Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mahakama ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam imewapandisha kizimbani washitakiwa saba, wakidaiwa kuiba magari mawili wakati yakipelekwa Bandari kavu ya Vingunguti.
Washitakiwa hao ni Isack Natus, Samson Mwamoto, Daniel Noah, Adam Sufian, Michael Marwa, Fadhil Munisi na Tusho Kalambire.
Washitakiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Victoria Mwaikambo na walikana shitaka la wizi.
Wakili wa Serikali, Nicas Kihemba alidai washitakiwa hao waliiba magari mawili, likiwemo aina ya Nissan Caravan na lingine Toyota Regiusace yaliyokuwa yametolewa bandarini kwa ajili ya kupelekwa bandari kavu ya Vingunguti. Magari hayo yanadaiwa ni mali ya Sudais Logistic Company Limited.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, badala ya magari hayo kufikishwa katika bandari kavu yalipokuwa yakipelekwa, mwelekeo wake ulibadilishwa na kupelekwa Kigamboni.
Inadaiwa Agosti 12, mwaka huu katika opereshenI ya kudhibiti wizi wa magari na vifaa vinavyotolewa bandarini kwenda bandari kavu mbalimbali, iliwafikisha maofisa katika nyumba ya Michael ambako magari hayo mawili yalikutwa. Washitakiwa wote walikana mashitaka yao.