KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

KRA vs TRA: Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania

Unashindwa kuelewa:

Kenya uzalishaji wao ni zaidi ya mara 3 ya Tanzania.

Obviously kodi lazima iwe mara tatu ya Tanzania.

Tanzania ni li-welfare state,kila kitu serikali eti inatoa bure wakati serikali haina hela hivyo Wananchi hawafanyi kazi seriously maana kila kitu eti serikali inatoa free.

Serikali ndio tatizo,huwezi ongeza uzalishaji kwenye nchi kwa kutoa vitu vya bure,vitu vya bure vina incentivize watu kutofanya kazi maana vitu ni vya bure!

Kitakacho okoa Tanzania ni Capitalism ya kweli.

Kama cure for poverty ni wealth,then lets talk about uzalishaji na sio hii legalized theft inayofanya serikali hovyo ya Tanzania kutoka kwa wazalishaji wachache na kugawa kwa wapumbavu 75% ya wananchi for free.

Asante
Hakuna mnachozalisha mara 3 ya Tz punguza upuuzi.turudi kwenye gpd per capital Tz $1080 ke $1900 ,yani kwa kifupi mnazalisha mara mbili kasoro kidogo.
 
[emoji1][emoji1] geza ulole na wewe pia.. basi bongo ni shida.. anyway tufanye TRA kinara wa kukusanya kodi africa.
Sio na wewe pia! Usifikiri wote ni zero brain kama wewe, wengine hizi ndio kazi zetu tupo kwenye vitengo husika, na kushangaa unaongea utopolo bila Soni.

Hujui hata unaongea nini masikini
 
Hapana JPM hana basic knowledge ya uchumi, yeye ndo ana demoralize watumishi wa TRA, mtaalamu wa uchumi huongozwa na economic statistics na data sio na political statements kama za JPM haiwezakani kubadili makamissioner watano kwa mda mfupi hivo bila hata annual data report ya kukuongoza
Katika historia ya uongozi wa Tanzania, ni Magufuli pekee ndiye aliyefikia ukusanyaji wa kodi kufikia 15% ya GDP. Ndiye ambaye amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuongeza ukusanyaji wa kodi zaidi ya 110% ndani ya kipindi cha miaka mitano, amefanikia kupunguza urari wa biashara kutoka hasi hadi chanya katika nchi za EAC na SADC, tulikua sisi ni soko la bidhaa za Kanya na South Afrika, leo hiyo hali ni kinyume chake. Amejitahidi sana Magufuli.
 
Umeeleweka na nakuunga mkono kwamba Magufuli kajitabidi lakini bado TRA wangeweza kufika mbali zaidi kama

1. Watatumia tehama zaidi
2. Watawafikia walipa kodi zaidi
3.wataongeza uwazi wa viwango vya kodi
4. Watapunguza manual processes.
5. Wataweka imani zaidi kwenye mifumo ya tehama kiliko kwenye mifumo ya watu watu ( intelligent systems)
Katika historia ya uongozi wa Tanzania, ni Magufuli pekee ndiye aliyefikia ukusanyaji wa kodi kufikia 15% ya GDP. ndiye ambaye amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuongeza ukusanyaji wa kodi zaidi ya 110% ndani ya kipindi cha miaka mitano, amefanikia kupunguza urari wa biashara kutoka hasi hadi chanya katika nchi za EAC na SADC, tulikua sisi ni soko la bidhaa za Kanya na South Afrika, leo hiyo hali ni kinyume chake. Amejitahidi sana Magufuli.
 
Unashindwa kuelewa:

Kenya uzalishaji wao ni zaidi ya mara 3 ya Tanzania.

Obviously kodi lazima iwe mara tatu ya Tanzania.

Tanzania ni li-welfare state,kila kitu serikali eti inatoa bure wakati serikali haina hela hivyo Wananchi hawafanyi kazi seriously maana kila kitu eti serikali inatoa free.

Serikali ndio tatizo,huwezi ongeza uzalishaji kwenye nchi kwa kutoa vitu vya bure,vitu vya bure vina incentivize watu kutofanya kazi maana vitu ni vya bure!

Kitakacho okoa Tanzania ni Capitalism ya kweli.

Kama cure for poverty ni wealth,then lets talk about uzalishaji na sio hii legalized theft inayofanya serikali hovyo ya Tanzania kutoka kwa wazalishaji wachache na kugawa kwa wapumbavu 75% ya wananchi for free.

