Korogwe, Tanga: Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa

Hizo njia za kumalizana na wezi kwa busara wamekuachia wewe,wao wametumia njia effective and efficient.
 
Wezi wa pikipiki wakikudaka wanakuua na kuchukua pikipiki...hao jamaa wako sawa kabisa sema wangemchoma moto tu
Najua kuna baadhi hawatokuelewa.
Ila niliwahi shuhudia mtu kakatwa kichwa na wezi hao wa bodaboda na kuuliwa na boda ikaibwa ....
so watu tusiangalie tu one side.
 
Mkuu mtu anapofanya tukio la wizi maana yake amejiandaa kwa outcome yeyote,hilo ni sawa!
Lakini
Ukifanya kama hao walivyofanya,unakuwa na tofauti gani na wao?
Tuishi kwa taratibu tulizojiwekea na si kuchukua sheria mkononi!Madhara ya kuchukua sheria mkononi ni makubwa sana kuliko faida zake!
Nikipata nafasi nitakueleza namna mwanafunzi mwenzangu alivyouwawa hostel za mabibo kwa kuitiwa mwizi na mpenzi wake aliyemfumani!
 
Mfanyabiashara ukidhulumiwa halafu ukamuua aliyekudhulumu unakua umetoa bold statement kwa mwingine atakayewazia kukudhulumu.

Madereva wa bodaboda wanachofanya hapo ni kutoa statement kwa wezi wengine waliobakia.
 
Hata kama wanafanya hivyo,huwezi kufanya kitendo cha namna hiyo kwa binadamu mwenzako!
Lazima utakuwa hauko sawa kichwani!
Kumpiga nondo na kumuua mwenye bodaboda wewe unaona sawa Ila akikamatwa wewe unamtetea, utakuwa mmoja wa wapiga nondo wewe.
 
Wapewe onyo na kuachiwa huru ukatili wa wezi wa bodaboda unatisha jinsi wanavyowafanyia wanaowapora

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Korogwe ndy zao
Kuna wakati fulani
Kuna jamaa mmja alikuwa
Anaitwa restaurant alikuwa ananunua
Pikipiki za wizi aliwekaga kituo hapo
Jamaa hko walimpigia kibiriti

Ova
 
Kumpiga nondo na kumuua mwenye bodaboda wewe unaona sawa Ila akikamatwa wewe unamtetea, utakuwa mmoja wa wapiga nondo wewe.
Kipi kinakufanya uwe binadamu na kipi kinakufanya uwe mnyama?
Ukifanya hayo,unakuwa na tofauti gani na wao?
Kwa ujinga wao,wanaenda kuozea jela!Tusipende kuchukua sheria mkononi maana madhara yake ni makubwa!
 
Najua kuna baadhi hawatokuelewa.
Ila niliwahi shuhudia mtu kakatwa kichwa na wezi hao wa bodaboda na kuuliwa na boda ikaibwa ....
so watu tusiangalie tu one side.
Ni kweli wanatenda hayo,sasa ukilipa huo unyama na wewe si unakuwa kama wao tu?
Ona sasa wanaenda kuozea jela!Hasara kwa nani?Familia zao zinabaki zinateseka kwa kuendeshwa na mihemko!
 
Tofauti yako na wao inakua wapi hapo?
Nimeshaibiwa sana na wameniingiza hasara sana tu. Lakini kumuua au kumburuza mtu kiasi hicho hadi mauti imkute sio jambo la kufurahia.
Wewe ni mwizi mwenzao bila shaka
 
Acha ujinga pumbavu wezi wakubwa nyie. Dawa yenu kuwaua tu
 
Vibya sana. Hata kama wameibiwa pikipiki, kumburuza mwizi namna ile sio sana hata!
Acha ujinga wewe. Wenyewe wanavowachinja bodaboda na kupora pikipiki unaona sawa tu.
Wewe ni mwizi mwenzao?
 
Acha ujinga pumbavu wezi wakubwa nyie. Dawa yenu kuwaua tu
Mwizi mama yako!!sasa kawatoe huko jela, vijana wadogo miaka 20s' sasa ndio basi tena, na kama hakuwa na mtoto ndio imetoka hiyo?!!kwanza wiki hizi mbili umeshawaona walivyo huko mahabusu??kweli ile kauli ya RPC, kuwa watasimulia, nimeiamini, madogo wametepeta, ile mbaya, sijui kama hata watafika kwenye hukumu yao!!!
 
Kuna rafiki yangu Mwanza walimvamia nyumbani kwake. Wakamkata mapanga vibaya sana, mwanae mmoja akauawa kwa mapanga, kisha wakaingia ndani na kuchukua fedha zote zilizokuwemo. Jamaa mpaka leo ni mlemavu. Alivoona hii video aliongea kama ulivoongea. Mtu kama hayajakutokea utakuwa na huruma lakini kama kimekukuta vizuri, sidhani kama utaongea habari ya ubinadamu maana wao wakija huo ubinadamu hawana.
 
Wewe ni mwizi mwenzao bila shaka

Afadhali umeweka neno bila shaka.
Huwezi kujua kama na mimi ni mwenzao ila narudia tena, kumfanyia binadamu kitendo cha aina hiyo ni zaidi ya unyama.

Mie ni muhanga mzoefu wa wezi lakini kamwe siwezi buruza binadamu hadi akate roho. Si umeona wameishia kufungwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…