Tatizo letu wengi hatujui maana ya neno ukoloni hivi jamamani tunaweza pata mtu akazungumzia defination ya ukoloni in very simple language labda watu wataelewa.
Watu wanadhania ukoloni ni bendera ya mkoloni ipepee kila mahali, wengine wanadhania ni magwanda na makofia ya PC na DC na au office attendant kuitwa messenger, wengine wanadhania ni kodi ya kichwa na baiskeli, lakini majority hawajui hii concept ya ukoloni.
Naomba mdau mmoja atueleze maana ya ukoloni
Naweza kusema UKOLONI ni hali ya mtu au kikundi cha watu wanaowakilisha matakwa ya taifa fulani lenye nguvu (kiuchumi, kijamii, kisiasa ma kiutamaduni) kulaghai wakuu wa taifa lingine (lenye raslimali zenye maslahi kwa taifa lao) au kutumia nguvu kuzimiliki au kuendelea kuzimiliki kwa manufaa yao.
Mfano, mikataba iliyofanywa na akina Karl Peters zamani kati yao na watemi wetu, inafanywa leo pia kati ya mabalozi/mawaziri au wakuu wa nchi zenye nguvu na viongozi wetu kwa lengo lilelile ila katika mazingira mapya.
Ndiyo maana unaona wananchi wanahamishwa kwa nguvu ili kumpisha mwekezaji fulani amiliki ile ardhi bila ya wao kushirikishwa. Kama wakati wa Nyerere tulishindwa kilimo cha Wachina, leo tutaweza kilimo cha Wakorea Kusini, Wahindi, Waindonesia nk? Matokeo yake Watz walio wengi watakosa ardhi hapo baadaye na watakuwa na maisha duni zaidi ya wananchi wa Zimbabwe.
Halafu kwa hapo baadaye atakuja mtawala atakayesema ana uchungu na watu wake ataanzisha sera za kuwanyang'anya wageni hayo mashamba ili wapewe wananchi na hali hiyo italeta mtafaruku mkubwa nchini kwani hao wawekezaji watakuwa wameishajiimarisha sana na pia watakuwa wameshatenga maeneo ambako watu wa kawaida watakuwa hawaruhusiwi kwenda kwa kisingizio cha kuzuia kuiba mali zao! Hii ndiyo 'prophesy' yangu kutokana na hali ninaoona inaendelea hapa nchini.