Kosea vyote, usikosee mume

Kosea vyote, usikosee mume

Joined
Jul 29, 2021
Posts
81
Reaction score
158
Aisee aikwambie mtu kosea kuchagua nguo, utabadilisha, kosea rafiki utawapotezea lakini usikosee mume. Ukikosea mwanaume wa kuolewa nae tu, umekosea kila kitu. Kikweli wanaume wa siku hizi, hawana uchungu hata kidogo na familia zao.

Utakuta mume ana mke na watoto lakini Bado anaongozwa na maeneno ya ndugu zake na mama yake. Sisemi kuwa Ni vibaya kuisikiliza wazazi wako na dada na Kaka zako la hasha. Unaweza kuwasikiliza lakini maneno ya kuambiwa changanya na ya kwako.

Wewe nii mume sasa na sio mtoto mdogo, unafamilia hao ndio kaka na dada zako wa kwanza, damu yako. Ndio watu wa kwanza unaotakiwa kuwasikiliza.

Unakuta mwanaume anapata mshahara wote anampelekea mama yake, mke akiitaji matumizi anaambiwa akayafutae kwa mama mkwe, hivi kweli jamani?

Wengine wanaleta wazazi, hasa mama zao waje wakae Hapo anapoishi na mke wake. Hivi unadhani Ni ustaarabu kwa mama kusikia mambo yote mnayoyafanya mkiwa chumbani.

Mnakosa hata muda wa faragha kati yenu mwishowe mnajikuta hamna mapenzi Tena kwenye ndoa kwasababu hamuhudumiani.

Na mwanamke hawezi kukuambia usimlete mama yako, kwasababu ataonekana ana roho mbaya. Ila ukweli ndio huo.

Wanaume wengine mkipata pesa kidogo tu mnataka ujionyeshe kwa watu kuwa wewe una mapesa, eti unaweka heshima baa. Embu acheni ujinga mkalee familia zenu. Kama hamuyataki majukumu kwanini mmeingia kwenye ndoa?
Wanaume mjirekebishe jamani, inasikitisha Sana.
 
Aisee aikwambie mtu kosea kuchagua nguo, utabadilisha, kosea rafiki utawapotezea lakini usikosee mume. Ukikosea mwanaume wa kuolewa nae tu, umekosea kila kitu.
Kikweli wanaume wa siku hizi, hawana uchungu hata kidogo na familia zao.

Wanaume mjirekebishe jamani, inasikitisha Sana.
Kwahiyo mume asipende Ndugu wala wazazi wake?;;
 
‘Utaonekana una roho mbaya?’

Kwanza nikutoe hofu ni kweli una roho mbaya ya asili kwahiyo usijali kuhusu kuonekana maana hata hapa kwenye uzi wako kuna chembe chembe za karoho kabaya.

Sasa badilisha uzi wako uandike usikosee ukaolewa na mtoto wa mama.Wewe umeolewa na mtoto wa mama na watoto wa mama wote ndo tabia zao hizo m,ulipaswa kujua mtoto wa mama akikuoa ujue umeolewa na mama yake pia.

Punguza kisirani kidogo inawezakana ukatatua 50% ya matatizo uliyonayo kwenye ndoa yako.
 
Sasa kama mwanamke hajui matumizi ya fedha unataka nifanyeje?!!.. Kwahiyo nikiwa na chumba kimoja mama yangu haruhusiwi kuja kunitembelea!!??..
Tafuta kwanza nyumba yenye vyumba zaidi ya kimoja ndo umlete Mama.Hapo sebuleni Ni kudhalilisha huyo bibi Na Kama mwanamke hajui matumizi ya pesa kwanini usimpe kidogo kidogo kadri unavyoona inafaa? Acha kumtesa mtoto wa watu.
 
Kwani wote tunaweza kuwa na vyumba zaidi ya kimoja?!!..Hivi unajua huko vijijini watu wanaishije?!..
 
Tafuta kwanza nyumba yenye vyumba zaidi ya kimoja ndo umlete Mama.Hapo sebuleni Ni kudhalilisha huyo bibi Na Kama mwanamke hajui matumizi ya pesa kwanini usimpe kidogo kidogo kadri unavyoona inafaa? Acha kumtesa mtoto wa watu.
Kwahiyo nikiwa sina uwezo nisioe na pia mama yangu asije kunitembelea!!..Hebu fikiri kama mwanadamu kidogo!!!
 
Kwahiyo nikiwa sina uwezo nisioe na pia mama yangu asije kunitembelea!!..Hebu fikiri kama mwanadamu kidogo!!!
Kwaiyo akikutembelea ndo alale hapo ??
Yaan wewe na mke wako mmelala kitandani alafu Mama yako naye amejikunja chini hapo, ukimshika tako mkeo bi mdashi anajifunika uso [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom