Kosa la Luhaga Mpina ni nini hadi aandamwe kiasi hiki?

Kosa la Luhaga Mpina ni nini hadi aandamwe kiasi hiki?

Wabunge wa CCM hawatakiwi kufanya kazi yao ya kuisimamia serikali kama walivyotumwa na wananchi.

Mpina ni ‘goody-goody’ kwa mabosi wake wananchi (anaichongea) serikali.

Sasa ukiwa ‘goody-goody’ (mnoko) darasani/shule unaonekana nuksi unajipendekeza kwa walimu.

Anatakiwa akae kimya mawaziri waibe bila ya bughuza kama wabunge wenzake. Hilo ndio lengo la wabunge wa CCM sio kuisimamia serikali.
 
Bunge la kupongeza na kusifu ,, halina maana kihivyo. Bunge kazi yake ni kuisimamia serekali na kuihoji iwajibike ,pia kuwakilisha wanaichi kutoka majimboni mwao. Kama halifanyi hivyo ni la HOVYO TU.
 
Tuanzie hapa:Mpina ni CCM hao wabunge wengine ni CCM. Je inawezekana vipi CCM yenyewe ijishambulie? critical thinkers ndo wanaelewa hapa..
 
Reforms hapo zinahitajika sana watu wengi hawampendi mkuu na wengi wao wanaamini mpina anachofanya ni kitu sahihi sana,
Shida system ya uongozi kiongozi mkuu ni mungu mtu kwenye serikali na chama anaweza aka dictate viongozi wengi nchini waendelee kuwepo ,na hiyo inapelekea watu wajipendekeze na wawashambulie wasema ukweli .

Hapo inapelekea uchawa na mambo mengine na siyo mpina ,gwajima ,Ndugai na wengine wate,hata leo kiongozi yoyote akaenda against na matakwa ya mtawala ataonekana mbaya na atasimagwa haijalishi anachopigania ni sahihi .
 
Back
Top Bottom