Mwaka 2017 katika kijiwe chetu kwa kopa kuna mmoja aliibiwa pikipiki waliomuibia pikipiki walimtoboa macho jamaa na kuondoka na pikipiki.
Mwaka huo huo nyuma ya Victoria Service Station ya Ali Hassan Mwinyi Road kuna bodaboda wa kijiwe cha Victoria aliporwa pikipiki akaibiwa hesabu ya siku na kuumizwa.
Mwaka 2018 kuna dereva bajaji aliuawa na kuporwa bajaji eneo pa Uporoto ya Mwananyamala Bwawani.
Mwaka 2018 hiyo hiyo kuna dereva bodaboda alipigwa na kuibiwa pikipiki eneo hilo hilo la Uporoto.
Mwaka 2018 hiyo hiyo aliuawa jamaa aliyemleta dereva bajaji hilo eneo la Uporoto ili kumuibia bajaji. Aliokua nao walikimbia.
Mwaka 2018 mwanakijiwe aliibiwa pikipiki Sinza kwa kipigo.
Mwaka 2018 deiwaka alitapeliwa pikipiki kwa kudanganywa anagewa dili ya kusafirisha mirungi.
Mwaka 2019 mwanakijiwe aliibiwa pikipiki Keko at knife point huku wauza vitumbua na samaki wa hapo mtaani wakiangalia.
Hayo ni matukio ninayoweza kuyakumbuka kwa haraka ambayo yalihusisha kutishia uhai. Bodaboda wakiungana kumshughulikia mwizi kwa ambaye nishakua in action naelewa kwanini wanafanya hivyo.
Utakuta pikipiki wanaiba wako watatu au wanne. Wanaiuza kuanzia laki nne mpaka nane so kwa wastani wanapata laki mbili kwa tukio. Kama yeye yupo radhi kuua mtu ili apate laki mbili kwanini asiwe radhi kufa kwa laki mbili hiyo hiyo?
Bome-e