Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

Kuugua so kufa...watu Ni lazima waugue ili miili ipate Kinga..if hutaki Hilo itakubidi uwafungie Hadi chanjo ipatikane..kitu ambacho so practical..
Well si magonjwa yote. Haswa kwa virus wanatabia ya lu mutate mara kwa mara.
However itafanikiwa kama gonjwa sio lenye virus. Virus wako smart sana..always wako kwenye constanr mutation.
Unachozungumzia ni herd immunity.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda tusiwe kama huko kwasababu tumeficha taarifa. Kingine huenda moto haukufika kwenye nyasi kavu kwa wagonjwa na wazee kama ilivyotokea huko kwingine. Hii ni kwasababu gonjwa lipo mjini na wazee wapo vijijini. Tuombe Mungu lisifike huko.
Gonjwa lipo nasi tumepoteza umakini hivyo kipimo ni mpaka December ndipo nitaamini nimepona. Sie wenye presha nimeshuhudia hata ukijivukiza au kula hizo dawa kufa ni asilimia kubwa.
Tushindwa kulindwa. Tukipona ni bahati yetu tu ila tunatakiwa kufa uchumi ukuwe.
 
What is herd immunity?
When most of a population is immune to an infectious disease, this provides indirect protection—or herd immunity (also called herd protection)—to those who are not immune to the disease.

For example, if 80% of a population is immune to a virus, four out of every five people who encounter someone with the disease won’t get sick (and won’t spread the disease any further). In this way, the spread of infectious diseases is kept under control. Depending how contagious an infection is, usually 70% to 90% of a population needs immunity to achieve herd immunity.
 
Zitto unazingua MH! Rais akiongea wewe kaa kimya, sio unasubiri aongee ndio ujibu, ni nidhamu ya wapi hii? Ungesubiri siku yako ndio uje na hoja zako. Hotuba yako haiwezi kuifunika ya mkuu wa nchi. Tunamwamini yeye sio wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watu 3% wamekufa wapi? Watu wote wa mkoa wa Njombe wafe afu hali iwe kama ilivyo, Subutuuu.

Kwa hili, nampongeza Raisi, he was a visionary.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni kweli usemavyo kwanini basi maabara kuu imefungwa?? Kwanini hivi sasa madaktari wanawakataa wagonjwa walio serious hata kwa magonjwa yasiyoambukizwa kwa hofu ya corona??

Kuna mama jirani yangu akiwa dukani kwake aliletewa taarifa kuwa mke mwenzake yaani mke wa shemeji yake amefariki. Kwa ule mshtuko yule mama alianguka chini na kupoteza fahamu. Alikimbizwa kwenye hosp ya wilaya wakamwambia wamuwahishe hosp ya mkoa Mt. Meru walipofika wakawambia wampeleke Kaloleni. Walipofika Kaloleni waliwaambia warudi Mt. Meru wakiwa njiani yule mama aliaga dunia.

Hospitali zote hizo mgonjwa hakutakiwa kushushwa kwenye gari bali kote madaktari walimu atend kwenye gari kisha kutoa maelekezo. So sad Kaka wawili kupoteza wake zao kwa muda mfupi tena kifo cha pili kikiwa ni cha kizembe kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Enzi za Nuhu na Safina watu wabishi dizaini yako walikuwepo...

Yaani walikuwa hawaamini kabisa walipokuwa wanaambiwa kuwa Mungu kasema anakwenda kuingamiza dunia nzima kwa maji ya mvua kubwa ambayo haijawahi kutokea huku akiwaleza cha kufanya kwa kila anayetaka kuokoka....

Kwa ubishi wao na kutokutii na kutokujali, matokeo yake ni kuwa wote waliangamia na mtu mmoja tu yeye na familia yake pekee waliotii ndiyo walio okoka wengine wote wakaangamia kwa maji.....

Ishu ya Korona si ya kawaida. Ni "wake up call" toka kwa Mungu mwenyewe ili kurekebisha akili na tabia za watu na kuwafanya waelewe kuwa pasipo yeye Mungu hawawezi kujiponya....

Korona whether we like it or not inakwenda kubadili kabisa mfumo wa maisha ya watu duniani....

Maisha hayawezi tena kuwa sawa na tulivyozoea miaka na siku za nyuma....

Rais John Pombe Magufuli yuko sahihi ktk jambo moja tu na hilo hata mimi nampongeza sana....

Ni la kutambua kuwa yupo Mungu Yehova mwenye nguvu na uwezo wa yote na kwamba huyo ndiye awezaye kumwokoa kila mtu iwapo atamwomba na kumpa maisha yake yote...

Lakini wokovu hauji kwa kuendelea kuwa na aina na staili ya maisha yaleyale tuliyozoea ya dhambi, maisha ya kumchukiza Mungu na kutomtii hata kama tutaomba huku tukipigiza vichwa kwenye mawe na kujichana chana kwa nyembe na visu....

