Korea yanunua ardhi "kwa mkopo" Tanzania, Serikali yasita kuthibitisha

Korea yanunua ardhi "kwa mkopo" Tanzania, Serikali yasita kuthibitisha

Wana JF,

tujadili namna ambavyo uwekezaji katika kilimo, uwe wa ndani au wa nje, unavyoweza kufanywa ili kuinua uchumi wa Taifa hili, linaloagiza mchele toka Pakistani,juisi toka Uarabuni, na toothpick toka Uchina.

Naona taa za barabarani na Nyerere vinachukua mkondo taratiibu, huku ardhi ikiendelea kuwepo bila kulimwa, na maji yakiingia baharini pasi na kutumika.

Mijadala yetu inatoa taswira ya viongozi wajao...tukitoa pumba, tutakuwa viongozi vilaza, tukijadili kwa umahiri, na kutoa mawazo mbadala, tutakuwa viongozi tutakaoleta mapinduzi...
 
Last edited:
kajenga UDSM
na kukusomesha bure wewe na viongozi walioko sasa madarakani
hiyo ndio inaitwa long term planning (kawasomesha bure badala ya kufanya kazi kwa bidii mnaendelea kuiibia taifa letu)

Mkuu Semilong hawalioni hilo! Nyerere alikuwa ni jabari bwana kamwe hawezi kulinganishwa na akina Mwinyi, Mkapa wala Kikwete. Chini ya uongozi wake Tanzania iliweza kufanya mengi sana pamoja na kupigwa vita sana na nchi za magharibi ukilinganisha na yaliyofanywa na Mwinyi, Mkapa na Kikwere combined. Leo hii Wasomi wa Kitanzania wanaofanya kazi katika nchi mbali mbali duniani wanatokana na sera za Mwalimu. Kama binadamu na Kiongozi Mwalimu hakuwa perfect alifanya makosa yake na hata yeye mwenyewe alilisema hilo lakini makosa yake ni madogo sana ukilinganisha na mazuri mengi aliyoyafanya alipokuwa madarakani. Mwacheni Mwalimu apumzike kwa amani~RIP Mwalimu.
 
It is a different ways of viewing things. Mie jambo hili sina tatizo nalo ikiwa tunafanya mambo kwa maslahi ya nchi na watu wake. Bahati mbaya sana hali haiko hivyo ndo maana kwa kila hoja watu wanakuwa na wasiwasi.

Tuna ardhi kubwa kwa muda mrefu. Tumeshindwa kuitumia to our own advantage. Tunaweza kuikodisha ardhi hiyo kwa watakaoitumia na sisi tule rent. Pengine hiki ndiyo kinachotufaa. Ikiwa thinking iko hivyo hawa watu tutawatoza rent ambayo ni commercial. Tuweke kabisa policy ya kukodisha ardhi yetu commercially kwa wanaotaka kuitumia hapa sitakuwa na shida, kwani policy itakuwa debated na hatimaye sheria zitatungwa.

Kwa mfano, mimi nina kieneo changu hapa mjini ambacho nimejenga kibanda changu cha kuishi. Sifanyii biashara yoyote. Eneo lile ni wastani wa meta za mraba 2,600. Kodi kwa mwaka nalipia jumla ya shilingi 26,000 kwa mwaka kama land rent (nenda wizara ya ardhi ukathibitishe). Hii ni kiwango cha karibu shilingi 10 kwa kila meta moja ya mraba.

Sasa kwa hawa watu wa nje (wawe wakorea, waarabu au wazungu) tuwakodishe kwa viwango hivyo hivyo! Eneo hilo linalosemwa yaani kilomita za mraba 1,000 ni sawa na mita za mraba Billion moja kwani kila kilomita ya mraba moja, ina mita za mraba milioni moja (1,000,000). Sasa hawa wakorea tukiwakodisha kwa kiwango sawa na hiki ninacholipa mimi cha karibu shilingi 10 kwa mita moja ya mraba, hapa tumeshapata jumla ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka (karibu Dola milioni 8).

