchi husika huwashawishi viongozi wao na viongozi hua adopt mifumo hiyo. Mifumo hi hainaga nabii wala haiamini katika Mungu, sema mmoja unaamini katika demokrasia while nyingine inaamini katika one man show or ukipenda UDIKTETA.
 
Jeshi la Korea Kusini limesema mapema hii leo kwamba limeanza kuondoa vipaza sauti vilivyopo kwenye eneo la mpaka na jirani yake Korea Kaskazini, kama hatua ya kupunguza mvutano kati ya mahasimu hao.

Vipaza sauti hivyo vilikuwa vikitumiwa kueneza propaganda dhidi ya Korea Kaskazini, lakini serikali mpya ya kiliberali ya Korea Kusini ilisitisha matangazo hayo mwezi Juni kama ishara ya maridhiano.

Serikali hiyo inaangazia kurejesha uaminifu na mazungumzo na Pyongyang ambayo imekata mahusiano na Korea Kusini kwa kiasi kikubwa katika siku za karibuni.

Korea Kaskazini ambayo inajilinda sana dhidi ya ukosoaji wa nje kuhusiana na utawala wake wa kiimla na kiongozi wake Kim Jong Un haikusema chochote kuhusiana na hatua hiyo.
Eeeh trump atanunaa 😃😃😃achelewi kueka tariffs Korea kusin 🤣
 
Back
Top Bottom