Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
- Thread starter
-
- #181
Vipi kuhusu Ulanguzi wa bidhaa hadimu na muhimu huko Tanganyika uliasisiwa na nani?
Teh teh teh teh! Nimecheka sana umekimbia kuedit bandiko lako lakini nimeku-quote post yako kama ushahidi.Mkuu karibu sana,
Daktari
James Emman Kwegyir Aggrey ni sehemu ya wasomi wa mwanzo kabisa barani Afrika,
Tanganyika haitamsahau mtu huyu Daktari
James Emman Kwegyir Aggrey katika harakati za Ukombozi,
Mwaka 1925 miaka miwili kabla ya kifo chake akiwa Gavana wa jimbo la Crown katika serikali ya kikoloni, alifika Tanganyika katika ziara ya kiserikali, ambapo alitumia fursa hiyo kukutana na msomi mwenzie Mwalimu Cesil Matola, Ally Ramadhan, na mhamiaji kutoka Afrika ya Kusini ndugu Kleist Sykes na kuwashawishi waunde chama cha kushughulikia matatizo ya Watanganyika/Wafrika, ambapo 1927 Gavana wa Tanganyika Sir Edward Cameron alikubali kuwaanzishishia chama kiitwacho African Association (AA) ambapo vikao vya mwanzo kabisa vilifanyika nyumbani kwa Mwalimu Cesil Matola mtaa wa Lumumba na swahili ya leo jirani na Bin Slum Tairi,
Licha ya Sir Cameron kuwaanzishia chama hicho pia akawapa nyumba mtaa wa Lumumba ya leo pale makao makuu ya ccm ambayo baadae Klest Sykes alikuja kuwatapeli wenzake na kusema ilikuwa ya kwake,
Dr Kwengyir Agrey ndie aliyetoa msukumo wa mwamko, kwakuwa ndie aliyekuja kuwastua Watanganyika
Dr Vedasto Kyaruzi licha ya kumaliza digrii ya kwanza ya udaktari pale Makerere pia alikwenda nchini Uskochi kuchukua shahada ya uzamivu ya udaktari wa binadamu,
Hebu tumsome hapa kwa kirefu Daktari Aggrey ambae leo Kariakoo anaenziwa kwa kupewa jina la Mtaa ambao zamani uliitwa Stanley lakini sasa unaitwa Aggrey
Hizo spining za kitoto ndiyo zimekufanya ufanye editing bandiko lako acha nipoteze muda kuwafahamisha wana JF ukweli.Ritz
Unapoteza muda wako kwa hizo spining za kitoto,
Soma sheria za jf ujue kwanini uzi huwekwa stick?
Mkuu mada kwa ujumla unamaoni gani?Hizo spining za kitoto ndiyo zimekufanya ufanye editing bandiko lako acha nipoteze muda kuwafahamisha wana JF ukweli.
Hauwezi kutuambia Dr. Vedasto Kyaruzi alikutana na Dr. James Kwegyir Aggrey, wakati Dr Aggrey anakuja Tanganyika Dr. Kyaruzi ana miaka 3.
Halafu hawezi kutuambia Dr. Kyaruzi kasoma Wales wakati siyo kweli baada ya kukwambia kasoma Scotland ndiyo umebadili hata shukrani hauna.
Mimi siwezi kuona uongo nikakaa kimya.
Kwasababu tulikuwa kwenye mfumo wa ujamaa ilikuwa nilazima kuzuia ubepari kwa vitendo kama hivyo.
Ritz
Unapoteza muda wako kwa hizo spining za kitoto,
Soma sheria za jf ujue kwanini uzi huwekwa stick?
Nafikiri Yericko inakubidi UMSHUKURU maalim Ritz kwani nimeangalia na kusoma ile quote aliyotoa kwako na maandiko yako halisi naona kuna mambo ume edit. sasa tueleze nani mkweli au umerekebisha mara baada ya kubanwa KAMA ULIVYO ONDOLEWA KATIKA VARIFIED MAMBER mara baada ya kukubana na kugundulika kuwa SIO miongoni mwa Familia ya Nyerere?
Nakupa kazi kidogo tu mkuu,
Hebu angalia wasifu wangu hapa jf,
Mimi ni verifed member ama laa?
Tena rudia kuangalia,
Mimi ni gold member,
Uliza nguvu niliyonayo hapa jf, mimi na wewe na wenzio akina Ritz nk, hatuwezi kukaa mstari mmoja hapa jf,
Hilo halipingiki, itifaki lazima izingatiwe
Nitarejelea kukueleza kuwa rushwa na mengine ya kufanana nayo vilianza baada ya kristu kuzaliwa na muasisi wake ni Yuda Iskarioti,Hilo lilikuwa by the way. Lakin suala la msingi ni Nyerere ni muasisi wa Ulanguzi na sasa ufisadi huko Tanzania. Je hili unasemaje?
Lakin nieleze ni nguvu gani uliyonayo huko JF kuliko mimi na hao uliowataja?
Je wewe kweli jina lako Yericko Nyerere kweli? au jina la kujibatiza mwenyewe kama mimi ninavyoitwa Barubaru wakti jina langu halisi ni Hamza Yousuf? Je wame verify nini hapo?
