Korea yanunua ardhi "kwa mkopo" Tanzania, Serikali yasita kuthibitisha


Mkuu siyo Serikali ya Pyongyang ni Serikali ya Seuol (Republic of Korea) siyo DPRK.
 

Tuwape ardhi? Tutajifunzaje namna ya kuendeleza ardhi wakati ardhi haipo na imeshachukuliwa na Wakorea. Kumbuka hatujui namna ya kulinda interest za nchi yetu kwenye mikataba, labda iwe baadaye baada ya kwanza kujifunza namna ya kuandika hiyo mikataba maana Mkorea hawezi kutufundisha namna ya kulinda interest zetu pale ambapo yeye ana interest. Nyerere kutaifinya mashamba ni blunder kubwa mojawapo tu ya zilizowahi tokea hapa TZ. Korea au nchi nyingine kwa namna yeyote ile haiwezi kuindeleza TZ kwani huko hawana interest nako.
 

Hebu fafanua hapo, una maana kilimo kikifanywa kwa usahihi kabisa, hakiwezi kumkomboa mwananchi? Unalinganisha na Uchina, kwa vipi?

Unaona ni rahisi "kuwaweka 80% ya watanzania kwenye service na manufacturing industries", kuliko kuwaendeleza kwenye kilimo, how?

Na ni asilimia ngapi ya Watanzania wako kwenye hiyo sekta uliyotaja?

Wakati huu ambapo chakula kimepungua sana duniani kutokana na nchi nyingi kukosa ardhi, na sehemu nyingi kujiingiza kwenye biofuels, mimi naona nchi kama Tanzania zinaweza kunufaika kwa kuzalisha sana chakula...chakula ndiyo bidhaa pekee ambayo haitaacha kununuliwa hata hali ya uchumi ikiwa mbaya namna gani.
 

who engineered the deal (contract)?? kama ni former AG, Chenge ... then Wallaah tumeliwa!!
 

Korea yatangaza kununua ardhi kubwa Tanzania, serikali yakana

Na Mwandishi Wetu


SERIKALI imesema kuwa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Ulaya kuwa imeuza ardhi ya ukubwa wa kilomita za mraba 1000 za kilimo kwa Korea ya Kusini kwa ajili ya matumizi ya kilimo si za kweli.

Taarifa zilizotolewa jana na vyombo hivyo zilieza kuwa Korea Kusini imekubaliana na serikali ya Tanzania kufikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya mataifa masikini na tajiri duniani.

Afisa wa Shirika linaloendeshwa na Serikali ya Korea linaloshughulikia maendeleo ya kilimo vijijini, Lee Ki-Churl, alinukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akisema kwamba mkataba huo utasainiwa mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkataba wa makubaliano kati ya mataifa hayo mawili ni matokeo ya ziara ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoifanya katika mataifa ya mashariki ya mbali.

Akizungumza jana, Waziri wa Kilimo na Chakula na Ushirika, Steven Wasira, aliliambia gazeti dada la hili la The Citizen kuwa hakuwa na taarifa na mkataba huo.

"Nilikuwa sehemu ya ujumbe wa Waziri Mkuu Korea Kusini na kilichotokea kule hakikuwa zaidi ya kuwakaribisha wawekezaji wa kigeni katika sekta zote ikiwamo ya kilimo."
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko alikanusha na akasema hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na serikali katika kilimo na Korea Kusini.

source: mwananchi 24/9/2009
 
Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni,

Mtukano ulikuwepo kati ya watanzania na wakorea, mazungumzo pia yalikuwepo hii haina ubishi. Ubishi uliopo ni je ni nini kiliongelewa na kukubaliwa?

Korea wanasema wanakuja kuchukua ardhi hapa Tanzania na sehemu na eneo linatajwa kabisa.
Tanzania tunaruka kimanga kwamba sio kweli, then the obvious conclusions is:

1. Mkutano ulifanyika kwa lugha ya Korea na ujumbe wetu kama kawaida haukuwa na mkalimani.

2. Mkataba uliandikwa kwa script za Korea kiasi kwamba mwanasheria wetu alishindwa kabisa kuona masharti ya huo mkataba.

3. Wajumbe wetu walikuwa wanafatigue na safari mpaka wakashindwa kuusoma vizuri na kuuelewa mkataba huo. Wakaamua kusaini tu ili warudi haraka nyumbani kupumzika.