Lakini hawa wanaitumia ardhi hii kwa kilimo cha kibiashara. Kwa hiyo kodi yao iwe ni ya kibiashara angalau shilingi 100 tu kwa meta moja ya mraba. Tutapata kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa mwaka. Fedha hizi zikiingizwa kwenye subsidies kwa wakulima wa Tanzania (kwenye mbolea, madawa na zana za kilimo) tuna uhakika wa kuwa kilimo chetu kitakuwa kimepona for good.

Tanzania tuna ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo, zaidi ya kilomita 250,000 za mraba. Hata tukikodisha kilomita 50,000 tu za mraba tutapata Zaidi ya Dola bilioni nne. Fedha hizi zitatosha kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda tunayoota ndoto kuyapata. Tunahitaji a different way of thinking!

Ikiwa ardhi ina thamani kihivyo, kwa nini tusikodishe tukala rent?? Tatizo tutawapa ardhi bure kwa ahadi kuwa tutaajiriwa mashambani na kukuza uchumi. Hata kodi hizi tunazowakandamiza watanzania WAGENI HAWAZILIPI!!! HILI NDO TATIZO LETU!!

Hiyo mentality inatuponza kwa nini tukodishe badala ya sisi wenyewe kulima, kuna ugumu gani jamani kulima sisi wenyewe mbona babu zetu wamekuwa wakilima miaka nenda miaka rudi bila GPS, setelite utabiri wa hali ya hela sisi tunashindwa nini na elimu tuliyonayo. Sio hoyo tu resources zipo nyingi tu we have never been serious i can tell you.

Ona mentality ya namna hii, viwanja tunavyo katikati ya mji badala ya NHC kwenda kuomba mkopo benki ili wajenge nyumba wao wanaingia ubia na mtu ambaye hana hela anenda kuomba mkopo kutumia title hiyi hiyo ya NHC anapewa mkopo anajenga at the end of the day sharing ni 75 kwa mwekezaji na 25 kwa NHC. Why this kind of arrangement wakati NHC wangepata mkopo toka benki yoyote na governement guarantee wangepata.

Tatizo letu ni dhana kuwa sisi hatuwezi mpaka tusaidiwe which is not true,

ardhi ni mali yetu, tuitumie sisi wenyewe tanzania ni nchi pekee amabayo ardhi anapewa mtu yoyote hata mgeni na kuacha mzawa akiwa hana ardhi, tunakwenda wapi.
 
Na kipindi cha Al Haj Mwinyi jee? Nadhani bila shaka utasema barabara, mataa ya kuongoza magari, mataa ya barabarani, ma-parking meters ya uhindini na ustawi wa Waswahili kwa ujumla yooote yalikuwa tambarare kwa mbele hadi alipoingia Mkapa na kuvuruga kila kitu kama kawa...halafu, alhamdulilaaah, kwa nguvu za Mwenyeez Alaah, akaja Kikwete ambaye tena akanyoosha mambo, au siyo?!

Na atakapoondoka JMK mataa yote yatazima na parking meta kuchakaa unless aje Mswahilina mwengine.
 
Nipeleke kwenye mahakama zilizojaa usanii! Hizo kesi za EPA, Richmond nanga inapaa ufisadi wa Mkapa kujiuzia nyumba za serikali na mawaziri wake na mgodi wa Kiwira bado wanajitahidi kupulizia kadri wanavyoweza. Rostam na utapeli wake wa Richmond/Dowans hadi leo hajaguswa. Utapeli wa kununua rada ya kifisadi na kuna ushahidi wa kutosha kwamba Chenge Vijisenti na Idrissa Rashid walipokea rushwa katika ununuzi ule bado wahusika wanapeta uraiani. Yule Vethlani alikuwa anahojiwa na vyombo vya dola badala ya kumuweka rumande wakati anavisaidia vyombo vya dola katika uchunguzi wao, lakini wakampa upenyo makusudi ili asiwachome vingunge wahusika aliokula nao zile $12 millioni.

