KQ yakiri kupata hasara kubwa kutokana na kufungiwa safari za Tanzania

KQ yakiri kupata hasara kubwa kutokana na kufungiwa safari za Tanzania

Nchi ya Kenya imekubalia tu nchi kumi, kati ya nchi zote zingine, kwenye usafiri wa anga. Vipi kuhusu route zingine zote pia ambazo zimekwama kwasababu ya COVID-19? Hivi mnadhani KQ huwa inapiga route kienyeji za daladala kama wale ambao sitawataja kwa jina? Hebu chambueni vizuri hii ramani ya route za KQ kote duniani.
images
It seems ATCL is the only airline making profit with parked planes, hawa wasee ni wathick bana
 
joto la jiwe,

Walizoea kujaeibu sasa hivi namuomba muheshimiwa Rais Magufuli asiwafungulie mpaka wakubali masharti yafuatayo 1: Abiria yeyote kutoka TANZANIA hatokaa karantini wala kupimwa korona Kenya anatoka na cheti tu kutoka TANZANIA, na wakikubali masharti hayo tunawapa mwezi mmoja wa kuandaa kituo cha kutoa vyeti vya Corona. Mwisho watatamani twende bila vyeti maana mwezi wa kuandaa kituo kwao mwaka.
 
Nchi ya Kenya imekubalia tu nchi kumi, kati ya nchi zote zingine, kwenye usafiri wa anga. Vipi kuhusu route zingine zote pia ambazo zimekwama kwasababu ya COVID-19? Hivi mnadhani KQ huwa inapiga route kienyeji za daladala kama wale ambao sitawataja kwa jina? Hebu chambueni vizuri hii ramani ya route za KQ kote duniani.
images
Tumekuwekea taarifa toka kwa viongozi wa KQ wenyewe wanasema wanapata hasara kubwa kwa kufungwa kwa safari za Tanzania, wewe unahisi wanasema uongo?, kweli wewe ni mkikuyu usiyekua na akili unatetea kila ujinga wa setikali ya Jubilee
 
Watalii hatuwezi kuwakosa eti kisa KQ haitui Tanzania, kuna options nyingi za airlines to Tanzania apart from KQ so ni kiasi tu cha kuswitch to the other options na hata kama wapo watalii waliokuja na KQ bado RwandAir ina route ya Nairobi to Dar as well
hivi vitu haviendi kienyeji kama unavyofikiria. Kuna watalii aina mbili, wanaojuoa wanapotaka kwenda na kuplan in advance hawa wataenda popote bila kujali vikwazo au gharama ila kuna level ikifika wanabadili plan. wapo wanaoshawishiwa na matangazo, travel agents, offers, gharama na wepesi wa safari. Sawa kukosa kabisa haiwezekani lakini kupungua watapungua. Not good for business.

So technically hatuumii sisi bali wakenya ndio wanaumia na hii iwe fundisho, waziri amekaririwa akisema this time hatutakaa nao kwenye mazungumzo kama watu waelewa kutokana na walichofanya baada ya mazungumzo ya malori mipakani, walikubaliana vizuri lakini wakaja kukiuka makubaliano
Sijui kama umewai kusafiri point A to C via B, nitofauti sana na kusafiri point A to B alafu point B to C. Gharama inaongezeka kwa %kubwa hasa safari za ndege. Sasa KQ inaaminika huko duniani, ni mshiriki wa skyteam na inaroute nyingi. Kusema sisi hatuumii ni kuwaza pafupi sana. hapa kilammoja anapoteza.
 
Huu mgogoro umesababishwa kwa kiasi kikubwa na Papamagamba Kabudi kukosa hekima ya kiuongozi na kidiplomasia.
Chizi we, badala ya kulalamikia ulipo jikwaa unalalamikia ulipodondokea !! Naona kuna kitu hujui nikukumbushe, TANZANIA ilifungua anga lake kwa nchi zote duniani bila masharti na ndio nchi pekee duniani iliofanya hivyo mpaka sasa hamna nchi yeyote iliyoweza kufanya hivyo uelewe.

