Kosa la karne kwa CCM ni kujitenga na hoja ya Katiba na kuwaacha upinzani watambe nayo

Moja ya mapungufu makubwa ya Watanzania ni usahaulifu. Huyu anayesema "kiwango cha subira na uvumilivu sidhani kama kitakuwa kwa Watanzania wengi" ameshasahau kuwa porojo za "tunataka katiba mpya" hazijaanza Machi 19 baada ya Mama Samia kuapishwa. Zilianza mwaka 1992 pengine wakati huo mtoa mada alikuwa hajazaliwa.

Na kati ya wakati huo na sasa, yamejiri mambo mengi ambayo kwa wenzetu wanaojielewa, basi huenda muda huu CCM ingekuwa historia. Kwa kukumbusha tu, utawala wa Mkapa ulitawaliwa na ubabe uliopelekea vifo vya Wazanzibari kadhaa Januari 2001. Lakini Mkapa alimaliza muda wake salama. Akaja Jk, ambaye aliigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi, ufisadi ukawa kama umehalalishwa na Katiba. Nae akatawala hadi muda wake ulipoisha 2015.

Na ilipotokea fursa bora kabisa kwa Upinzani kuing'oa CCM mwaka 2015 kwa kuzingatia rekodi ya kutisha ya ufisadi wa Jk na CCM yake, Upinzani ukaamua kumpokea na kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea wake wa urais, licha ya upinzani huohuo kumtangaza tangu 2006 kuwa ni papa la ufisadi.

Na 2015 hadi Machi 2021, Tanzania ilipitishwa kwenye tanuru ka moto mkali chini ya utawala wa Magufuli. Na laiti korona isingemwondoa, angeendelea kutawala hadi aamue kuachia madaraka.

Sasa hizi "hasira mpya" na "uvumilivu una mwisho" vinatoka wapi? Usahaulifu au kujimwambafai ilhali uwezo pekee uliopo ni kwenye kufuatilia ubuyu?

Yes Katiba mpya ni muhimu lakini you guys need to be realistic. Itapatikana kwa matakwa ya Mama Samia na si kwa porojo za mtandaoni. I'm not saying kwamba Katiba inahitaji ridhaa ya Rais bali nakumbusha tu hali halisi ilivyo.
 
S
Sidhani kama CCM haitaki katiba mpya au katiba bora suala hapa ni muda mwafaka wa kutekeleza hilo. Ni wazi kuitaka katiba mpya na lini wazo hilo linahitaji kutekelezwa kwa mmaana ya TIMING ni jambo lingine. Utekelezaji wa hatua hii unahitaji umakini ili kuepuka madhara, maandalizi na kutathmini matokeo ya utekelezaji ni muhimu sana. Jambo lolote lenye sura ya kitaifa kugawanyika" if mishandled" linahitaji umakini mkubwa. Nashauri Rais asikurupuke ili mradi upande wa pili unashinikiza. Dhamana ya usalama wa taifa na utulivu wake uko mikononi mwa Ccm.
 
Hapa umemaliza kila kitu.
Huu ndio ukweli halisi.
Mama alipata Golden chance in political platform lakini akaamua kuichezea nafasi vibaya. Ipo siku itajuta na kuikumbuka hiyo nafasi. Huu ndio ulikuwa wakati bora zaidi kwa mama Samia kuvuna point zote tatu za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kuifungulia nchi kutoka kwenye gereza la utumwa wa utawala wa kimabavu kwa kuwapa katiba mpya.

Sasa amewapa wapinzani agenda nzuri ya kuipinga serikali yake, wapinzani wanaibeba agenda ya Katiba mpya nzima nzima na kwenda kuiuza kwa wananchi, na wananchi watainunua kwa gharama yoyote.

Mama ajiandae kukosa usingizi.
Atapata tabu sana.
 
Tate Mkuu nakusalimia

Katiba mpya ni kwa maslahi ya nchi sio ya Chama
 
Tate Mkuu nakusalimia

Katiba mpya ni kwa maslahi ya nchi sio ya Chama
Ila kwa bahati mbaya hii katiba ya mwaka 1977, iliandaliwa kwa ajili ya kunufaisha vitu viwili tu; ccm na makada wake, na Mwenyekiti/Rais kutoka ccm! Full stop.

Wengine tuliobaki ni maumivu tu. Hili halikubaliki hata kidogo rafiki yangu mama D
 
Tatizo sio ccm tu,imekua ni kasumba ya viongozi wengi wa Afrika, kuweka maslai Binafsi badala ya nchi zao wanazoziongoza, kiongonzi anasema kuleta maendeleo kwenye nchi yake wakati mifumo bora ya kuongeza uwajibikaji ili maendeleo wayasemayo yawepo haupo,inabaki ni utashi wa kiongonzi alipo, alafu utasikia mie mzalendo wizi mtu,
 
Kosa kubwa ni mama aliwapa kichwa kuwa mtandaoni wajadili mambo ya msingi na watachukua ushauri CCM hawata lala salama kwa hili la katiba la litafika kwa wanachi

Hizi katiba ni kwa ajili ya vyama vya siasa na sio wanachi kama wanavyo dai tangu lini mwana siasa akawa yupo juu kwa ajili ya mwananchi badala ya masilahi yake.
 
Nimeishia hapo uliposema kuwa upinzani ulifanya kosa kumsimamisha Lowasa na ndio maana ukashindwa. Kusema ukweli umeongea pumba tu.
 