Katika kipindi cha "Je tutafika" cha channel ten, Kingunge ameonyesha masikitiko yake kwa kitendo cha JK kuridhia kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya kwa sababu CCM haikuwa imejiandaa kwa mabadiliko ya katiba! Kingunge amedai kuwa CCM iliandaa sera za masafa marefu za 2000 - 2010 na 2010 - 2020 ambazo hakuna hata moja ilikuwa na mpango wa kuandika katiba mpya!
Aidha Kingunge ameishangaa Tume kupendekeza serikali tatu katika katiba mpya kwa kuwa haikuwa sehemu ya hadidu za rejea walizopewa Tume ya Warioba!
Kingunge amesema kitendo cha JK kuridhia kuanzishwa kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ni surprise kwa CCM kwa kuwa haikuwahi kujadiliwa katika kikao cho chote cha CCM!
Naye Vuai Naibu katibu mkuu wa CCM (Zanzibar) aliyeshiriki katika kipindi hicho amesema kuanzishwa kwa serikali tatu ni pigo kwa Wazanzibari kwa kuwa kwa kiwango kikubwa Wazanzibari wamekuwa wanategemea Tanzania Bara kwa elimu, uchumi na shughuli za kijamii!! Amesema katika muundo wa sasa wa muungano Wazanzibari wamekuwa huru kufanya shughuli zao Tanzania bara bila bugudha zo zote!
Aidha Vuai amelaani slogan ya CUF huko Zanzibar inayosema "Tunataka nchi yetu"
Kingunge na Vuai wote wanadhani kitendo cha Warioba kupendekeza serikali tatu ni kuvunja muungano!
Tutafakari upya hoja zetu za serikali tatu au nne zinazopendekezwa wa Wapemba!!
Mkuu asante sana kwa hojaNdugu Yericko Nyerere:
Kuna ukweli katika posti yako. Lakini ningependa kusahihisha kitu kimoja. Kuwa na katiba ni kitu kimoja na kufuata yaliomo kwenye katiba ni kitu kingine.
Kwa kutumia hoja hii si kweli kuwa Afrika haikuwa na wasomi. Afrika ilikumbwa na tatizo la viongozi kutoheshimu na kupindisha katiba kwa matakwa yao. Hili tatizo likiendelea tutaendelea kubadilisha katiba kila kizazi. Hapa ninayo mifano ya kukupa.
Kabla ya kupata uhuru kamili, Ghana ilipewa madaraka ya ndani kwa kipindi cha miaka sita. Katika kipindi hiki Kwame Nkrumah alipewa nafasi ya kupata uzoefu wa western democracy. Uzoefu wa western democracy ilikuwa sio kitu ambacho kinamvutia Nkrumah. Uhuru kamili ulipopatikana na gavana kuondoka, Kwame akaanza kufanya vitu kwa mapenzi yake.
Vilevile nchini Tanganyika au Tanzania, Nyerere alikuwa na mawazo na vitu gani avifanye tukipata uhuru. Kuna vitu Nyerere asingeweza kuvifanya kama tungekuwa na western democracy au tungekuwa na katiba aliyoacha mkoloni. Katika vitu alivyosomea Nyerere nchini Scotland yalikuwa ni masuala ya katiba.
Liberia ni nchi iliyoanzishwa na wamerakani weusi na katiba yao ilifuata misingi ya katiba ya Marekani. Lakini hawakuipa heshima katiba yao.
Zimbabwe ni nchi iliyopata uhuru ikiwa na kila kitu. Lakini Robert Mugabe amebadilisha katiba mara nyingi kukidhi matakwa yake.
Kwa kifupi tu, kubadilisha katiba bila ya kuwa na nia ya kuifuta sio ufumbuzi wa matatizo.
Nitarejelea kukueleza kuwa rushwa na mengine ya kufanana nayo vilianza baada ya kristu kuzaliwa na muasisi wake ni Yuda Iskarioti,
Mwalimu Nyerere alizaliwa na kuyakuta,
Alichofanya ni kupunguza ukuaji wa hali hiyo kwa kutia mkazo adhabu stahiki. Yani unakwenda jela miaka miwili, na viboko ishirini na viwili, kumi na mbili unapoingia na kumbili unapotoka ukamuonyeshe mkeo,
Jina langu halisi ni hilohilo Yericko Yohanesy Nyerere,
Ukitaka kuthibitisha ingia kwenye tovuti ya wizara ya mambo ya ndani, wizara ya elimu, mamlaka ya vitambulisho vya taifa, daftari la wapiga kura Tanzania, mamlaka ya uandikishaji vizazi na vifo,uhamiaji, wizara yamambo ya kigeni,
Na zaidi ukijisikia nenda ikulu ya Tanzania muone rais wa Tanzania anaitwa Jakaya Kikwete, mwambie unataka kumfahamu Yericko Nyerere wa Tanzania na jf, haitachukua saa moja kabla sijaletwa mbele yako,
Kuhusu nguvu niliyonayo hapa jf,
Nimekupa fursa kuwa waulize wanajf wenyewe kama Mohamed Said, Ritz, The Big Show, Boko Haram nk,
Hawa watakupa ukweli,
acha uzandiki na kujipaka kinyesi
Nyerere hana watoto au wajukuu wajinga kama wewe, katika wajukuuu au watoto wa nyerere lukuki wewe tu ndio uko masaa yote JF haujishtukii..............unaharibu jina la Nyerere
mjinga
Jason na Yericko mna ungudu?