Kozi gani kijana wa kiume asomee VETA?

heartbeats

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
6,736
Reaction score
10,669
Wakuu, nina mdogo angu age 18 kamaliza four mwaka huu, bila shaka hatoweza pata maksi za kwendelea. Sasa ni kozi gani ambayo itamsaidia mbeleni uko hata kwa kujiajiri.

Ya kwanza napendekeza udereva, ila ningetaka kujua na nyingine ambayo haitopitwa na wakati maana maendeleo haya ya sayansi isije ikamkosti.

Yani kitu ambacho hata akitoka nje ya nchi anaweza jiendeleza kiasi na kufanya mambo yake vyema.

Hakusoma sayansi.
Nawakilisha.
 
Udereva ndio,lakini udereva wa nini? Jibu sio ma magari !

Akasomee udereva wa bulldozer,kijiko,katapila huko kuna hela za maana na ajira zipo (mashine kubwa za ujenzi wa barabara),winchi.

Akasomee ufundi madilisha ya vioo(Aluminium).

Akasomee kuunganisha vyuma(kuchomelea)

Akijua moja ya hizi kazi anaweza kujiajiri au kuajiliwa na maisha ya mjini atayaishi fresh tu.

Lakini sio udereva wa kawaida huu
 
Mpeleka Veta Shinyanga akasomehe Ufundi Mitambo ,, ikiwemo Excavator, Motor Grader na Greder
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…