Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Ningeweza kutumia maneno mengi kuelezea kosa hili ambalo hata hivi sasa bado tunalifanya lakini hatuna budi kujisahihisha kama mabadiliko tunayoyataka yataweza kupata nafasi yoyote. Kosa hilo ni kosa ambalo hatujaona ubaya wake na ni nafasi hii kutafakari kama kuendelea nalo tunaendelea kujihukumu sisi wenyewe na uzao wetu kwenye utegemezi na uombaomba wa kudumu.
Kosa tulilolifanya ni Kuwaachia wanasiasa wetu kuendelea kutengeneza ajenda za kisiasa kwa taifa letu na kutuletea sisi wananchi; tumewaacha waandike ilani zao na kutuletea sisi; tumewaacha wao waamue nini tunataka halafu wanatuomba kura kwa msingi huo..
Nasema sasa yatosha; 2010 "sisi wananchi wa Tanzania mahali popote tulipo na katika hali zetu zote tulizonazo, tutaamua tunataka nini, lini, na kwa namna gani; tutauza ajenda hiyo kwa wanasiasa wetu na ni kwa msingi huo ndio tutawachagua".
Sijali tena CCM itaahidi nini; sijali CUF wataahidi nini; sijali Chadema wataahidi nini au watakuja na ilani gani. Wakati huu wao ndio watagombania kile tunachokitaka ili watuletee kwa namna tunayotaka.
Kwa maneno mengine, hatima ya kisiasa na kiuongozi ya nchi yetu tunataka kurudisha mikononi mwa wananchi wenyewe.