KRA YAMNASA ABIRIA JKIA NA iPHONE ZA Sh8.2M - KWANI KUNA KOSA?

KRA YAMNASA ABIRIA JKIA NA iPHONE ZA Sh8.2M - KWANI KUNA KOSA?

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Mamlaka ya ukusanyaji wa kodi KRA imenasa iPhone 40 aina ya iPhone 18 Pro na iPhone 18 Pro Max zenye thamani ya takriban Sh8.2 milioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Kilichowafanya maafisa wa forodha kumtilia shaka abiria huyo si mizigo pekee, bali pia ratiba yake ya safari kati ya Nairobi na Dubai.

Kwa mujibu wa KRA, abiria huyo aliingia Kenya mara nne ndani ya siku tisa. Aliingia Septemba 15 na kuondoka Septemba 17; akarudi Septemba 19 na kuondoka siku iliyofuata; akarudi tena Septemba 21 na kuondoka Septemba 22, kabla ya kurejea Kenya Septemba 23.

Katika mahojiano, KRA ilisema abiria huyo alikiri kuwa alikuwa akizisafirisha simu hizo kwa niaba ya mteja aliyeko Dubai.

KRA imeonya wasafiri dhidi ya kubeba bidhaa ambazo hazijatangazwa kwa niaba ya watu wengine bila kujua aina ya bidhaa, umiliki wake na hali yake ya forodha.

Kwa mujibu wa KRA, wasafiri wanaoingia Kenya wanapaswa kutangaza vifaa vya simu wanavyoleta nchini, pamoja na taarifa za IMEI, huku waagizaji wa simu wakitakiwa kuwasilisha taarifa za bidhaa katika mfumo wa forodha.

Lakini swali kubwa hapa ni hili:
Safari nne za Dubai ndani ya siku tisa zilikuwa zikificha nini? Na je, hii ni kesi ya mtu mmoja tu, au imefungua pazia kuhusu namna simu za thamani zinavyoingizwa nchini bila kutangazwa kwa KRA, kama sheria za mamlaka hiyo zinavyosema?
 
Back
Top Bottom