Sasa huu ufisadi wa kuingia Ikulu 2005 ndiyo unadhani utashughulikiwa na hizi mahakama za kishkaji!!? Huoni kama hapa kuna pattern ya kuficha kila madhambi yanayowahusu mafisadi!? Au na wewe ni mmoja mafisadi hao huoni dhambi zozote!? Acha hizo za kutaka kuufumbia macho ukweli uliojidhihirisha.

Mkuu Bubu Ataka Kusema, naona jamaa ametonesha kidonda! Unampa 'live' bila kumung'unya maneno. Ndivyo inavyotakiwa.

Amandla......
 
..ondoa uwendawazimu wako,hiyo bure pesa katoa mfukoni mwake au ni kodi ya wananchi na madeni tunayoyalipia mpaka leo,
kazi ya kiongozi ni kutumia kodi za wananchi kwa ajili ya maendeleo ya taifa. kama kodi haitoshi anaweza hata kukopa. Akitumia kodi zetu vizuri tunamsifia, akitumia vibaya tunamshutumu.

bora zile shule angewaachia hao wakoloni waziendeshe wenyewe na ajenge za kwake ndio uongee hizo pumba zako!
unategemea raisi ajenge shule zake kutokana na hela zake nadhani hii ndio pumba
na kama unamaanisha raisi ajenge shule nyingine kwa kutumia kodi zetu hii inaonyesha uwendawazimu wako, kwa ajili mwazo umelalamika anatumia kodi zetu halafu mwisho unashauri atumie kodi zetu
 
Laiti ungallijuwa history ya UDSM, usingesema hayo.

Wakati mimi nasoma kulikuwa na ada ya Shillingi 33 kwa mwaka au Shillingi 11 kwa term (primary), baada ya hapo nikaenda kusoma nje ya Tanzania, si kwa fedha za Serikali. Kumbuka, enzi hizo za ubepari (Kabla ya Azimio la Arusha), kama ilivyo tena sasa, ilikuwa ni sifa kwa watu wa Dar Es Salaam kupeleka watoto wao Ulaya kwenda kupata masomo zaidi, kama vile ilivyokuwa kwa nyinyi wa bara kuletwa hapa Dar.

Waliosomeshwa bure na Nyerere nadhani unawajuwa, kwa kuchaguliwa na vigezo vya kuchaguliwa nadhani unavijuwa.

dsm
inaonekana wazazi wako walikuwa na uwezo wa kukupeleka nje kusoma, mimi naongelea wa TZ ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kuwasomesha.

kutokana na wazazi wako kuwa na uwezo wa kukusomesha nje inamaanisha walikuwa ni watu wazito + ukijumlisha na chuki ulizokuwa nazo dhidi ya nyerere = najiuliza sijui wazazi wako waligombana nini na nyerere!!!!

basi kama hutaki UDSM nakupa TAZARA
 
....ushaanza mambo yako tena. Leo hii tunaongelea Wakorea, hawa watu hawana dini za kishabiki shabiki tulizozoea sisi mkuu!! Ardhi ya Watanzania kwanza, mambo ya Imani baadae!

Huo ndio ukweli, baada ya Serikali na hifadhi za Taifa, hakuna mwenye Ardhi kubwa Tanzania zaidi ya Vatican aka Kanisa Katoliki. Sasa nimeanza nini na hivyo ndivyo ilivyo!
 
Sawa, nikubaliane nawe kuwa Mwl. aliondoa taa mabarabarani, kunyofoa parking meters na kuziba mifereji. Maana hayupo hapa kuweza kujitetea. Lakini kuvirudisha vitu kama hivi inahitaji miaka mingapi, 20, 30, au?!!

