Korogwe: Watu 6 wafariki Dunia, 19 wajeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka

Korogwe: Watu 6 wafariki Dunia, 19 wajeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
SITA WAFARIKI KWA AJALI TANGA.

Kutoka Tanga.

Watu sita wamefariki Dunia na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya gari waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea eneo la Kwamdulu ambapo gari aina ya Coastal yenye namba za usajili T833 DMH kuacha njia na kupinduka.

Kamanda Jongo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya Magunga Korogwe.Na majeruhi wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo.

Aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva hivyo kushindwa kukata kona na gari kutelezaa kisha kupinduka na wito Kwa watumiaji wa vyombo vya Moto barabarani kufuata sheria ili kuzuiya ajali zinazoweza kuepukika.

Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Dk Salma Swedi amethibitisha kupokea miili 6 na majaruhi 19 na kwamba majeruhi wawili hali zao nii mbaya na wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa zaidi.

Mwambela.JPG
 
Dah! Pole nyingi kwa wafiwa. Madereva wa hizo Coaster wamekuwa na tabia ya kukimbiza sana hizo gari, na hasa wakitoka tu stendi ya Korogwe, kuelekea Tanga!

Mara nyingi huandikiwa faini na wale trafiki wa pale getini wakati gari inatoka nje ya stendi! Sasa baada ya kutoka hapo akili yake unakuta imevurugika kabisa! Atakimbiza gari weee! Mpaka akifika stendi ya Segera, ndiyo anarudi katika hali yake ya kawaida.
 
Usiku mwendo kasi huwa haufai, hasa kama barabara huna uzoefu nayo!
Utaweka full light, sawa, lakini kuna kona nyingine ni za ghafla mno.
Madereva wengi huwa wanaamua kunyoosha moja kwa moja porini!
 
 
Back
Top Bottom