Kwenye ccm kufariki ndo nimekuelewa hasa. Hii nchi bado ni mfumo wa chama kimoja. Hata wapinzani ni kama wanashindana na goliath. Hawana hadh ya chama cha siasa dhidi ya chama cha siasa kisera na kiitikad. Wanabakishiwa ka roho kiduchu kama tu ishara ya uwepo wa demokrasia
Wanaccmm vigogo na wapambe wameshaiba na kuibiana kwa miongo mingi kiasi hakuna wa kujitoa faham kuikomboa nchi kiuchumi, kisiasa na kifikra. Ndo mana zilizokuwa mali za ccm kikiwa chama dola pekee ati hadi leo ni mali yao badala ya zingerudishwa serkalini hasa viwanja vya wazi na michezo na majengo na kumbi.
Changamoto kubwa ni hatuna wapinzani wa kweli hadi sasa. Sabab wanafanya siasa kwa hisan ya ccm na si kidemokrasia. Wanaofurukuta nao wengi ni juu ya tumbo zao. Ndo mana hoja ya kutathmin malipo yao na KODI hawaip ushirikiano. Hata raia tumeshamezwa na ccm kias kwamba wapinzan wanaonekana wapingaji badala ya sera mbadala. Tusubiri kizaz flan kiishe labda! ccm ndo ikufe. Ni suala la muda tu.
 
Ukweli ni kwamba wananchi wengi kwanza hawajui hata katiba ni nini.

Pili, Ni ukweli usiopingika kwamba CCM bado inao uwezo wa kushinda uchaguzi kwa haki kabisa kutokana na machinery waliyonayo. Makundi yote muhimu kama wazee, wanawake bado yako upande wao.

Vyama vya upinzani vinaungwa mkono na vijana ambao wengi ni OYA OYA, kiasi kwamba kupiga kura inategemea mihemko yao imepandaje.

Tatu, Ni kweli taifa hili linahitaji sera mpya kiuchumi kutokana na wingi wa watu hasa miaka 10 ijayo.

Kwa vyovyote vile kama ni joto la kisiasa litakuwepo hata kama itakuwepo katiba mpya.

Kwanza katiba mpya ni kitu relative sana, haijulikani ni ipi na iliyoje maana mpaka sasa siasa na madaraka tu ndio yameteka mjadala na ndio maana hata imekwama.
 
Well, umejaribu kujibu hoja yangu lakini tatizo moja umemulika hili suala kwa darubini ya kihistoria zaidi ambayo kwa sasa ni kama haina nafasi tena kwenye hili taifa.

Unaanza kwa kusema vuguvugu la katiba halikuanza leo lilianza mwaka 1992, lakini unashindwa kutambua kwamba unafanya reference ya miaka 30 nyuma ambapo population ya Tanzania ilikuwa kama watu milioni 26 na sasa hivi ni watu tunaenda milioni 60 (Tayari kuna tofauti kubwa sana)

Darubini yako pia haijaeleza mchango wowote wa literacy rate ya sasa na ya miaka ya nyuma, kuna issue ya demography pattern ya sasa na kipindi cha nyuma, kuna issue ya mitandao ya kijamii na mawasiliano kipindi cha sasa na kilichopita. Hivi vyote vinafanya matamanio ya katiba kwa sasa na vugu vugu yawe tofauti kabisa na kipindi cha nyuma, sio tu kwa kufananisha na mwaka 1992, bali hili vugu vugu la sasa lina utofauti mkubwa hata na vugu vugu la katiba kipindi cha kikwete.

So, naona moja kwa moja, unakuwa umejifunga kwenye darubini ya historia kuliko uhalisia, whihc means hata hoja uliyoitoa haina nguvu na haipo tangible.

Nakushauri urudi kufanya utafiti tena, unajua kuandika vizuri ila unakosa contents.
 
Vyovyote CCM itavoamua, shida kubwa na ambayo inajulikana ni kwamba CCM wanakwepa mwamvuli wa katiba mpya kwa msingi wa kulinda madaraka na 'doctrine na ideology ya CCM' ila wanasahau kwamba kwa mabadiliko haya ya demographia, kijamii, kiuelewa, ki social media, miaka 10 mpaka 20 itakuwa mingi sana kwa nchi kuendelea kuishi kwa katiba iliyotungwa miaka 50 iliyopita.

Ni changes ambozo itakuwa ngumu kuzizuia.
 
Kwa sababu hakuna tafiti rasmi iliyofanyika, huwezi kusema eti 'wananchi wengi hawajui katiba ni nini' nadhani unafanya makosa makubwa, kwani wewe tafsiri ya wengi maana yake nini?

Na kumbuka kinachopiganiwa hapa kwa mwamvuli wa 'Katiba', ni mjumuisho wa sheri zote kandamizi ambazo watu huku mtaani wamekuwa wakipambana nazo kila uchwao, mambo tunalia dhidi ya ardhi, kodi, demokrasia.. vyote hivo framework yake ni katiba, halafu unasema watu hawafahamu.. sio kweli ... rudi kafanye utafiti tena.

Unasema vyama vya upinzani vinaungwa mkoko na vijana ambao ni OYA OYA... Oya oya maana yake ni nini? jaribu unapotoa mada uwe specific na unachosema, unafanya generalization ambayo inafanya unapoteza maana ya unachosema mkuu.
 
Yaani neno CCM inatakiwa kufa kabisa, hatari ambayo naiona ni kwamba, itafika kipindi hawa viongozi watadhani CCM ni dini ambayo ni dhambi kufa na ambayo ni lazima ilinde kitu ambacho sio sawa
 
Umemaliza kabisa mkuu, hata Kenya uchumi wao upo na nguvu sana sasa hivi ni kwa sababu walikaa chini wakatengeneza katiba ambayo ni bora kwa nchi yao, sisi bado tupo na makasia.. sijui kama tutafika kama viongozi wanaogopa katiba ambayo itanyoosha hizi taasisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…