Mapato tu pekee ya pale stand ya mabasi ubungo kama yangelikuwa yanasimamiwa ipasavyo na kwenda kwenye mfuko wa halmashauri, leo hii tungelikuwa na maUDA na hizo parking meters zingelikuwa operational mpaka Kawe Tangini. Lakini cha kushangaza hao unaowataja kama visionaries wa jiji, wengi wako implicated kwenye scandals kubwa za ufisadi. Na kwa pale Ubungo, hata ripoti ya CAG inasema kuna ubadhirifu.

Kingine unachosahau ni vita vya NDULI. Bila jitihada za wanabara na jemedari Nyerere leo hii hapo Kigamboni huchelewi kukuta watu wangelikuwa wanaongea Kiganda kama lugha ya Taifa. Backing ya Shekh Gadaffi kwa Nduli ndiyo uilaumu, kwani gharama za kumwondoa Nduli na kuhakikisha hela yetu inabakia stable iliongezeka. Bila yeye mpambano usingechukua muda mrefu. Sasa hapa ni mambo ya priority. Je, ungelipendelea lipi - Kulazimishwa kuongea Kiganda na Nduli na kuacha kuongea Kizaramo? Kuhakikisha ukabila unasambaratishwa kwa kufanya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa au kuwa na parking meters?!

It took Nyerere 30 Years ku haribu kila kinachofanya kazi Tanzania. It may ta ke a long time kuirudisha kama ilivyokuwa na it will take longer kuiboresha kwani waswahili hunena ''kubomoa ni rahisi lakini kujenga...).

Hayo ya Nyerere na Idi Amin, wala usiyalete, sio mahala pake hapa. Kwako Idi Amin ni Nduli kwanguu ni Shujaa aliechangiwa na nchi zinazoongozwa na wakiristo kumuondoa madarakani kwa kuwa ni muIslam. Usitake tubadili mada, naomba ya Idi Amin humu tusiyalete tuyatafutie thread nyingine ikibidi.

Kiswahili, kilikuwepo kabla ya Nyerere kikiongewa si tu, Tanganyika bali mpaka Kongo na kwingineko kwingi. Ukitaka kujuwa waliekieneza kiswahili, rejea historia na utazame wapi kiswahili kimetoka na ilikuwaje kikafika kilikofika.

Niambie, Tanzania tulikuwa na Nyerere miaka 30, tumepigana vita ngapi na niambie miaka 30 kabla ya Nyerere tumepigana vita ngapi na miaka 30 baada ya Nyerere tumepigana vita ngapi?

Ukipata jibu za statiscs hizo utaelewa alikuwa ni kiongozi aina gani.
 
Nipeleke kwenye mahakama zilizojaa usanii! Hizo kesi za EPA, Richmond nanga inapaa ufisadi wa Mkapa kujiuzia nyumba za serikali na mawaziri wake na mgodi wa Kiwira bado wanajitahidi kupulizia kadri wanavyoweza. Rostam na utapeli wake wa Richmond/Dowans hadi leo hajaguswa. Utapeli wa kununua rada ya kifisadi na kuna ushahidi wa kutosha kwamba Chenge Vijisenti na Idrissa Rashid walipokea rushwa katika ununuzi ule bado wahusika wanapeta uraiani. Yule Vethlani alikuwa anahojiwa na vyombo vya dola badala ya kumuweka rumande wakati anavisaidia vyombo vya dola katika uchunguzi wao, lakini wakampa upenyo makusudi ili asiwachome vingunge wahusika aliokula nao zile $12 millioni.

Sasa huu ufisadi wa kuingia Ikulu 2005 ndiyo unadhani utashughulikiwa na hizi mahakama za kishkaji!!? Huoni kama hapa kuna pattern ya kuficha kila madhambi yanayowahusu mafisadi!? Au na wewe ni mmoja mafisadi hao huoni dhambi zozote!? Acha hizo za kutaka kuufumbia macho ukweli uliojidhihirisha.

Kuna mahakama za Rushwa za kimataifa kama za Tanzania huziamini, unangoja nini?
 
