Kosa gani ulimfanyia mama yako hadi likasababisha akuchape au kukuadhibu?

Kuna siku home ilipotea fedha kiasi kikubwa naweza sema, kwa kuwa nilikuwa mdogo na mjanja-mjanja pale home, familia hasa mother akani-point kwamba nahusika moja kwa moja na upotevu ule wa fedha, sio siri nilichezea sana fimbo siku ile na sitasahau kamwe...baadaye ikajagundulika mzee wangu alizichukua na kuzihifadhi sehemu baada ya kuona zinazagaa baada ya yeye kuzitoa, kisha kwenda kwenye matembezi yake! Hali hiyo ilipelekea sisi kutokula jioni kwa kuwa mzee alichelewa sana kurudi! Asubuhi yake ilibidi mama alazimishe urafiki na mimi japo nilikuwa na hasira ilinilazimu nikubali kishingo upande hah hah kweli Old is Gold! Hiyo ilikuwa around 1992 pale Arusha sinoni daraja mbili!
 
Kwa kweli Mimi sikumbuki kama niliwahi chapwa na Mama kwa sababu ni mpole mno.
Kweli nilikuwa nafanya makosa lakini alikuwa akinisamehe.

Ila kina mama ni watu wa kipekee sana.
Kuna siku moja mama alinituma nikawashe moto kwenye jiko la kuni yeye alikuwa akimenya viazi.
Sasa nilipofika jikoni nikakuta moto kidogo, nikachukua kuni nikaweka jikoni nikaanza kupuliza ili moto uwake sasa kila nilipopuliza moto haukuwaka badala yake ni moshi tu ndo ulitawala.

Moshi uliniwasha machoni hadi michozi ikanitoka, kwa kweli hasira zikanishika nikachukua zile kuni nikazivurumisha kwenye majivu pale jikoni, nikaenda nje nikachukua michanga nikaja kufukia pale jikoni kabisa hadi moto wote ukazimika.

Nikaenda kukaa nyuma ya nyumba huku nikilia macho yamenivimba hatari.

Mama akaanza kuita sikuitika, alipoenda jikoni alichokiona huko ilibidi aniite tena kwa hasira na hapo nikaitika ila sauti ilionyesha nilikuwa nalia.

Basi akaja kule nyuma, kakasirika kweli kweli lakini aliponikuta na hali ile hasira zikamuisha ghafla na kuanza kunibembeleza ninyamaze. Nilipotulia nikamueleza kilichotokea.

Doh!
Sikuwa kumuona mama akicheka kama siku hiyo.
Hadi leo hua akikumbuka hilo ananicheka sana.

Hili ni tukioa ambalo kamwe sitalisahau.
Yani imefanana na stry yangu.mm yangu ni hivi.
Dada wa kazi alikua ameteleka mafuta ili akaange samaki,akasema niangalizie mm naenda ndan mara moja,nkamwambia ok,mda ukawa unaenda huku mafuta yanazid kupata moto.
Nikajitia kiherehere nkachukua samaki nakuanza kuwatia ndani ya mafuta,weee moto ai uwake lile karai lote vile vishikilio vya mbao vilivunjika yaani.

Nkaanza kupiga kelele dada kuja akawa anahangaika kutupia mchanga ili moto uzimike,nkasema leo ntapigwa mm,leo ntauliwa mm karai lishaungua,hofu ilinizid.
Mpk nkapata homa ya ghafla kwa kuogopa mama akirud leo ni kichapo tu.nkawa nmelala kitandan homa full[emoji16][emoji23].
jioni mama anarud anasema yuko wapi huyu,dada akasema anaumwa yupo ndani ,mama akaja mbio ndani,waswas umemjaa anauliza maswal mara mbil mbil kua ninaumwa na nn mara anishike shingo apime joto la mwili basi ilimradi tu[emoji23]hapo macho yamenivimba kwa kulia na homa full,kichwa kinauma hatar.

Dada wa kaz akaanza kumuhadithia A to Z mama akaanza kucheka mbavu hana [emoji23][emoji23]kwaio unaogopa mm kukupiga kisa kuunguza karai tu,[emoji23]haya nyanyuka ule panadol,si ulikua unajifunza kupika ntaanzaje kukupiga,yani nlipata nafuu ghalfla na nlipona hapohapo[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dooh! Eti nilipona hapohapo
 
Kiukweli, Najivunia kuwa na mama alikulia kwenye maadili mema na kunikuza kimaadili.
Najua nilimuudhi mama Mara nyingi lakini hakuwahi kunichapa, labda nilipokuwa sijajitambua!!!
Hata Dada zangu wamekuwa wakimuudhi but hajui kupiga wala kutukana.
Akikuta Dada zangu wanatukanana yeye ndiye anayelia na kusema Mnamkosea Bwana,Mungu wenu.
Baadae anaingia faragha kufanya Maombi.
Basi, mkishaona hivo; mnajua mmemkosea mama.
Have a long last my Mama.
 
Mimi nilikuwa sipendi kuoga kabisa, sasa ikifika muda natakiwa kuoga ilikuwa tunakimbizana na Dada mtaa mzima so mama alikuwa ananilisha bakora za kutosha
 
Alinituma chumvi dukani siunajua michezo niliporudi kifika mlangoni nikamtupia nikageuka nakimbia kuwai kucheza mpira akaniita wakati naondoka nikazani napewa zawadi nilipewa kifinyo hatariiiii..... Hata mpira sikwenda kucheza
Hahah,kweli ase iyo weng san tmechapw kw style hyo.mambo ya mpira uko na michez,kuach njian ukiitw hasa ukiwa unaplay karbu na hme ni kero ukskia unaitw.
 
Yani imefanana na stry yangu.mm yangu ni hivi.
Dada wa kazi alikua ameteleka mafuta ili akaange samaki,akasema niangalizie mm naenda ndan mara moja,nkamwambia ok,mda ukawa unaenda huku mafuta yanazid kupata moto.
Nikajitia kiherehere nkachukua samaki nakuanza kuwatia ndani ya mafuta,weee moto ai uwake lile karai lote vile vishikilio vya mbao vilivunjika yaani.

Nkaanza kupiga kelele dada kuja akawa anahangaika kutupia mchanga ili moto uzimike,nkasema leo ntapigwa mm,leo ntauliwa mm karai lishaungua,hofu ilinizid.
Mpk nkapata homa ya ghafla kwa kuogopa mama akirud leo ni kichapo tu.nkawa nmelala kitandan homa full[emoji16][emoji23].
jioni mama anarud anasema yuko wapi huyu,dada akasema anaumwa yupo ndani ,mama akaja mbio ndani,waswas umemjaa anauliza maswal mara mbil mbil kua ninaumwa na nn mara anishike shingo apime joto la mwili basi ilimradi tu[emoji23]hapo macho yamenivimba kwa kulia na homa full,kichwa kinauma hatar
Hah ulijiadhibu.
 
Mimi nilikuwa sipendi kuoga kabisa, sasa ikifika muda natakiwa kuoga ilikuwa tunakimbizana na Dada mtaa mzima so mama alikuwa ananilisha bakora za kutosha
Hahah safi san,mambo ya kuoga ayo ase afu ukute ni ya barid maji,apo lazma tkimbizane t na mama.
 
Back
Top Bottom