Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Ni kama vile ''ile pesa tuma kwa namba hii'' Wengi wanajua kabisa ule ni uongo, ila ni wachache sana ambao hata wanaelewa wale wahuni huwa wanapataje namba zao. Kujua tatizo inaweza kusaidia ktk kupambana nalo.
Tuachane na hayo.
Huo ujumbe hapo juu ukisema u-report. Maana yake unam-report huyo mtumaji hapo na WhatsApp wata-review hiyo sms na possibly hata kufikia uamzi wa ku-ban hiyo account.
Wanaojua, wanajua kwamba hata huyu aliyetuma hapa nae ni victim. Ameikuta pahala akafata process ya kujizolea hizo GB's, akaambiwa a-share kwa watu kadhaa na groups mpaka ikafika humu.
Kwa mfano, huyu mtu account yake ikawa banned. Kwa kukiuka sheria na sera za usalama WhatsApp, kosa ni la nani? Tunaweza kusema kosa ni la kwake, sababu ya ujinga wake. Ndio ni kweli!
Jukumu la kuifanya WhatsApp kuwa sehemu salama ni la WhatsApp na Mtumiaji mwenyewe. Kila mmoja anao wajibu wake hapa. Na kama tunavyoona tatizo bado lipo!
Hivyo, naona ipo haja ya Mtumiaji kuongeza nguvu kwenye wajibu wake; kuongeza umakini na uwelewa.
Vile vile ipo haja pia ya WhatsApp kuongeza nguvu kwenye wajibu wake; uwelewa kwa watumiaji wake. Kuja na mbinu nzuri zaidi za kupambana na spam na scams hasa upande wa links, pasipo kuingilia uhuru wa Mtumiaji.
Salamu.
Ipuli Boy