Kwa hizo scenario tatu na majibu ya waziri inaonekana dhahiri kuwa tumepigwa changa la macho, wanasheria wa serikali wanasemaje kuhusu kuepuka balaa hili???????
 
Mwashangaa nini?mbona ingali tayari tumeshauza kwa falme za kiarabu kule loliondo-arusha,kwenye nchi yetu wenyewe tunakaribishwa kuwa tupo falme za karabu......kweli tumechoka.Hawa nao wanakuja hawana mtaji kama richmond tu,watachimba kwanza madini ili wapate mtaji!!!!!tuna viongozi wafu........neo-colonioslism
 


4. Pamoja na wajumbe wetu kuwa na jetlage, walipewa "lishe bora" na "mvinyo wa kutosha" hivyo kuwafanya 'laini' kufikia makubaliano ya mkataba.

5. Wajumbe wamerudi nyumbani, jetlag imekwisha na wamezinduka kwenye hangover ya mvinyo, sasa wanaona madudu waliyofanya...denial game is taking over
 
It is a different ways of viewing things. Mie jambo hili sina tatizo nalo ikiwa tunafanya mambo kwa maslahi ya nchi na watu wake. Bahati mbaya sana hali haiko hivyo ndo maana kwa kila hoja watu wanakuwa na wasiwasi.

Tuna ardhi kubwa kwa muda mrefu. Tumeshindwa kuitumia to our own advantage. Tunaweza kuikodisha ardhi hiyo kwa watakaoitumia na sisi tule rent. Pengine hiki ndiyo kinachotufaa. Ikiwa thinking iko hivyo hawa watu tutawatoza rent ambayo ni commercial. Tuweke kabisa policy ya kukodisha ardhi yetu commercially kwa wanaotaka kuitumia hapa sitakuwa na shida, kwani policy itakuwa debated na hatimaye sheria zitatungwa.

Kwa mfano, mimi nina kieneo changu hapa mjini ambacho nimejenga kibanda changu cha kuishi. Sifanyii biashara yoyote. Eneo lile ni wastani wa meta za mraba 2,600. Kodi kwa mwaka nalipia jumla ya shilingi 26,000 kwa mwaka kama land rent (nenda wizara ya ardhi ukathibitishe). Hii ni kiwango cha karibu shilingi 10 kwa kila meta moja ya mraba.

Sasa kwa hawa watu wa nje (wawe wakorea, waarabu au wazungu) tuwakodishe kwa viwango hivyo hivyo! Eneo hilo linalosemwa yaani kilomita za mraba 1,000 ni sawa na mita za mraba Billion moja kwani kila kilomita ya mraba moja, ina mita za mraba milioni moja (1,000,000). Sasa hawa wakorea tukiwakodisha kwa kiwango sawa na hiki ninacholipa mimi cha karibu shilingi 10 kwa mita moja ya mraba, hapa tumeshapata jumla ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka (karibu Dola milioni 8).

Lakini hawa wanaitumia ardhi hii kwa kilimo cha kibiashara. Kwa hiyo kodi yao iwe ni ya kibiashara angalau shilingi 100 tu kwa meta moja ya mraba. Tutapata kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa mwaka. Fedha hizi zikiingizwa kwenye subsidies kwa wakulima wa Tanzania (kwenye mbolea, madawa na zana za kilimo) tuna uhakika wa kuwa kilimo chetu kitakuwa kimepona for good.

Tanzania tuna ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo, zaidi ya kilomita 250,000 za mraba. Hata tukikodisha kilomita 50,000 tu za mraba tutapata Zaidi ya Dola bilioni nne. Fedha hizi zitatosha kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda tunayoota ndoto kuyapata. Tunahitaji a different way of thinking!

Ikiwa ardhi ina thamani kihivyo, kwa nini tusikodishe tukala rent?? Tatizo tutawapa ardhi bure kwa ahadi kuwa tutaajiriwa mashambani na kukuza uchumi. Hata kodi hizi tunazowakandamiza watanzania WAGENI HAWAZILIPI!!! HILI NDO TATIZO LETU!!
 

Wakorea wataichukuwa Ardhi kuipeleka wapi? unanshangaza! na hiyo work force yoooote ya kwenye hiyo Ardhi itakuwa ni wa Korea? Unanshangaza!
 

