Kosa Dogo Ambalo Hupelekea Wakurugenzi Wa NGOs Kutumia Mamilioni Ya Fedha…

Kosa Dogo Ambalo Hupelekea Wakurugenzi Wa NGOs Kutumia Mamilioni Ya Fedha…

akwilau

Member
Joined
Jun 18, 2020
Posts
12
Reaction score
16
Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) ambayo yamesajiliwa kwa mjibu wa sheria ya mwaka 2002 ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali, mashirika hayo yanawajibika kufanya marejesho ya taarifa za shughuli zake pamoja na taarifa zilizo kaguliwa na kuidhinishwa na mkaguzi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).

Pamoja na matakwa ya sheria hiyo, bado kuna wakugurugezi wa NGOs ambao hushindwa kuwasilisha marejesho ya taarifa hizo kwa wakati na kupelekea mashirika yao kutozwa mamilioni ya faini na riba kwa kushindwa kutumiza matakwa ya sheria hiyo.

Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakalo shindwa kuwasirisha marejesho ya taarifa za shughuli zake pamoja na taarifa zilizo kaguliwa na kuidhinishwa na mkaguzi kwa kipindi cha miaka miwili litafutiwa usajiri wa leseni yake na msajiri wa NGOs.

Kifungu cha sheria namba 29 (1) (a) na (b) ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kinasema; kila NGO kwa kila mwaka husika wa fedha litawajibika;
  • Kuandaa taarifa za shughuli zake za mwaka wa fedha husika na kuhakikisha zinapatikana kwa wadau, baraza la NGOs pamoja na kwa msajiri wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

  • Kuandaa taarifa ambazo zimekaghuliwa na kuidhinishwa na mkaguzi aliyesajiliwa, taarifa hizo zitawasirishwa kwa msajiri wa NGOs pamoja na kwa baraza la NGOs Tanzania.
Vile vile kupitia Baraza la NGOs Tanzania lililoanzishwa na sheria ya mwaka 2002 ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali kupitia kifungu cha sheria namba 25 (1) linasisitiza pia uwasirishwaji wa taarifa na mashirika hayo yasiyo ya Kiserikali.

Aya namba 7.1 (l) na (m) Baraza la NGOs Tanzania, inasisitiza kuwa Shirika lolote lisilo la Kiserikali linawajibika kuandaa taarifa za shughuli zilizo tekelezwa mwaka wa fedha pamoja na taarifa zilizo kaghuliwa na kuidhinishwa na mkaguzi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi. Taarifa hizo ziwasirishwe kwa msajiri wa NGOs pamoja na kwenye Baraza la NGOs Tanzania.

Tarehe ya mwisho wa kuwasirishwa taarifa hizo huwa inatangazwa na msajiri wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Hata hivyo mara nyingi tarehe ya mwisho ya uwasirishwaji wa taarifa hizo huwa mwezi wanne wa mwaka unaofuata baada ya kufunga mwaka wa fedha.

Hivyo Mashirika yote yasiyo ya Kiserikali yanapaswa kuwasirisha taariza hizo kabla ya tarehe inayotangazwa na msajiri wa NGOs ili kuepuka kutozwa faini kwa kuchelewesha taarifa hizo.

Marejesho ya taarifa hizo zinawasirishwa pitia nis.jamii.go.tz

BY THE WAY…unaweza kutuchagua kuwa wakaguzi (auditors) wako wa hesabu za mwaka wa fedha 2024. Tuma ujumbe (appointment) wa kuwa na utayari wa kufanya kazi na sisi kwenda namba ya simu 0752 187 434 au pitia barua pepe info@halaconsultants.co.tz tuma ujumbe huo ndani ya saa 24 ili taasisi yako ijumuishwe kwenye mpango kazi ya mwaka 2025 mapema mapema iwezekanavyo.

HALA Consultants, Certified Public Accountant
info@halaconsultants.co.tz
0752 187 434
 
Back
Top Bottom