Baada ya kuona taarifa za Korea Kusini kutaka kuhodhi eneo kubwa la ardhi nchini Tanzania kwa ajili ya kuendesha kilimo kukidhi mahitaji ya matumbo ya raia wake, nime-search online kwa dakika kumi nimegundua madudu ya kumwaga!

Viongozi kuanzia aliyeko Ikulu mpaka mwenyekiti wa kijiji wanafumbia macho dhuluma ya ardhi kwa wananchi masikini wasioweza kuchanganua faida na hasara za kuachia wageni kutoka nje ya Tanzania kukwapua ardhi yetu ( land grabbing) - ukoloni umerudi kwa lugha tofauti.

Ukweli ni kwamba, we have been too lenient kwa mkuu wa nchi Jakaya Kikwete, kiasi kwamba haoni sababu ya kuzuia huu uozo chini ya utawala wake. Kikwete kama rais ana jukumu la kulinda maslahi ya usalama wa taifa la Tanzania, na ardhi pamoja na nishati ni maswala yaliyo juu katika kusimamia usalama wa nchi.

Kwanini kiongozi huyu anashindwa kupiga marufuku hii dhuluma? Anaweza kutumia madaraka yake kutoa agizo la rais au kwa kutunga sheria mpya katika bunge kudhibiti umiliki wa ardhi kwa wageni? Kuwa rais ni kazi ngumu, hiki ni kipimo, si kila anayeomba anaweza kuongoza. Na kuongoza siyo kufungua miradi na kuhudhuria harusi na misiba, au kwenda UN kuhutubia. Leadership ya nchi kitu kingine kabisa.

Rais anaona fahari kufunga barabara zinazozunguka Ikulu yake, lakini haoni sababu ya kudhibiti ardhi ya wananchi anaowaongozwa isiporwe na mabepari wa kigeni.

Tayari tunafahamu kuna makampuni kadhaa ya kigeni yameshanunua au yako mbioni kununua kiasi kikubwa cha ardhi ya kilimo - ni serikali ndiyo inawakaribisha kwa kisingizio cha uwekezaji. Hawa wageni hawawezi kuja kisha wakaanza kujipimia land. Tutakuja kulaumiana baadaye, lakini bora tuyaseme tupate ufumbuzi sasa.

Hapa chini naorodhesha links za baadhi ya madudu yanayofanywa kwenye ardhi yetu na hakuna anayekemea. Land grabbing business ventures are taking place Tanzania, it's real. We got to act now, we can't stand by and just watch, tuseme ardhi yetu is not for sale kwa wageni. Haiozi, tuiache mpaka watanzania watakapopata mtaji na maarifa ya kuitumia wenyewe - waliotangulia wangeiuza kwa wageni sisi tungekuwa wapi?

Huenda si habari mpya, lakini inaonyesha msimamo wa serikali ni uza uza uza!!!!

Dhuluma ya ardhi Tanzania

Swedish neo-colonialism or Tanzania's savior?

Hawa ndiyo SEKAB wenyewe, wanaomba ardhi bure Rufiji

Tanzania Govt On Spot Over Biofuel Production

Sun Biofuels Tanzania Ltd
 
Kuna mahakama za Rushwa za kimataifa kama za Tanzania huziamini, unangoja nini?

Ha ha ha ha naona umefilisika kimawazo! Kuna haja gani basi ya kuwa na mahakama Tanzania kama haziwezi kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa!? Si bora tu wazifunge na kuwapunguzia gharama walipa kodi kwa kujua kwamba mahakama hizo zimeshindwa kazi na wahalifu wote ndani ya nchi yetu wakashtakiwe kwenye mahakama za kimataifa. Jumamosi njema 🙂
 
Niambie, Tanzania tulikuwa na Nyerere miaka 30, tumepigana vita ngapi na niambie miaka 30 kabla ya Nyerere tumepigana vita ngapi na miaka 30 baada ya Nyerere tumepigana vita ngapi?

