Uchaguzi 2020 Kosa kubwa walilofanya CCM kwenye kampeni zao ni kupoteza muda kusifia yaliyopita badala ya kueleza watafanya nini

Daaaaaaah basi tuko hatarini, ko mitano tena ya kuuana, kutekana, kugeuza bodi ya mikopo ya elimu ya juu kua Bank ya biashara kwa wanafunzi, kutowaongezea mishahara wafanyabiashara, kufanya miradi kwa kuangalia watu wenye pesa badala ya mamilioni ya watanzania ambao wanakosa hata maji.

Kuogeza gharama za maji kwa wanyonge ili wenye pesa wanunuliwe Ndege za kupanda, kutumia pesa za wanyonge kujengeana nyumba wastaafu, ya watu kukosa ajira, ya kuzorota kwa shughuli za biashara, za kuwabambikizia kodi wafanyabiashara ili kuafilisi, Kweli tutalimia meno.
 
Uko sahihi sana, lakini kuongezea kitendo cha kampeni kutawaliwa na sanaa kwa asilimia 80% badala ya Sera ni kosa kubwa kisiasa. Wenye busara wanakuona kama una mizaha na maisha yao.
 
Duuuu kweli Wazee walisema "Ukiona chongo unaita kengeza"; maana CCM ndiyo Ilani yao imesheheni tuliyofanya miaka mitano iliyopita na nini tumepanga kufanya miaka mitano ijayo. Wagombea wote wa CCM wamekuwa wakieleza haya bayana.

Ni Chadema tuu ambao wamekuwa wakiogopa kusema waliyofanya miaka mitano ikiyopita maana ni mabaya saaana k.m. kupinga bajeti zote ambazo zimewanufaisha Watanzania; kupinga SGR, Umeme wa Stiegler's Gorge, Ndege za ATCL, kutaka nchi iende lockdown kwa Corona,..... n.k.

Vilevile wameogopa kueleza kuwa miaka mitano ijayo wamepanga kuweka dhamana madini yetu kwa mabeberu, kuanzisha utawala wa majimbo......... Mjomba HATUDANGANYIKI. Tunawaelewa saaaana Lissu na vibaraka wote. Subiri tarehe 28 Oktoba.
 
hata mkeo ndani anapenda kuskia ahadi mpya kwamba nitakununulia nguo nitakuletea viatu nitakupeleka movies.

Lakini ukimwambia nilikununulia nguo nilikuletea viatu nilikupeleka movies anakuchoka sababu yale ameshayaona hayana jipya tena kwake.
Haswaa.. pimbi wa Lumumba hawajui haya. Wanaishi kwny history tu
 
Mitano tena ya Bombardier
Mitano tena ya Meli na vivuko
Mitano tena ya barabara
Mitano tena Madaraja
Mitano tena ya Masoko ya kisasa
Mitano tena ya Shule
Mitano tena ya hospitali na vituo vya afya na zahanati..
Mitano tena ya kutopandisha nadaraja watumishi
Mitano tena ya kuwaibia wa kulima korosho
Mitano tena ya kitambulisho vya ujasiriamali
Mitano tena ya kuwanyanyasa wafanyabiashara
 
Yani nyie wafuasi wa aunti Lee mmeshikiwa akili sana.

Ccm inaenda kushinda kwa kishindo mana inashindana na vyama dhaifu.
 
Huwezi kushindana na wakati ndugu yangu.kila chenye mwanzo kina mwisho wake pia.
Mikutano yake watu wanakusanyika kuona na kusikiliza wasanii.. Akina diamond wakishuka jukwaani, jiwe akianza porojo zile zile za kila siku, wasikilizaji wanasepa
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua ni dhaifu Kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Haya ni matokeo tu ...Wapambe wa JPM walishindwa kuelewa kuwa Uongozi Ni kushawishi! Inategemea unashawije! Wao waliamua (JPM)!?kutumia nguvu na hila!

Mtindo huu unatanya /ilikuwa unatanya kazi kwenye Jamii zilizotopea ujinga,kukosa taarifa...
Tunduma waliwaambia kaeni na maji yenu tumeshazoea kuishi bila maji kwa miaka 60 leo mnatutishia maji,

ndio maana nikasema kampeni ni ushawishi sio nguvu, kwenye dini unaweza kumtisha muumini kuwa usipomwamini Yesu utakuja kuchomwa moto akaogopa sio kwenye siasa.
 
Umesema kweli lakini kuna mijitu inayolipwa kuongea pumba itakuja kukupinga hapa na kukubishia.

ukweli kampeni ni kama kutongoza vile hata mkeo ndani anapenda kuskia ahadi mpya kwamba nitakununulia nguo nitakuletea viatu nitakupeleka movies...
Mume anaeongelea aliyoyafanya ni dalili za masimango.
 
CCM walikua wanasafisha njia kwa uongo na ulahai wenu mlowalisha wananchi katika kampeni.

Kwamba ndege,ujenzi wa nchi,maendelo ya vitu hayaitajiki nchi hii.

Hapo ndo watu wakawaona nyinyi kweli Ni mwezi mchanga
Na wewe unaendeleza ulaghai ule ule, hakuna mtu aliyesema ndege hazihitajiki bali priorities, huwezi kununua ndege 10 huku hospitali hakuna dawa kama ni lazima kununua ndege kwanini usinunue mbili au 3?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…