Baada ya kuona taarifa za Korea Kusini kutaka kuhodhi eneo kubwa la ardhi nchini Tanzania kwa ajili ya kuendesha kilimo kukidhi mahitaji ya matumbo ya raia wake, nime-search online kwa dakika kumi nimegundua madudu ya kumwaga!
Viongozi kuanzia aliyeko Ikulu mpaka mwenyekiti wa kijiji wanafumbia macho dhuluma ya ardhi kwa wananchi masikini wasioweza kuchanganua faida na hasara za kuachia wageni kutoka nje ya Tanzania kukwapua ardhi yetu ( land grabbing) - ukoloni umerudi kwa lugha tofauti.
Ukweli ni kwamba, we have been too lenient kwa mkuu wa nchi Jakaya Kikwete, kiasi kwamba haoni sababu ya kuzuia huu uozo chini ya utawala wake. Kikwete kama rais ana jukumu la kulinda maslahi ya usalama wa taifa la Tanzania, na ardhi pamoja na nishati ni maswala yaliyo juu katika kusimamia usalama wa nchi.
Kwanini kiongozi huyu anashindwa kupiga marufuku hii dhuluma? Anaweza kutumia madaraka yake kutoa agizo la rais au kwa kutunga sheria mpya katika bunge kudhibiti umiliki wa ardhi kwa wageni? Kuwa rais ni kazi ngumu, hiki ni kipimo, si kila anayeomba anaweza kuongoza. Na kuongoza siyo kufungua miradi na kuhudhuria harusi na misiba, au kwenda UN kuhutubia. Leadership ya nchi kitu kingine kabisa.
Rais anaona fahari kufunga barabara zinazozunguka Ikulu yake, lakini haoni sababu ya kudhibiti ardhi ya wananchi anaowaongozwa isiporwe na mabepari wa kigeni.
Tayari tunafahamu kuna makampuni kadhaa ya kigeni yameshanunua au yako mbioni kununua kiasi kikubwa cha ardhi ya kilimo - ni serikali ndiyo inawakaribisha kwa kisingizio cha uwekezaji. Hawa wageni hawawezi kuja kisha wakaanza kujipimia land. Tutakuja kulaumiana baadaye, lakini bora tuyaseme tupate ufumbuzi sasa.
Hapa chini naorodhesha links za baadhi ya madudu yanayofanywa kwenye ardhi yetu na hakuna anayekemea. Land grabbing business ventures are taking place Tanzania, it's real. We got to act now, we can't stand by and just watch, tuseme ardhi yetu is not for sale kwa wageni. Haiozi, tuiache mpaka watanzania watakapopata mtaji na maarifa ya kuitumia wenyewe - waliotangulia wangeiuza kwa wageni sisi tungekuwa wapi?
Huenda si habari mpya, lakini inaonyesha msimamo wa serikali ni uza uza uza!!!!
Dhuluma ya ardhi Tanzania
Swedish neo-colonialism or Tanzania's savior?
Hawa ndiyo SEKAB wenyewe, wanaomba ardhi bure Rufiji
Tanzania Govt On Spot Over Biofuel Production
Sun Biofuels Tanzania Ltd