ndugu zangu, mabishano ya Nyerere aliweza au hakuweza hiyo ni historia. hivyo mnavyofanya mnawa-let down wale wanaowachukulia nyinyi kuwa mifano ya kuigwa. kwasasa, tunajua kilicho mbele yetu - kwanini ardhi yetu inaporwa? na tufanye nini kuzuia dhuluma hii?
Ardhi haiporwi, wa Korea wanawekeza katika ka kilimo, kuna mtu kaandika hapo juu kuonesha kuwa wanawekeza kwenye ardhi ya kilimo hata Urusi.
Leo hii sisi, ardhi safi tunayo, lakini ikifika wakati fulani fulani tunatangaziwa kutakuwa na tishio la njaa kwa kukosa mazao au kuna njaa, na inabidi hapo serikali ifanye jitihada za ziada, kama hapo nyuma kidoogo, alivyofanya JMK na kuahidi ''hafi'' mtu kwa njaa Tanzania.
Sasa, tuendelee na hii management ya kutatua tatizo linapotokea au tuchukuwe measures za makusudi za kufanya kila njia, za muda mrefu na mfupi kuhakikisha kuwa tunamaliza tatizo hili la njaa wakati wa kiangazi?
JMK anafanya linalostahiki, ameamuwa kuwekeza kwenye kilimo, ameamuwa kuwaita wawekezaji kwenye kilimo, ameamuwa kuongeza tija kwenye kilimo, kwa kutumia njia zote anazoziona zina/zitafaa, kwa muda mrefu na mfupi.
Baada ya yote hayo, anakuja mtu anasema wageni wanatupora ardhi, inashangaza sana hii!
Jena kuna mTanzania anaetaka ardhi ya kulima akanyimwa? Jee, kuna mTanzania atakae kuwekeza kwenye kilimo akanyimwa? jibu ni simply, hakuna. Jee, tuna Ardhi ya kilimo ya ukubwa gani ambayo haijaguswa mpaka sasa? jibu, ni nyingi sana. Jee, Ardhi hii tunayowapatia hawa wawekezaji wa ki Korea ambao kuna kila dalili inaonyesha kuwa tuna uwezo wa kukubaliana nao uwekezaji wao uwe na tija kwa mwanachi wa Tanzania, inawezekana tukafaidika? Ndio, tunaweza kujifunza mengi sana kutoka kwa hawa wawekezaji.
Ikumbukwe, tuliwakaribisha wa Canada kule Hanang, kutusaidia kilimo cha Ngano, kilifanikiwa sana, wakatuachia kila mashine ya kulima na kuvuna ngano kwa ustadi, wakatufundisha kwa miaka, tukawa na mashamba makubwa katika Afrika mashariki, ya ngano. Cha kustaajabisha ni kuwa, walipoondoka tu na kutuwachia wenyewe, kama kawaida yetu ya kuuwa kila kilicho cha umma, na haya mashamba na ma mashine na materekta na ma havesta na ma kombaina na majumba waliojenga na makarakana waliosimika na ujuzi waliotuachia, yote hayo tukashindwa kuyaendeleza, tukayaua. Leo hii, baadhi ya mashamba yale, wamepewa wa Kenya kuwekeza. Yana/tafanikiwa, kwa kuwa si ya umma, ni ya mashirika binafsi.
Sasa, tuwaache hawa wa korea wawekeze, na safari hii tuhakikishe wanawafundisha wakulima na mashirika (companies) ya wakulima binafsi, si umma tena, haya ya mali ya umma yalitushinda kabisaaaa. Wataweza na tutafanikiwa, ikiwa tu, tutaamsha bongo zetu zilizo lala, tuwe macho na yale makosa aliyokubali Nyerere kuyafanya, tusiyarudie sisi. Nyerere, wengi hawakumuelewa kukubali kwake makosa, kwa kuwa, wengi wetu hawana mantiki ya kupima maneno na wao ndio kwanza hujidai kuwa ndio wajuzi. Nyerere aliposema kashindwa, he meant it, na alikuwa akituambia tusirudie makosa. Leo, unapeleka mkono wa kushoto shimoni unagongwa na nyoka halafu unautowa unapeleka tena wa kulia?
Tuwape wa Korea, tuhakikishe, wanaweka research centres kwenye hayo mashamba na ziwe accessible na wa tanzania wote watapohitaji data, au kufanya reseach, of course kuwe na sheria fulani fulani isiwe holela tu.
Tuhakikishe wanachukuwa wa Tanzania kuwafundisha hapo mashambani, kila kazi zitazikuwepo, we can even agree with them, iwe wanachukuwa intake ya certain number of interns kwa kila shamba kwa fani tofauti zinahusika na kilimo. Tutafaidika.
Besides, wamesha sema nusu ya mazao yatabaki hapa hapa nchini. Hii pekee ni faida. Nauliza, haitopunguza shida ya njaa wakati wa kiangazi ikiwa ni mazaon ya chakula? jibu, itapunguza. Jee, hiyo nusu ya mazao ikiwa ni mazao ya mali ghafi za viwandani, haitotupatia kipato? jibu itatupatia. Jee, kuna faida ya kuiwacha ardhi tupu ya kilimo ikae wazi tu wakati kwa kuwa kwa sasa hatuna uwezo wa kuilima wenyewe na tukiikodisha au kuwapa wawekezaji kwa masharti yatayo tupa tija na faida, kwa nini tusifanye hivyo.
Sioni mantiki ya kusema wanatupora ardhi yetu! wanatupora wanaipeleka wapi? Korea?
Kama ulivyosema, nasema ya Nyerere tumwachie Nyerere, tutazame ya sasa, wapi tunatoka tunajuwa, wapi tulipo tunajuwa, jee wapi tunakwenda? KWA KUTAZAMA MAKOSA YA TULIPOTOKA, KUFANYA JITIHADA YA KUYAREKEBISHA HAPA TULIPO, BASI TUTAFIKA TUNAPOKWENDA KWA KASI YA AJABU.