JMK sio Dikteta wala mtu wa kukurupuka kama alivyokuwa Nyerere, kila mwenye kosa atashughulikiwa systematically na hakuna atae escape, its a matter of time.
 
Nadhani jibu unalo!

Miye siye niliyeuliza swali 🙂 Najua fika kwamba mikataba inayosainiwa na Serikali ya CCM ya kuchimba madini yetu au kuwakaribisha "wachukuaji" ni ya bei ya kutupa kabisa haina maslahi yoyote kwa nchi yetu na Watanzania wengi tunalijua hili siyo siri kabisa.
 

Hayo ya kuwajibisha na kuwajibishwa nimeshayajibu katika post hiyo hapo juu, sitaki kuyarudia.

Nyerere, aliikuta Dar Es Salaam nzuri kama mtoto, na kama ilivyo.Hakuna alichokiongeza wala kuwa na nadharia ya kuongeza. Uozo wa Dar Es Salaam wa hivi sasa unatokana na huko nyuma (Kwa Nyerere). Na Dar Es Salaam ilianza kuharibika wakati wa Nyerere. Tuulize sisi tuliozaliwa na kukulia hapa tukueleze! Hakuna muundo mbinu mpaya wowote alioufanya Nyerere Dar Es Salaam utaozidi asilimia moja ya aliyoyakuta.
 
JMK sio Dikteta wala mtu wa kukurupuka kama alivyokuwa Nyerere, kila mwenye kosa atashughulikiwa systematically na hakuna atae escape, its a matter of time.

Atawashughulikia mwaka gani? 2015 wakati anamaliza awamu yake ya pili!? Yeye mwenyewe kaingia Ikulu kwa kubebwa na mafisadi unadhani atakuwa na ubavu wa kuukata mkono uliombeba!? Si ndiyo nchi itawaka moto maana mkanda mzima sinema ya yalitokea katika kampeni za kutafuta mgombea wa CCM 2005 mafisadi wanao sasa wakiamua kuuweka hadharani mkanda huo basi itakuwa patashika nguo kuchanika.

Hatafungwa fisadi yoyote wa Richmond wala wa EPA na baada ya yatakayojiri October 2010 kesi zote hizi zitafutwa ama watafungwa wale wasiokuwa na majina lakini mapapa wa ufisadi wataendelea kupeta tu!
 

Tumeshaona mawaziri na vigogo wako Mahakamani kwa sasa na kila ataekuwa na hatia atakwenda mahakamani. Hakuna ataenusurika.

Huna aibu, kusema JMK kaingia Ikulu kwa kubebwa na mafisadi? au habari ya kuwa JMK alikuwa aingie Ikulu toka 1995 huijui? na akafanyiwa Roho mbaya na Nyerere na akamuweka Mkapa ili amalizie agenda za siri!

Kama hilo hulijui utakuwa ni mtu wa kushangaza sana.
 
JMK sio Dikteta wala mtu wa kukurupuka kama alivyokuwa Nyerere, kila mwenye kosa atashughulikiwa systematically na hakuna atae escape, its a matter of time.

Bora hata Nyerere alikuwa dikteta lakini hakuiuza nchi kwa wageni au kuiacha nchi ikielekea pabaya huku akiwa kimya na siku zote maamuzi yake yaliweka mbele maslahi ya Watanzania na Tanzania. Hata Viongozi wa dini wameamua kusema sasa maana wanaona mwelekeo wa nchi ni wa kutisha.
 

Huo ni usanii tu. Siyo siri mapapa akina Rostam, Subhash Patel, Manji, Jeetu na wengineo ambao ni mapapa walichangisha mabilioni yaliyotumika kuwanunua wajumbe. Hulijui hili wewe!? Uliza utaambiwa! Unafikiri kwanini wote hawa hawaguswi pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha dhidi yaokuhusu ufisadi!?
 

Nakubaliana na wewe Nyerere hakuiuza nchi, Nyerere kaiuwa nchi, katika kipindi chake. Na kaigawa bure. Unajuwa kuwa leo Tanzania ni nani anaehodhi Ardhi kubwa kuliko mwengine yeyote? wa kwanza ni Kanisa!, Kanisa Katoliki, walipewa na nani bure hiyo Ardhi? wakati Kanisa Katoliki ni Nchi na Makao yake Makuu ni Vatican na ina ubalozi wake hapa Tanzania. au hilo hulijui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…