Krismasi za kukumbuka (sad memories)


Hii sasa ndo ilikuwa komesha .
😤😢🤔
 
Alizingua tuu huyo na msosi upo ndani,

Saa hz nimegonga ugali dagaa hapa sina wasiwasi mimi....

Kufatisha sikukuu kama nipo childhood hpn aseeh.....
 
Acha tu mkuu. Yaani kula ugali dagaa sikukuu inaonekana dhambi au mateso fulani
kaka nimetoka kula hapa kwani nimeulizwa? Hapana nimesema mwenyewe

Miaka hii 20+ siwezi kwenda kwa mtu na kuanza kujichekesha mara hivi mara vile, siwezi wana bajeti zao....

Nasubiri jioni ifike nikale chochote ninachomudu basi maisha yaendelee mkuu,

Sipo kwenye nafasi ya kumfurahisha yeyote kisa ni sikukuu au la...
 
Hadi huruma
 
Umekua.Ingekuwa siku zile za utotoni ungemvunja mtu mguu kwa kilio cha kulilia ubwabwa.
 
Christmas ya 2006, niko ugenini kwa jamaa zangu flani,mchana ukapita empty halijarushwa,kufika jioni bado naona kimya na ndio kwanza mke wa jamaa kalala zake chumbani tu,ikabidi nijiongeza nikazama kwa mama ntilie nikajitetea na chapati maharage afu nikakausha,baadae kwenye saa 2 usiku ndo mwenyeji wangu akanichana kuwa wamezinguana na mkewe hivyo mkewe kagoma kupika,nikamwambia haina neno tukazama chimbo na jamaa tukapiga mdudu then tukarudi home kwa jamaa kila mtu akaenda kulala.
 
Kimyakimya halafu kibabe sana😀💪🏿💪🏿💪🏿
 
Alizingua tuu huyo na msosi upo ndani,

Saa hz nimegonga ugali dagaa hapa sina wasiwasi mimi....

Kufatisha sikukuu kama nipo childhood hpn aseeh.....
Ni katika kufurahi tu mkuu, wala sio kama unafanya utoto.

Mimi huwa nafurahi sana sikukuu inikute niko kwetu, home watoto ni wengi, watoto ni chachu/chachandu/kachumbari ya sikukuu yoyote.
Bila watoto sidhani kama sikukuu zitanoga.

Mwaka huu nipo kama Poor Brain tu, sina furaha, naangalua tu videos nazotumiwa toka home wanavyoenjoy, mnyama kachinjwa, nyomi la kuzidi watoto, watu wazima mpaka wazee.
 
Bibi muuza maji akakupa 5000. Mwka 1994.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…