QUOTE]

unajua kuhesabu kweli? halafu Tanzania miaka 30 kabla ya Nyerere ni Tanzania ya watu gani hiyo? Na kweli ungetaka turudishe tulivyokuwa miaka 30 kabla ya Nyerere?
 
Nyerere, aliikuta Dar Es Salaam nzuri kama mtoto, na kama ilivyo.Hakuna alichokiongeza wala kuwa na nadharia ya kuongeza. Uozo wa Dar Es Salaam wa hivi sasa unatokana na huko nyuma (Kwa Nyerere). Na Dar Es Salaam ilianza kuharibika wakati wa Nyerere. Tuulize sisi tuliozaliwa na kukulia hapa tukueleze! Hakuna muundo mbinu mpaya wowote alioufanya Nyerere Dar Es Salaam utaozidi asilimia moja ya aliyoyakuta.

Labda ni wewe huijui historia ya Dar Es Salaam. Ukiacha sehemu zilizojulikana kama Uzunguni ama Uhindini, sehemu kubwa ya iliyojulikana kama Uswahilini wakati nchi inapata uhuru mwaka 1961, Ilala, Magomeni, Mwananyamala na kwingineko zilisheheni nyumba za makuti na hazikuwa na barabara za lami.

Mwaka mmoja tu baada ya nchi yetu kupata uhuru, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilianzishwa ili kusaidia upatikanaji wa nyumba bora za makazi, hasa mijini. Baada tu ya Shirika kuanzishwa, Serikali ilikuwa inatoa ruzuku kwa Shirika ili kuliwezesha kujenga nyumba nyingi kadri ilivyowezekana. Kwa kutumia ruzuku hiyo, Shirika liliweza kuondoa nyumba za makuti (slum clearance), hasa jijini Dar es Salaam na kujenga nyumba za saruji na kuezekwa kwa mabati.

Hivyo ndivyo zilivyojengwa nyumba za Ilala, Magomeni, Mwananyamala. Ujenzi kama huo ulienea pia kwenye miji yote ya mikoa na wilaya nchini. Ni wakati huo huo wa "operation makuti" barabara zote katika sehemu hizo (Ilala, Magomeni na Mwananyamala) ziliwekewa lami. Kabla ya hapo sura ya jiji la Dar es Salama na hasa zile sehemu za uswahilini hazikuwa tofauti na yale mabanda tunayoyashuhudia hadi leo sehemu nyingi za mkoa wa pwani.
 
Mag3,
Uongo huumbuliwa na ukweli. Huyu Darisalama chuki zake kwa Nyerere ndizo zinazomwongoza kusukumiza uwongo na kubadilisha ukweli. Kuna thread aliongopa kuwa msikiti wa Butiama ulijengwa baada ya kifo cha Nyerere wakati mimi niliuona nilipokwenda kule kwa mazishi Oktoba 1999.
Jamani tusipofushwe na chuki.
 
Nafikiri huyu Governor wao ana make sense kidogo,lakini ukweli kilimo cha peasant hakiwezi kuondoa umaskini,nafikiri kilimo kwa TZ kina weza kuondoa umaskini zaidi ya utalii na madini lakini lazima kuwatumia watu wanaojua kilimo,Zimbabwe ilikuwa haina kitu zaidi ya hawa commercial farmers ambao walikuwa ndio wanaendesha uchumi wa nchi na kwa waliofika harare kabla ya Mugabe kuiharibu atakubali jamaa walikuwa tofauti na nchi zilizoendelea/states...tuna ardhi nzuri sana mikoa ya kusini ya kuweza kuondoa njaa na kuweza kuuza nje na kutoa ajira kwa mamilioni lakini lazima kama tuna taka tushirikiane na serious investors sio blah blah za kina Richmond!
Koba,
Mkuu wangu weee. nenda Harare leo ukaone maduka yalivyojaa vyakula..Uliza watu wanaokwenda Zimbabwe utaambiwa story tofauti kabisa na ile ya mwaka jana.. Sasa tuseme Wazimbabwe wamejua kulima baada ya kupatanishwa?..Hivi kweli ktk akili zenu mliamini kabisa kwamba Wazimbabwe weusi ndio tatizo la production ya chukula nchini humo?..mkiamini kabisa kuwa commercial farmer ni wazungu lakini kilichokosekana ni chakula, hivyo weusi ndio wa kulaumiwa kutokuwa commercial farmer... yaani hata sielewi lugha hii!..

