Tutapata huzuni ya kukoksa mteja, kama ilivyo kawaida ya biashara zote, unapompoteza mteja, lazima uhisi ovyo, lakini kama mteja mwenyewe siku zote ana tabia na wivu wa kike na maringo na majigambo na mikwara na asiyetabirika wala kueleweka ilhali ukiangalia kwenye mapato unakuta asilimia yake ni ndogo sana (negligible), basi unamwondolea mbali ili udumishe mibaba ya biashara.
Sasa nyie hizo sifa zote mbaya mnazo, lakini tatizo tumeunganishwa na nyie kwenye kiuno, hivyo inabidi kuwavumilia tu, ni kama kwamba kijijini uwe na ndugu yako mkubwa, ambaye ni mzembe, mzushi, mwenye wivu siku zote na asiyejiamini na huzua ugomvi kwa kila kitu na kila akiona unafanya maendeleo anakerwa, sasa unakua huna jinsi maana ni kakako na utaendelea kuishi naye mkao wa kumkwepa kwepa tu ilmradi siku zisonge.