Kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa. Najuta

Pole, yalinipata mpaka nilichanganyikiwa, nilimpeleka mahakamani, hakimu akamuuliza mke wangu kama bado anahitaji ndoa, eti akasema bado ananitaka, hakimu akamwambia labda anania na kitu kingine ila sio ndoa. Maana hakimu (tena ni mwanamke) alimshangaa mwanamke mwenzake kwa yale anayoyafanya kwenye ndoa, mwishoalitoa hukumu ya kuvunja ndoa. Mpaka nimenenepa aisee, mwanamke anakutesa mpaka uwaza kutenda jinai
 
Ukioa wa pili utakosea zaidi cha kukushauri tengana nae tu ishi single na ulee wanao tu, Hawa wanawake wa sasa wasioridhika japo tu kwa uumbaji wa MUNGU aliewapa kucha,Rangi,Nywele na maumbo mazuri lakini wanaishia kwenda kujibadili na kuweka feki, Yaani ashindwe kuridhika na yote MUNGU aliyomfanyia ndo Leo aje aridhike na anachomfanyiwa na Mumewe? mwisho wa siku ni Mgogoro tu.

Sent from my TECNO CD6j using JamiiForums mobile app
 
Kosea Kuoa/Kuolewa Maana Mtaachana Tu
Lakini Ukikosea Kuchagua Ni Mpaka Miaka Mitano Tena
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,~~••~~~~~~~••••••~~~~~~~,,,,,,,,,,,,,,,,
Hapo Kwako Kazi Ipo Yaani Wazigua Wanasema Kozeza Umo
 
Mtafute MUNGU wa kweli ukimpata utaridhika lahsivyo sahau kuridhika, Duniani tunapita tu imagine Kila kitu utakachotaka Sasa hivi unakipata, Je, unafikiri utakuwa na furaha??? hapana, hii ni kwa sababu utakuwa overstressed kwa ajili utakuwa ukiwaza tu Kuwa kilichobaki ni kifo[emoji23][emoji23][emoji23] Jambo ambalo laweza kukunyima raha kabisa.

Sent from my TECNO CD6j using JamiiForums mobile app
 
Huwa anaonesha gubu na kiburi ukimfanyia nini?ama ni kila siku zote na muda wote yuko hivyo?

Miaka sita ni mingi kumvumilia mtu wa namna hiyo....
 
Ukimuacha, watoto watalelewa na Nani? Umeona mapungufu yake wewe huna mapungufu???

Kesi hii haiwezi kuamuliwa kwa malalamiko ya upande mmoja!

Madhara ya kuachana yatawakuta watoto ambao ugomvi wenu wala hauwahusu!
 
Ukishakuwa na hela unaanza kuwaza kuhusu afya yako na namna ya kukiepuka kifo.yaani mtu angenunua kutokufa.
Maiko Jackson alikuwaga na 8 doctors wa kumuangalia afya kila mtu idara yake Ila still hatunaye
 
Umeeleweka [emoji419]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…