Asante
Uzalishaji upi ni mara Tafu?

Ninasisitiza tena, ndugu zetu wakenya punguzenu hii tabia ya kupenda kujisifu bila ushahidi wowote, tabia hii ndiyo inayojenga chuki baadae mnalalamika kwa Tanzania ina chuki dhidi ya Kenya.

Tunakuomba uweke ushahidi kuonyesha kwamba Kenya inazalisha mara tatu ya Tanzania, Tafadhali tutajie hizo sectors ambazo Kenya inazalisha mara tatu ya Tanzania.
 
KRA vs TRA (Kwanini Kenya inakusanya kodi mara 3 ya Tanzania)

KRA: Kenya Revenue Authority

TRA: Tanzania Revenue Authority

Makusanyo (Tax Collection July 2019 to June 2020)

KRA-Kenya: 34 Trillion (Tsh)

TRA-Tanzania: 14 Trillion (Tsh)

Sababu ni hizi hapa.
  • Matumizi duni ya teknologia (ICT) kwa TRA
  • Kodi kubwa kwa walipa kodi TRA
  • Kazi nyingi kufanyika kwa mikono (manual processing)- TRA
  • Walipa kodi kukosa elimu ya walipa kodi: TRA
  • Kukosa ubunifu katika kuongeza walipa kodi (Tax base) : TRA
  • Kukosa uwazi kwenye viwango vya kodi kwa walipa kodi - TRA
Matumizi ya teknologia

Mfano mdogo ni ukilinganisha tovuti ya TRA vs KRA.

Tovuti ya TRA ipo duni sana na siyo tovuti ya karne hii bado ni zile tovuti static ambazo taarifa zake hazibadiliki na hazina umuhimu kwa walengwa .

Mfano.

Home page ya TRA vs Home page ya KRA.

Main menu TRA.


Ukifungua tovuti ya TRA kwanza ubnakutana na mambo yafuatayo
View attachment 1571980
Ukweli ni kwamba menu yote ambayo ndiyo memyu kuu haina umuhimu wowote kwa mlipa kodi , hata wanao isimamia hii tovuti sijui wana elimu gani.

Main menu KRA.
Ukifungua tovuti ya KRA unakutana na menu ifuatayo
View attachment 1571981
Hii umekaa kihusika kabisa kwa mlipa kodi wa aina zote , ukifungua hapa individual unakutana na taarfiza zote na kodi kwa watu binafsi, ukifungua business unakutana na taariza zote za kodi kwa makampuni na taasisi, na investors unakutana na taarifa zote za kodi zinazo husu wawekezaji.

Home page TRA vs KRA
Home page ya TRA
.
Utakutana picha zinazo za wanasiasa, ndege za ATCL, picha ya commissioner general ,picha za barabara etc, hivi vyote havina umuhimu wowote na wala havimusaidii mlipa kodi . Ni mambo ya kizamani sana .. nadhani mkuu wa ICT TRA atakua na miaka zaidi ya 50. Picha ya CG inahusika na nini na walipa kodi.. tovuti imejaa taarifa ambazo hazina mashiko.
View attachment 1571983
Home page ya KRA .
Unakutana na maelezo ya jinsi ya kutafuta huduma yoyote ya kodi na kuna sehemu una chagua taarfia na huduma unayo itaka (very friendly )
View attachment 1571984
Hii ni mifano tuu jinsi TRA ilivyo nyuma katika matumizi ya teknologia katika kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Tovuti hii ya KRA inafanya kazi za watu zaidi ya 5000, na uhakika KRA itakua na wafanyakazi wachache kuliko TRA pamoja na kwamba inakusanya kodi mara 3 ya TRA.
View attachment 1571985
Kwa ujumla tovuti ya TRA na KRA zina tofauti zifutazo.
  • KRA ina maelezo karibia yote ya aina za kodi na jinsi ya kulipa Pamoja na maelezo mengine ya kumsaidia mlipa kodi mkubwa na mdogo wakati tovuti ya TRA , taarifa ni chache san ana hazija pangwa kiutaratibu kiasi kwamba tovuti haina msaada .
  • KRA kodi karibia zote unalipa kwa kutumia mitandao au una faili kwa kutumia teknologia na ii unapunguza sana rushwa na kubambikiwa kodi sizizo na maana. Mfano Capital Gain tax ambayo Tanzania Tax pengine inayo ongoza kwa rushwa, Kenya una faili online na baada ya muda unapewa risiti online ya kulipia .
  • KRA imejengwa vizuri na ina taarifa ambazo zinamsadia mlipa kodi, zimehuishwa , tofauti na tovuti ya TRA ambayo imejaza taarifa ambazo hazina maana mfano: number of vistors inamsadia nini mlipa kodi, au link za taasisi za kodi ambazo hazipo Tanzania, utadhani hawana kitu cha kuweka kwenye tovuti sasa wanaamua kukusanya chochote na kujaza huko.
Kwa leo niishie hapa.. nitamalizia next week.