Ni lini mtakuja elewa mkuu wa ngu kwamba hii Bongo yetu kesho tukisha fungiwa tu kuagiza mbegu kutoka nje tutakwisha within 2 years kwa sababu leo kwa umaskini wetu tunakula hadi mbegu... Nenda madukani katazame mchele unaouzwa, ingia supermarket unambie ni vitu vingapi tunazalisha nchini..
Supplier wa chakula na maduka Zimbabwe ni mzungu mtu kama Bakhrezsa sasa nambie Bakhresa na Mohammed Interprise waache kuagiza na ku supply chakula na mafuta tutakuwa ktk nafasi gani? walanguzi wanzungu wasinunue korosho na mazao yetu..
Yaani kifupi siku waarabu na wahindi nchini wakigoma na kupata support ya nje tumekwisha... Hivi sasa nakwambia hatuwapati Zimbabwe hata kwa chembe.. ni kiasi cha wao ku recover tu na pengine wame learn from their mistakes!...
 
Mag3,
Uongo huumbuliwa na ukweli. Huyu Darisalama chuki zake kwa Nyerere ndizo zinazomwongoza kusukumiza uwongo na kubadilisha ukweli. Kuna thread aliongopa kuwa msikiti wa Butiama ulijengwa baada ya kifo cha Nyerere wakati mimi niliuona nilipokwenda kule kwa mazishi Oktoba 1999.
Jamani tusipofushwe na chuki.

Huyu Dar Es Salaam ama ni mtoto mdogo mtukutu au ni limbukeni asiyejua lolote kuhusu historia ya Tanzania. Lakini lazima atambue kuwa humu tupo ambao hatukusimuliwa, tuliyashuhudia kwa macho yetu. Kuna wakati iliyojulikana kana Magomeni Makuti haikuwa na nyumba hata moja ya bati. Mwaka 1964, barabara karibu zote za Magomeni Mapipa zilikuwa za lami tupu na nakumbuka tulivyojivunia mitaa ile kama ya Idrissa, Uweje na kahoteli ketu ka Butiama. Naomba huyu anayejiita Dar es Salaam mumwelewe kama alivyo - ni limbukeni.
 
Mag3,
Uongo huumbuliwa na ukweli. Huyu Darisalama chuki zake kwa Nyerere ndizo zinazomwongoza kusukumiza uwongo na kubadilisha ukweli. Kuna thread aliongopa kuwa msikiti wa Butiama ulijengwa baada ya kifo cha Nyerere wakati mimi niliuona nilipokwenda kule kwa mazishi Oktoba 1999.
Jamani tusipofushwe na chuki.

Mkuu Jasusi
Huyu darislama ni mpuuzi sana na hoja zake za udini kila mara kiasi kwamba hawezi kuona ukweli hata mara moja .
 
Niambie, Tanzania tulikuwa na Nyerere miaka 30, tumepigana vita ngapi na niambie miaka 30 kabla ya Nyerere tumepigana vita ngapi na miaka 30 baada ya Nyerere tumepigana vita ngapi?

QUOTE]

unajua kuhesabu kweli? halafu Tanzania miaka 30 kabla ya Nyerere ni Tanzania ya watu gani hiyo? Na kweli ungetaka turudishe tulivyokuwa miaka 30 kabla ya Nyerere?

Of course, utakapopata jibu ndio utajuwa speed iliyomchukuwa kuimaliza nchi
 
Back
Top Bottom