Sasa Kenya anavyofungua kachukua nchi 11 akiwemo na Uganda TANZANIA kamuacha maana yake Kenya na Uganda wapo salama ila TANZANIA maambukizi yapo juu au hali mbaya, lakini wakati huohuo Kenya inavyofanya hivyo akili yake zote kwenda TANZANIA kwenye wagonjwa wengi sasa propaganda hizi za kitoto muheshimiwa Kabudi anazishughulikia kisawa sawa na kama roho inauma jinyonge maana huu ni mwanzo yatakuja makubwa kuliko hayo bora ufe mapema usije ukaumia roho zaidi.
 
Shirika la ndege la Kenya Airways linasema kuwa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania haijabatilisha uamuzi wa kufuta kibali cha kuziruhusu ndege zake kusafiri nchini humo takriban wiki moja baada ya Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Macharia kueleza kuwa nchi hizo mbili zimefikia makubaliano.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika hilo la Kenya, Allan Kilavuka, ameeleza kuwa usimamizi wa KQ unasubiri jibu kutoka kwa serikali ya Kenya kwa sababu bado hawajapata idhini ya kusafiri Tanzania.

Takriban wiki moja baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa imefanya mazungumzo na Tanzania kusuluhisha mgogoro ulioibuka Ijumaa wiki iliyopita baada ya Tanzania kutangaza kufuta ndege za shirika la ndege la Kenya Airways(KQ) kufanya safari zake humo katika viwanja vyake vya ndege vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar, Kenya Airways inasema bado hamna jibu ya kufanya safari nchini humo.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hilo Allan Kilavuka ameeleza VOA kuwa shirika hilo linasubiri maelekezo kutoka kwa serikali ya Kenya kujua utaratibu uliopo.

Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya James Macharia wakati akizindua safari za ndege za Kenya Airways to nchi 30 wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) alieleza kuwa amefanya mazungumzo na Waziri wa Kazi, uchukuzi na mawasiliano nchini Tanzania Isack Aloyce Kamwelwe na kukubaliana mgogoro huo.

Hata hivyo, Bw Kilavuka anakariri kuwa Kenya Airways haiwezi kufanya chochote ila kusubiri jinsi mgogoro huo unavyosuluhishwa na mamlaka husika za serikali hizi mbili.Lakini anaeleza kuwa kusitishwa huko kuna athari kubwa kwa Kenya Airways.

Hatua hiyo ya Tanzania ilifuatia tangazo la serikali ya Kenya kutoiorodhesha nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi 11 ambazo wasafiri wake wanaruhusiwa kuwasili Kenya wakati usafiri wa kimataifa unaporejea.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga nchini Tanzania (TCAA), Hamza Johari alisema serikali ya Tanzania imesimamisha mara moja safari za ndege za shirika la Kenya Airways kutoka Nairobi kutua viwanja vyake kufuatia tangazo la Kenya kuiacha nje ya nchi zinazoruhusiwa kufanya safari humo.

Hata hivyo siku moja baadaye, Kenya ilitoa ufafanuzi kuwa haijapiga marufuku ndege za Tanzania kuingia nchini mwake hata kama si miongoni mwa nchi zilizoorodheshwa ndege zake kuingia anga ya Kenya.

Kenya Airways ilirejelea safari za ndege za kimataifa Agosti mosi mara ya kwanza baada ya kusitisha safari hizo Machi mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mgogoro kuhusu safari za Tanzania bado kutatuliwa, yasema Kenya Airways

MY TAKE: Magufuli shikilia hapo hapo Hakuna kuwaruhusu hawa wajinga kwasasa hadi wapige magoti.
Siku kizuri, kumbuka hilo shirika limeajiri watanzani pia, sasa likipata hasara, ajira za wabongo pia zinakuwa mashakani.
 
Kwahiyo bangi za Uhuru na konyagi za mbowe azihusiki
Hawa c ndio wale wafuasi wa yule Rais wao Sera zake kulalamika tu madala ya kuwahidi wananchi nitafanya iki anabaki ooh uchumi umeshuka, nimekaa ulaya mwaka na lakini sijaona kama huku , Ulaya watu wanaandamana bila shida mgongoni nina goroli sasa kama akili ya Rais wao zipo hivi unategemea wafuasi watakua na uwezo wa kuchanganua mambo?
 