Wanaopona na watakaopona na kifo cha Corona ni wale pekee wanaojinyenyekesha kwa Mungu Baba Yehova na kumheshimu na kumtii yeye pekee yake...

Wengine wote watapiga kelele na kujifanya kwa unafiki tu kuwa wanampenda Mungu Yehova huku mioyo yao ikiwa mbali naye, lakini kamwe, Corona haitawaogopa watu wa namna hii...

Haiwaogopi na itakuwa inawapitia na kuwaua mmoja mmoja kama moto utafunao nyasi kavu uwandani mpaka pale watakapogeuza nyuso zao kumuelekea/tazama Yehova....

Wimbo wa "....maombi, maombi, maombi...." hautamsaidia mtu awaye yeyote kama moyo wake mtu huyo umejaa "chachu" ya dhambi bila kujali mtu huyo ni nani....

Ni bora sana watu hao wakatumia njia za kibinadamu kujiokoa wenyewe na Corona ili ingalau waweze ku - extend siku zao kidogo za kuishi hapa duniani....

Hii ndiyo "logic" iliyo ndani ya kile kisemwacho na kinachoshauriwa na kina Zitto, Mbowe na wengine kitu ambacho siyo kibaya na ni jukumu la serikali yeyote kuwalinda wananchi wake....

Tukirudi kumjadili Rais Magufuli, ni kuwa;

Amewahimiza watu sana waelekeze sauti na nyuso zao kwa Mungu Yehova kwa maana ndiye pekee awezaye kutuokoa. Hilo ni jambo jema sana kwa Rais kuwa na ufahamu huu....

Haieleweki if it's just coincidence ama Mungu kaamua mwenyewe kumtumia bila hata yeye kujua kuwa anatumiwa kama "kipaza sauti cha Mungu" ili yeye Mungu aokoe watu wake.....

Hii inathibitishwa na kitu kimoja, kuwa, Rais Magufuli ana tatizo lake binafsi kama binadamu....

Yeye personally anaabudu miungu yake mingine tusioijua sisi. Utamgundua kwa kauli na matendo yake....

Anahimiza watu waombe Mungu wa kweli - Yehova, lakini yeye mwenyewe akiwa anachanganya changanya ya MUNGU (kwa kusema kwa mdomo), lakini wakati huohuo MOYO WAKE unaamini na kutenda vinginevyo...!!

Mfano huyu Rais anahusudu na kupenda ushirikina wa kujifukizia huku akiwa amejichimbia Chato...

Hivi tunadhani alikuwa anafanya nini kwa zaidi ya siku 50 huko Chato kijijini kwao ili hali hayo ni makazi ya wazazi wake na yeye mwenyewe binafsi..!!??....

Akili kumkichwa....

Kwa hili Mungu Yehova wala hana shida naye, bali adhabu yake kama binadamu wengine ipo juu yake mwenyewe....

Hataikwepa "unless" atambue kosa lake mapema, anyenyekee, atubu na kumwabudu Mungu wa PEKEE, wa KWELI katika Yesu Kristo....!!

Hapo naye ATAPONA....!
 
Herd immunity kwani tupo Ngorongoro au Serengeti huyo Zito ni Choo na yeye anahutubia raia kama Rais wa nchi eti ndugu wananchi...... kichekesho
 
Inatia faraja sana kuona ndani ya Tanzania bado tuna baadhi ya viongozi wachache ambao wanaweza kuja na makala ya uchambuzi iliyosheheni hoja zenye fikra pevu huku zikisindikizwa na mifano ya ukweli iliyowasilishwa kwa upeo wa hali ya juu. Zitto unaitendea haki elimu yako, sio kama wale maprofesa uchwara ambao siku zote huja na hoja mfu zionyeshazo ugoigoi na uzumbukuku wao kifikra.

Nchi yetu inapitia kipindi kigumu sana kutokana na mawazo mengi ya kipumbavu na kijinga kupewa nafasi kubwa kwa lazima ili yatawale masikioni mwa Watanzania bila hata ya ridhaa yao. Hoja zako zinaonyesha jinsi ulivyokuwa na uelewa na upeo mkubwa wa mambo ya kijamii, kisayansi, kiuchumi na kiuongozi.

Umeeleweka vizuri sana kwa wote wenye upeo mkubwa wa kufikiri huku wakiongozwa na hulka za kudadisi, kuhoji, kukemea na hata kupinga mambo mbalimbali yasiyofaa nchini Tanzania.
 
I think the government has decided to throw us under the bus. They fail to contain it in the early stages so now the pandemic is all over the country!. It can’t be controlled any more.
So now it’s your choice to protect yourself, your family, the people you love and society in general.
It’s your call.
Usitegemee tena Serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…