Korogwe, Tanga: Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa

Korogwe, Tanga: Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
26,858
Reaction score
23,768
Inatisha... Kwa anayefahamu.

Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa​

Global Publishers Aug 11, 2021
article_image_1628677907280.jpeg

JESHI la Polisi mkoa wa Tanga linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kumshambulia na kumuua mtu mmoja aliyetuhumiwa kuiba pikipiki huko Korogwe.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga amesema marehemu alituhumiwa kuiba pikipiki Korogwe Tanga, Julai 27, mwaka huu na kutokomea nayo kusikojulikana.

Baada ya kufanya tukio hilo, Madereva bodaboda wa eneo aliloiba pikipiki hiyo wakaanza kumsaka ambapo baada ya siku chache walimkamata akiwa na pikipiki hiyo.

“Baada ya kumkamata walianza kumshambulia kwa vipigo kisha kumfunga kamba kwenye pikipiki na kuanza kumburuza barabarani (barabara ya vumbi). Hata hivyo, kutokana na majeraha makubwa aliyoyapa, mtu huyo alifariki dunia.

“Mpaka sasa tumewakamata watu 11 kwa kwa ajili ya uchunguzi na kuhusika na tukio hilo la kinyama. Uchuguzi ukikamilika tutawafikisha mahakamani,” amesema Chatanda.

Aidha, RPC Chatanda amewataka wananchi kutojichukulia hatua za kisheria mikononi kwani ni kuvunja sheria, hivyo iwapo kuna uhalifu basi waripoti katika vyombo vya sheria.
 
We ndo ungetuambia Chief. Siye tutajuaje? Ila inaonekana atakua mwizi then hao jamaa wamechukua sheria mkononi
 
Aisee kuna watu wana maamuzi magumu....
 
This is simply inhuman!Lazima uwe na genes za wanyama kufanya tukio la hivyo!
 
Inasadikika aliiba toyo na walipomkamata adhabu yake ikawa hiyo
 
Back
Top Bottom