Kuna swali limulizwa. Wakati jiwe anaingia nauli za fast jet kutoka Dar Mwanza ilikuwa 70,000 tu! sasa ni 400,000!
Sukari ilikuwa 1800tu! sasa ni 3000-3500
MAUZO YA MAZAO
Pamba ilikuwa inauzwa 2500@kg sasa ni 1200 na wanunuzi wote ni makada wa ccm!!
Kahawa ilikuwa inauzwa sh 2500-3000@kg, sasa inauzwa 1200
Kwa kifupi. Magufuli ameua uchumi wa nchi yetu!!! lazima aende!!!
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUPIGA KURA TAREHE 28 OKTOBA.
------------------------------------
1. Miaka mitano iliyopita hatukua na Zahanati kila Kata, sasa kila Kata nchi nzima kumejengwa Zahanati.
2. Miaka mitano iliyopita watumishi walikua wanapata mishahara yao tarehe tatu hadi tano ya mwezi unaofuata. Sasa kila tarehe 23 siku saba kabla ya mwezi kuisha mshahara umelipwa.
3. Miaka mitano iliyopita Machinga na Mama Ntilie walikua wanafanya biashara kwa tabu na manyanyaso makubwa, sasa wanaheshimika na biashara zao zimehalilishwa kwa tsh. 20,000/= kwa mwaka.
4. Miaka mitano iliyopita Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu walikuwa wakipata pesa za boom wiki tatu hadi nne baada ya kusain. Sasa ni express siku tatu hadi tano kwisha kusaini pesa imejaa ktk akaunt bila usumbufu wowote.
5. Miaka mitano iliyopita tulipoteza mabilioni ya pesa kwa ajili ya foleni katika jiji la Daslamu, kwa sasa alhamdullah foleni zimepungua na zinakwenda kuisha kabisa baada ya ujenzi wa njia NANE na Flyovers, Tazara na Ubungo.
6. Miaka mitano iliyopita Ziwa Victoria kulikua na Meli moja tu ambayo pia ilikua imechakaa, hivi tunazungumza Meli Mpya ya NEW VICTORIA inachana mawimbi Mwanza to Bukoba na nyingine nyingi zimekamilika, Ukerewe, Ukara Ruvuma, Kilwa nk.
7. Miaka mitano iliyopita tulikua hatuna Ndege ya Serikali hata moja, yaani hata ya dawa lkn kwa sasa zipo zimetapakaa ktk anga la Tanzania Ndege NANE kwa hewa.
8. Miaka mitano iliyopita vijijini waliusikia UMEME kwenye redio lakn sasa hadi bibi yangu Kisiwani Kome anawashia UKUTANI. Tumeongeza uzalishaji kutoka megawati 1308 hadi megawati 1602.32. Bado ule wa Mto Rufiji, haya ni maajabu yanayostahili heshima kubwa.
9. Miaka mitano iliyopita maji ya bomba ilikua ni ndoto katika baadhi ya mikoa nchini, sasa mtandao wa maji umeongezwa kwa nchini nzima na tunaendelea kusambaza ili maji safi na salama yawafikie Wananchi ktk maeneo yote.
10. Miaka mitano iliyopita RUSHWA ilikua ni donda ndugu, bila kidogo hupati huduma hata kama ni haki yako. Miaka mitano baadae taratibu tunaendelea kunyooka, rushwa inapungua na haki inapatikana kwa halali.
11. Miaka mitano iliyopita kulikua na utitiri wa tozo na KODI katika biashara ya mazao. Sasa ni free of charge gunia la kilo 100 safirisha uwezavyo Tunduma hadi Ukerewe.
12. Miaka mitano iliyopita Watumishi wa Umma wote walikua KAMBALE, hakuba mkuvwa wala mdogo wote walikua na ndevu. Kama humfahamu utamfahamu, walikua hawaambiliki wala kugusika, sasa kila mtumishi wa Umma ni mfanyakazi wa Mwananchi. Sasa nidhamu imerudi na heshima ipo kazini.
13. Miaka mitano iliyopita wachimbaji wagodo wa Madini hawakutambulika katika ardhi ya kwao, sasa wanatambulika kwa leseni, wamepatiwa vitalu vya kuchimba madini ili wajipatie kipato. Katika hali hii kuna mtu anataka kuweka rehani MADINI, hakikisha unapiga KURA kwa CCM kutoa ujumbe kuwa madini yetu ni mali yetu.
14. Miaka mitano iliyopita Reli ya Kanda ya Kati haikua na mbadala wake, siku tatu Dar hadi Mwanza. Sasa karibuni kutakua na mtambo wa kusaga na kukoboa unaitwa SGR, yaani saa saba tu umetoka Mwanza unakula lunch Silver Paradise Hotel pale TIPTOP Daslam.
15. Miaka mitano iliyopita Salender haikufikiriwa kuwa na daraja la baharini, busisi ilikua ndoto kuweka daraja ziwani, sasa mda si mrefu tutakua tunachagua wenyewe kupita katikati ya maji au barabarani. This is wonders brothers and Sisters.
16. Ni hivi; miaka mitano iliyopita ilikua ya kwetu. Tulifanya tukaisha hapo, sasa tumesogea zaidi ya pale. Tunaomba miaka mingine mitano tupige hatua kubwa maradufu!
Orodha ni ndefu, Oktoba 28, piga KURA kwa Diwani wa CCM, Mbunge wa CCM na Rais wa CCM kazi iendelee!!!
Utakosa PEPO bure, kuwa muungwana tumefanya mambo mengi mazuri kwa miaka mitano tunastahili KURA yako.
#MitanoTena!