Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Kwasababu bado sina chama cha siasa, nataka kuwashauri viongozi wakuu wa CCM. 'Msijitenge na hoja ya katiba na kuwaachia upinzani pekee, mnafanya kosa kubwa'.
Nimeangalia trend mpaka sasa huko mitandaoni, nimesikitika kuona kwamba kila mwana CCM ambaye ataongea kuhusu katiba mpya, basi ataongelea kwa kusema kwamba nchi haihitaji katiba mpya kwa sasa. Hili ni kosa kubwa sana, nadhani ambacho CCM wangepaswa kufanya kwa sasa ni kufanya utafiti wa kisayansi wa kujiridhisha ni kwa asilimia ngapi wananchi milioni 60 wana kiu ya katiba mpya.
Baada ya kujiridhisha ndipo haswa wanatakiwa kuja na hoja ama za kupinga katiba mpya ama na wao wajiingize moja kwa moja kwenye ajenda ya katiba mpya.
Kufuatia miaka mitano ya 'stress' ni wazi kwamba upepo uliopo sasahivi ni upepo wa mabadiliko, na wala CCM wasidhani kwamba upepo huu wakudai mabadiliko ni hoja ya CHADEMA, la hasha, kuna wana CCM wengi tu sasahivi nao wanahisi kwamba kuna mabadiliko yanahitajika kufanyika.
Sasa ukiwa kwenye hali hiyo ya uchu wa watu kutaka kubadilika, kama chama cha siasa na wewe itabidi uone namna gani uta flow na mawimbi, na hii itakuwa na matokeo makubwa sana kwenye umaarufu wa chama cha mapinduzi chenyewe, hatari kubwa na ya mapema ya CCM ni kuanza kuonesha eti wanapinga katiba mpya.
Ningeshauri uongozi mpya wa CCM waone namna ya wao kuikumbatia hii ajenda ya kuwa na katiba mpya, wasiwaachie upinzani peke yao, kama kweli wanamipango ya CCM kuendelea kuonekana kwenye uso wa Tanzania miaka 20 inayokuja. Hakuna namna CCM itataka kupinga katiba mpya na kuendelea kutawala kwa miaka 20 inayokuja, sidhani kama taifa hili la vijana wenye uchu wa mabadiliko wataacha hichi kitu kitokee.
Sidhani kama ndani ya miaka 10 hadi 20 ijayo ambapo nchi itakuwa na watu kati ya milioni 70 au 80, asilimia zaidi ya 65% wakiwa vijana ambao wengi watakuwa wamesoma na hawana ajira, hapo hapo kiwango cha umasikini bado ni kikubwa, halafu hapo hapo nchi bado inaishi bila katiba mpya, hichi kitu kitakuwa kigumu sana kuwezekana, na kama kuna watu huwa wanafanya analysis ya kutabiri matukio ya miongo miwili ijayo, ni wazi kwamba kwa dunia ya sasa inavokwenda, CCM hawatakiwi kabisa kufikiria kwamba wataendelea ku exist salama bila nchi kuwa na sheria na katiba ya kueleweka.
Na itakuwa ngumu sana ku guarantee Tanzania isiyomwaga damu kama hakuta kuwa na katiba na sheria za kueleweka ndani ya miaka 10 mpaka 20 inayokuja maana ni kipindi ambacho kiwango cha subira na uvumilivi kwa watanzania walio wengi kitakuwa kimefika ukomo.
So mi nachukulia huu utawala wa mama kuwa ni kipindi cha muhimu na cha mpito kwa mustakabali wa utulivu wa nchi ya Tanzania kwa miaka 10 na 20 inayokuja. Hili suala lisichukuliwe ki uwepesi, watanzania wengi hawapo tayari kwa 'another Magufuli' ndo mana hili vugu vugu la katiba mpya ni tofauti na vugu vugu la katiba kwenye enzi ya Kikwete. Completely different atmosphere.
So kwa mtizamo wangu, katiba mpya ni damu na moyo wa CCM kama kweli itataka kusalia madarakani.