Pimbi wewe,wao walivyotuzuia walifanya hekima,alafu comments zako,hua za kitoto Sana mkuu,Ila samahani,nina unakika wewe elimu yako ni darasa la Saba,au form 4,umejitahidi Sana,form 6,alafu ukafeli.kama unabisha,prove me wrong.
Mbona unawatuc watu huyu mtoto wa mtaani ajasoma kabisa. Darasa la Saba anauwezo wa kua mbunge na akaweza kuendesha Jimbo lake.
 
Siku kizuri,kumbuka hilo shirika limeajiri watanzani pia,sasa likipata hasara,ajira za wabongo pia zinakuwa mashakani
Hata tulipoamua kwenda vitani na Uganda tulijua kwamba kuna watanzania wengi watakufa na uchumi utasambaratatika, tungeweza kukaa kimya na kumuacha Idd Amin afanya vile atakavyo kwa kuogopa hasara, lakini tuliamua kukubali hasara ili kulinda heshima ya Tanzania na kuhakikisha kwamba chokochoko zinafikia mwisho na hazitojirudia tena, tulifanikiwa Sana.
 
hivi vitu haviendi kienyeji kama unavyofikiria. Kuna watalii aina mbili, wanaojuoa wanapotaka kwenda na kuplan in advance hawa wataenda popote bila kujali vikwazo au gharama ila kuna level ikifika wanabadili plan. wapo wanaoshawishiwa na matangazo, travel agents, offers, gharama na wepesi wa safari. Sawa kukosa kabisa haiwezekani lakini kupungua watapungua. Not good for business.


Sijui kama umewai kusafiri point A to C via B, nitofauti sana na kusafiri point A to B alafu point B to C. Gharama inaongezeka kwa %kubwa hasa safari za ndege. Sasa KQ inaaminika huko duniani, ni mshiriki wa skyteam na inaroute nyingi. Kusema sisi hatuumii ni kuwaza pafupi sana. hapa kilammoja anapoteza.
Kila mmoja anapoteza ila Kenya anapoteza zaidi ,hivi unajua Kenya inapata abiria huko nje kupitia vyanzo vya utalii vya TANZANIA? Sasa kQ kama ikifungiwa kuingia TANZANIA hata ruti zao za kimataifa zitaumia maana ule uongo wao wa kuwaambia wazungu karibuni Kenya muone mlima Kilimanjaro kisha wawaambie ukitaka kuupanda twendeni kule upande wa Tanzania uongo huu utakua hufanyi kazi tena.

Kwahiyo kitakachotokea mtalii alietaka kwenda Serengeti na mt Kilimanjaro atabalidi shirika la ndege badala ya kenya atatumia mashirika mengine .Na Dunia zima inajua kama ukienda kenya Tanzania hukanyagi sasa lazima mpaka huko duniani mashirika ya Kenya yatanyanyapaliwa Kwasababu ktk utalii Kenya hata kitu anachotegemea kutoka vyanzo vya TANZANIA ndio maana ndege zao unaona wameandika majina ya vivutio vya utalii wa Tanzania sasa wewe sijui uchumi unaozungumzia uchumi gani wa kuangalia mwisho hapo kwenye vidole vyako vya miguu ,uchumi mpana usiangalie faida ya malipo ya kutua na maegesho tu ambayo ni ela ya mboga tu angalia Kwa upana na ndio maana unaona hata wenyewe wanalia lia usizani wanalia Kwasababu ya safari za TANZANIA tu laa wanalia hata safari za huko nje zimevurugika .
 
Nyie mbona mna akili za kijinga? Hivi unafikiri inaathirika kenya peke yake kwa kuzuia ndege za KQ kuja TZ? Nyie ndio manaomdanganya JIWE na anafanya mambo yanayoharibu uchumi na uhusiano wa kimataifa.
Kwaiyo ww ungekuwa pale kweny nafasi ile g mamuzi ungeanza kumbembelez Mkenya sio?
 
Wewe unae elewa ulitakiwa useme...km hujui pia funga bakuli
Hivi unadhani ndege zinatua na kuondoka bure pale, unadhani wageni wanakuja na teksi zao, unadhani wanakuja na bidhaa zao za matumizi kwenye mabegi, unadhani wanalala kwenu.
 
Back
Top Bottom