Naamini department ya TRA mtabadirika, au tafuteni namna mkajifunze kwa wenzenu wa KRA.

Tanzania bado inanafasi ya kufikia walau nusu ya makusanyo ya kenya kama itazingatia matumizi ya tehama na kuaachana na matumizi ya binadamu kwa sehemu kubwa, lakini kwa utaratibu huu wa sasa kenya muda si mrefu itakusanya mara 4 ta kenya .
Hata kama data zako zingelikuwa ni sahihi lkn c kwa chai hii[emoji116][emoji116]

34 = 14 × 3?
 
Je population ya Tz ni ngapi?

Walipa kodi ni ngapi?

Kwanini tuna pupulation kubwa lakini GDP ndogo?

Huoni kama mfumo mbovu wa kodi unachangia kwa kiasi fulani ukuaji wa GDP?

Correct me if am wrong..
Kodi inaendana na GDP, Kama GDP ni kubwa, maana yake kodi itakua kubwa, GDP haina uhusiano wa moja kwa moja na Population, ila kuna uhusiano na uzalishaji mali, nchi inaweza kuwa na watu wachache kama Qatar lakini ikawa na Mafuta mengi au Almasi nyingi kama Botswana.

Sasa swali lako la kwanini GDP ndogo lakini population kubwa, hilo ni swali pana ambalo sababu zake ni mtambuka, there is no silver bullet answer". Labda tulifungulie uzi wake maalum.
 
One thing that has made KRA increase revenue collection is the use of KRA PIN numbers in most of Kenyans' lives.

To buy land, vehicles, open a bank account, apply for govt tenders, most private tenders, buy shares in the capital markets, open sacco accounts, apply for HELB loans and many other you need a KRA PIN number, meaning more individuals and businesses need to apply for Pins and file returns.

There is also this document called KRA tax clearance certificate, makes you very compliant on filing taxes.
 
Au kwenye akili kisoda yako unafikiri mapato yote ya serikali ni TRA inakusanya? Yapo mapato mengi tu ya serikali ambayo hayapiti TRA

[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706] Zero brain
Kuna uwezekano Tanzania na Kenya kuna mifumo tofauti ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali, huku Tanzania, TRA haihusiki kukusanya mapato ambayo sio ya kodi, wakati Kenya mapato yote hupitia KRA kama sikosei.

Ila ngoja tusubiri wakenya wenye ufahamu mzuri watuambia juu ya hili, nadhani Mkikuyu akili timamu anaweza kuwa anafahamu vizuri au Tony254, ila hawa wakenya wengine wengi huwa wanaongea kiushabiki zaidi, hawaaminiki Sana.
 
Umeeleweka na nakuunga mkono kwamba Magufuli kajitabidi lakini bado TRA wangeweza kufika mbali zaidi kama

1. Watatumia tehama zaidi
2. Watawafikia walipa kodi zaidi
3.wataongeza uwazi wa viwango vya kodi
4. Watapunguza manual processes.
5. Wataweka imani zaidi kwenye mifumo ya tehama kiliko kwenye mifumo ya watu watu ( intelligent systems)
Hicho ndicho anachohangaika nacho Magufuli, kwa kifupi ni kwamba TRA sio wabunifu ni mpaka washituliwe kama gari bovu, bado hatujapata kamishina mzuri pale TRA ambaye ataleta Mageuzi makubwa kama aliyofanya Kimei CRDB.
 
Uchumi wa Kenya upo juu sana kulinganisha na TZ.. TRA kipewa kazi ya kukusanya kodi Kenya ingeweza kukusanya mara 10 ya hii inayokusanywa na KRA.
 
