Kalaga Baho Nongwa
JF-Expert Member
- Sep 27, 2020
- 9,953
- 23,150
Na kalaga baho.
Salaam!
Leo wakuu naomba niwasilishe hoja makini ya waandishi wa masuala ha kijamii, Jamrozik. A na Noccela. S. Wakiyazungumza matatizo ya kijamii hasa tatizo la muundo unaotumika kuipanga Jamii (structural arrangement) na kukosekana kwa usawa (social inequality) katika Jamii hii ya watanzania.
Katika maisha yanayotumia muundow a kibepari, yani pyramidal scheme/ survival of the fittest Umaskini unafungaman sawia na kutengwa, taabu zisizoisha na mbebano wa matatizo yasiyoeleweka nini sababu na tiba ni nini. Moja kati ya matatizo hayo, mzizi au kiini ni UMASKINI.
Umasikin unaweza kufutwa na elimu, lkini ukiungalia vizur umaskin huu kuna watu ndo umefika. Pamoja na hawa watu wanapata elimu lakin kuna kazi fulani zinazotoa nafuu ya maisha hawazipat, na kuendelea kuishi vilevile. Familia hizi hazina desturi ya kusapotiana kabisa, kula kwa tabu, kusoma kwa tabu na hata wanaoingia kwenye system kuu hujitenganisha na watu mikoa hiyo. Ni rahisj pia kusikia au kuhisi hisi kuwepo kwa Dalili za uchawi na ushirikina katika ngazi ya familia, ujirani au ukoo.
KUA UYAONE.
Ukizaliwa katika familia hizo hapo, ni lazima uyaone tu.. ndizo hizo ukipata pesa haikai na hujui umeifanyia nn. Ndio hizo utaona kama ndugu hawataki mafanikio yako mana hakuna wa kujitoa kuhusu mapambano yako. Ni mates! Dhiki! Fedheha na masimango kila kukicha. Vijana wengi katika umri wa kuanza kujitegemea wanayaanzaga maisha kwa minded yani mtu akipat hela ya kupanga miez mitatu tu ananunua na mkeka na sufuria mbili anainua maguu
Kalaga baho nakumbuka kipindi nimepata mchongo kuja zanzibar nauli nililipiwa na mwanangu ambayr ni mfayakaz wa Azam marine. Hapo nishalala njaa siku na kutembea kwa miguu siku zisizo na idadi.
Nina hakika vijana wengi sana jamii forum wanaoitia situations kama hizo. Hilo unalopitia ndio maana halisi ya "kua uyaone"
NINI KIFANYIKE?
Pamoja na jitihada mbalimbali zilizopo kupunguza utofauti uliopo katika kuzifikia rasiliamili kwa makundi mbalimbali ya jamii hasa yanayohangaika na mpango wa jamii na kukosekna kwa usawa hasa vijana, wazee, wanawake na watoto. Utekelezaji, usimamiaji na ufatiliajj bado haujafikia hata nusu ya ufanisi unaotarajiwa. Katika pendekzo hili naomba nitete sana vijana.
1. Huzuiwi kuwa na mawazo chanya kwa kile unachofanya. Hata kama unabeti, hakikisha kile unafnya ushakichunguza ndani ya miaka mitatu mbele kitakufikisha mahali pengine/juu zaidi ya hapo ulipo sasa. Hii inajumuisha kusuka mpango mwingne mpya punde utakapoona dalili ya kuanguka punde utakapomaliza chuo/shule
2. Andika, andika, andika Miradi ya kibiashara pelekea wahusika. Miradi kama ile ya Azam pesa, watu baki, uni talent ni idea nzuri za vijana zilizowafikia walengwa
3. Kuwa muumin wa mabadiliko, badili mazingira, jaribu vitu vipya, badili watu wanaokuzunguka kwa kuhama. Huu ni mwanzo mzuri wa mabadiliko kamili
4. Ubunifu na uthubutu.
Uwezekano wa kila mtu kuajiriwa tukiri haupo. Buni, weka wazo meaning na lijaribu. Kila kitu kinawezekana. Jipambanie unavyoweza.. mwanzon kugumu sana mana utaandamwa na aibu, watu wanaokatisha tamaa nk. Wekeza nguvu
Ukizaliwa katika familia za tia maji tia maji mchuzi utoshe! Lazima ukikua utayaona tu!.
Na kalaga baho
Mjini Magharibi
Unguja