KQ yakiri kupata hasara kubwa kutokana na kufungiwa safari za Tanzania

KQ yakiri kupata hasara kubwa kutokana na kufungiwa safari za Tanzania

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Shirika la ndege la Kenya Airways linasema kuwa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania haijabatilisha uamuzi wa kufuta kibali cha kuziruhusu ndege zake kusafiri nchini humo takriban wiki moja baada ya Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Macharia kueleza kuwa nchi hizo mbili zimefikia makubaliano.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika hilo la Kenya, Allan Kilavuka, ameeleza kuwa usimamizi wa KQ unasubiri jibu kutoka kwa serikali ya Kenya kwa sababu bado hawajapata idhini ya kusafiri Tanzania.

Takriban wiki moja baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa imefanya mazungumzo na Tanzania kusuluhisha mgogoro ulioibuka Ijumaa wiki iliyopita baada ya Tanzania kutangaza kufuta ndege za shirika la ndege la Kenya Airways(KQ) kufanya safari zake humo katika viwanja vyake vya ndege vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar, Kenya Airways inasema bado hamna jibu ya kufanya safari nchini humo.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hilo Allan Kilavuka ameeleza VOA kuwa shirika hilo linasubiri maelekezo kutoka kwa serikali ya Kenya kujua utaratibu uliopo.

Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya James Macharia wakati akizindua safari za ndege za Kenya Airways to nchi 30 wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) alieleza kuwa amefanya mazungumzo na Waziri wa Kazi, uchukuzi na mawasiliano nchini Tanzania Isack Aloyce Kamwelwe na kukubaliana mgogoro huo.

Hata hivyo, Bw Kilavuka anakariri kuwa Kenya Airways haiwezi kufanya chochote ila kusubiri jinsi mgogoro huo unavyosuluhishwa na mamlaka husika za serikali hizi mbili.Lakini anaeleza kuwa kusitishwa huko kuna athari kubwa kwa Kenya Airways.

Hatua hiyo ya Tanzania ilifuatia tangazo la serikali ya Kenya kutoiorodhesha nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi 11 ambazo wasafiri wake wanaruhusiwa kuwasili Kenya wakati usafiri wa kimataifa unaporejea.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga nchini Tanzania (TCAA), Hamza Johari alisema serikali ya Tanzania imesimamisha mara moja safari za ndege za shirika la Kenya Airways kutoka Nairobi kutua viwanja vyake kufuatia tangazo la Kenya kuiacha nje ya nchi zinazoruhusiwa kufanya safari humo.

Hata hivyo siku moja baadaye, Kenya ilitoa ufafanuzi kuwa haijapiga marufuku ndege za Tanzania kuingia nchini mwake hata kama si miongoni mwa nchi zilizoorodheshwa ndege zake kuingia anga ya Kenya.

Kenya Airways ilirejelea safari za ndege za kimataifa Agosti mosi mara ya kwanza baada ya kusitisha safari hizo Machi mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mgogoro kuhusu safari za Tanzania bado kutatuliwa, yasema Kenya Airways

MY TAKE: Magufuli shikilia hapo hapo Hakuna kuwaruhusu hawa wajinga kwasasa hadi wapige magoti.
 
Serikal ya Tz nayo inatakiwa kuwa peleka qarantini wakenya wanaoingia Tz na KQ ila wathungu wasiende karantin na wabongo wenzetu wasiende karantin ila mkenya ni kumpima kumtwanga + ve corona kumrejesha kwao.
 
Watalii hatuwezi kuwakosa eti kisa KQ haitui Tanzania, kuna options nyingi za airlines to Tanzania apart from KQ so ni kiasi tu cha kuswitch to the other options na hata kama wapo watalii waliokuja na KQ bado RwandAir ina route ya Nairobi to Dar as well

So technically hatuumii sisi bali wakenya ndio wanaumia na hii iwe fundisho, waziri amekaririwa akisema this time hatutakaa nao kwenye mazungumzo kama watu waelewa kutokana na walichofanya baada ya mazungumzo ya malori mipakani, walikubaliana vizuri lakini wakaja kukiuka makubaliano

So saivi tumewachukulia kama watu wenye matatatizo ya akili ndio maana hata hatuna muda na mazungumzo wanayolilia, tutazungumza nao tukijisikia na tutachokubaliana nao tutachukichukulia kama tumekubaliana na mwendawazimu nothing serious to expect from.
 
Huu mgogoro umesababishwa kwa kiasi kikubwa na Papamagamba Kabudi kukosa hekima ya kiuongozi na kidiplomasia.
Wao walivyotuzuia walifanya hekima,alafu comments zako, hua za kitoto Sana mkuu, ila samahani, nina unakika wewe elimu yako ni darasa la Saba,au form 4, umejitahidi Sana, form 6, alafu ukafeli.kama unabisha, prove me wrong.
 
Kwa mtu anayejuwa biashara na anafahamu vizuri KQ asingeifungia kuleta abiria hapa
Umemwaga ugali sisi tunamwaga mboga! Lazima tuheshimiane! It is tit for tat. We are teaching you a reciprocal relationship!! Before you act in relation to Tanzania always expect a reciprocal response! Usilie huo ndio utaratibu mpaka tuheshimiane!
 
Nyie mbona mna akili za kijinga? Hivi unafikiri inaathirika kenya peke yake kwa kuzuia ndege za KQ kuja TZ? Nyie ndio manaomdanganya JIWE na anafanya mambo yanayoharibu uchumi na uhusiano wa kimataifa.
Hivi akili zako umezisahau wapi? Yaani Kwa akili yako unafikiri walichikifanya Kenya kuzuia ndege toka Tz ndio kuboresha uhusiano Wa kimataifa na kuboresha uchumi au?? Hakuna kuongea nao wapuuzi hawa, tumechoka!! Hivi Kwa akili yako hizo nchi walizizifungulia hazina corona au? Kenya ni ya 7 katika Africa Kwa wingi Wa maambukizi ya Corina, halafu wanataka dunia iamini Tz ndo kuna corona zaidi!! Inabidi mtu awe mwendawazimu kwanza kuamini kuwa Tz kuna tatizo kubwa la corona!

Mkubali msikubali Mungu ameiondoa corona Tanzania Kwa ajili ya utukufu wake mwenyewe!! Tulipotangaza kumtegemea Mungu mlitubeza! Mkasema watu watajifia barabarani, hilo halijatokea! Shule zotezimefunguliwa na hakuna tatizo lolote! hakuna vifo wala mtoto wake na vifo!

Lakini huko Kenya kiburi cha kutikumheshimu Kwa kufunga nyumba za ibada kinawatafuna!!
 
Nchi ya Kenya imekubalia tu nchi kumi, kati ya nchi zote zingine, kwenye usafiri wa anga. Vipi kuhusu route zingine zote pia ambazo zimekwama kwasababu ya COVID-19? Hivi mnadhani KQ huwa inapiga route kienyeji za daladala kama wale ambao sitawataja kwa jina?

Hebu chambueni vizuri hii ramani ya route za KQ kote duniani.

images
 
Back
Top Bottom