Tunakuomba sana, punguza hii tabia yako, mbona wenzako wanachangia vizuri bila kushambulia wengine?
MK254 ni mkenya mpumbavu na asiyetaka kubadilika na ndiyo maana akiona Tz inasonga mbele huwa anapotea kabisa kwenye nyuzi cz amekaa kishabiki mno, ss nani asiyejua kwamba kenya kuna madudu mengi kuliko Tz, usikute hata hyo KRA inapika taarifa ionekane inakusanya sn.

Kama wanakusanya sn mbn wananchi bado wana maisha magumu tofauti na Tz? Kama wanakusanya sn mbn GoK inakesha kuomba misaada hata ya ku finance miradi midogo midogo? So lengo la huu uzi ni kuonesha mapungufu yaliyopo TRA japo mtoa uzi ameandika kishabiki zaidi but ukweli ni kwamba TRA inanuka madudu.
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] umenichekesha sana. Eti itakusanya mara 10.

Kenya hakuna issue zile za njoo ofisini tuongee ukifika ofisini tena njoo liquid bar tuongeee.

Huku kenya kila kitu ni digital.[emoji1][emoji1]
Uchumi wa Kenya upo juu sana kulinganisha na TZ.. TRA kipewa kazi ya kukusanya kodi Kenya ingeweza kukusanya mara 10 ya hii inayokusanywa na KRA
 
Kuna vitu vinatia aibu.. mtu unatoka huko unatafuta ulipe kodi haraka unadhani kuna namna rahisi unakutana na menu ambazo hazina hata mashika.


Kuna tatizo kwa wanao ongoza kitengo cha ICT TRA.. inawezekana yupo busy sana kiasi kwamba vitu vidogo kama hivi hajawahi kuwaza kwamba vina impact kubwa sana kwenye kazi za TRA.

TRA inahitaji mabadiriko makubwa kwenye matumizi ya tehama na siku wakilijua hilo watashangaa kazi zao zilivyo rahisi na makusanyo yatakavyo kua kwa haraka japo tunatambua tehama itaua mapato yao binafsi yale ya pembeni..
Tatizo hawataki kuwapa vijana ajira wamejaza wazee wa miaka ya 70 ni tatizo ambalo lipo ofisi nyingi za serikali hata ukienda ttcl wazee wejazana ofisini wakati wanapaswa kuwaachia vijana. Mzee wa miaka 60+ na technology wapi na wapi?
 
Kuna uwezekano Tanzania na Kenya kuna mifumo tofauti ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali, huku Tanzania, TRA haihusiki kukusanya mapato ambayo sio ya kodi, wakati Kenya mapato yote hupitia KRA kama sikosei

Ila ngoja tusubiri wakenya wenye ufahamu mzuri watuambia juu ya hili, nadhani Mkikuyu akili timamu anaweza kuwa anafahamu vizuri au Tony254, ila hawa wakenya wengine wengi huwa wanaongea kiushabiki zaidi, hawaaminiki Sana.
Mkikuyu- Akili timamu ndio mkenya pekee huwa anandika ukweli kuhusu kenya,

Hawa wengine wapo kishabiki mtakesha humu kuanzisha argument zisizo na mbele wala nyuma huku wengine wakiweka siasa zisizo hitajika.
 
Nasikia CIO (Chief Information Officer ) TTCL ni mjeshi mstaafu kama ni kweli..[emoji1]
Tatizo hawataki kuwapa vijana ajira wamejaza wazee wa miaka ya 70 ni tatizo ambalo lipo ofisi nyingi za serikali hata ukienda ttcl wazee wejazana ofisini wakati wanapaswa kuwaachia vijana. Mzee wa miaka 60+ na technology wapi na wapi?
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] umenichekesha sana. Eti itakusanya mara 10.

Kenya hakuna issue zile za njoo ofisini tuongee ukifika ofisini tena njoo liquid bar tuongeee.

Huku kenya kila kitu ni digital..[emoji1][emoji1]
mkuu KE wapigaji sana.
 
Hicho ndicho anachohangaika nacho Magufuli, kwa kifupi ni kwamba TRA sio wabunifu ni mpaka washituliwe kama gari bovu, bado hatujapata kamishina mzuri pale TRA ambaye ataleta Mageuzi makubwa kama aliyofanya Kimei CRDB.

Je, mfumo wetu wa elimu wa kuzingatia tu marks za darasani na aina ya ajira za TRA kulingana na tuhuma zinavyosemwa semwa huku mtandaoni inaweza kuwa ndio sababu ya TRA kukosa ufanisi na ubunifu katika kukusanya mapato?
 
Back
Top Bottom