Kosa wanalolifanya watu wengi na kuwagharimu katika maisha yao yote.

Kosa wanalolifanya watu wengi na kuwagharimu katika maisha yao yote.

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Katika maisha watu wengi wanasahau kuweka kumbukumbu ya watu wanaokutana nao na reactions zao.

Kila mtu unayekutana anaweza kuwa daraja la kupanda , kushuka au neutral yaani ni mtu tu hana msaada kwako na hawezi kuwa daraja la kukushusha.

Mtu ambaye ni adui atabaki kuwa adui tu maisha yako yote.

Hilo lazima ulitambue.

Hii ni tofauti na tunavyofundishana kanisani kuwa usimweke moyoni mtu. Sizungumzii umweke moyoni na umchukie bali kila utakapokutana naye ishi naye kwa tahadhari.

Mtu aliyewahi kukufanyia ubaya usitarajie kuwa atabadilika juu yako na kukutendea mema ingawa anaweza kukufanyia mema kwa muda kulingana na mazingira ila ukimpa nafasi zaidi atakuua au kukuharibia njia zako.

Maana ni yeye tu peke yake ndiye anaweza kujua lililojificha moyoni mwake. Kama amebadilika au hajabadilika wewe hupaswi kujua.

Wengi wameharibikiwa zaidi baada ya kuwaamini waliowahi kuwa maadui zao.

Mwanamke alikuwa anakutema mate leo hii umepata kazi au amejua kuwa ni mtu mzito anakuchekea na wewe na ujinga wako unakwenda kumwoa.

Ndugu yako fulani alikuwa yuko kinyume nawe eti leo hii unafurahia ukaribu wenu. Utakufa amka.

Kazini kuna mtumishi mwenzako alikuwa kinyume nawe leo hii mnakula pamoja, amka utakwisha.

Kumbuka watu waliokuwa nawe tangu day 1. Hao ambatana nao mpaka kifo chako.

 
Yote mema, nishachoka kukaa na kinyongo kuwindana windana windana na watu.
 
Duuh kuna dada fulani nilikuwa namuelewa sana ila nilipofanya maombi alinifungia kiyoo kwa speed kali mno ila alipopata taarifa zangu nyeti naona ananitafuta tu..eti anasema hakunijua vema tungeanza na urafiki...
 
Duuh kuna dada fulani nilikuwa namuelewa sana ila nilipofanya maombi alinifungia kiyoo kwa speed kali mno ila alipopata taarifa zangu nyeti naona ananitafuta tu..eti anasema hakunijua vema tungeanza na urafiki...
Huyo nyau ibuni pusi mkimbie mita 2000
 
Back
Top Bottom