Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
Mahusiano ni mchezo wa kutafutana ambapo kwa washiriki wa mchezo huo wengi hawajui nani wanamtafuta ndio maana unakuta hawa leo wanapendana ila kesho wanaaachana kwa sababu kuwa hawaendani sasa swali ni je kama ulijua hamuendani kwnini ulimpa nafasi?
Majibu ni mepesi kuwa wengi tunajua kuwa tulipo sipo baada ya kuwa ndani ya mfumo wa mahusiano ndio unaona huyo sio wako kumbe bali ni wa mwingine na hapo ndipo kuna kuachana au kuvumulia huku ukilalamika ishara kuwa unavumilia tu kwa sababu huna pakwenda.
Kuna watu ambao ni wazito kukubali matokeo na hawa ni wale ambao huwa wanaamini kuwa Dunia nzima wapo wao tu hivyo mkiachana wanaanza kukutamkia laana za kila namna kama vile:
# Sidhani kama utapata tena mwanamke/mwanaume kama mimi.
# Utakuwa maskini wa kutupa na kila mwanamke/mwanaume atakukataa.
# Maisha yako yatakuwa ya hovyo sana huwezi kuniacha mimi na Mungu akupe maisha mazuri.
Hiyo ni mifano tu ila hiwa yanatamkwa mengi sana lakini kwanini yote hayo? Huu ndio mchezo wa mahusiano sio uhakika kumaliza na uliye anza naye.
Taarifa mbaya ni kuwa wengi unaowatamkia hawapati hizo laana tena huwa wanafanikiwa tu vizuri na mahusiano mapya mpaka wanasahau kuwa umewahi kuwa naye kimahusiano katika historia yake.
Ni kweli kuna usaliti mbaya huwa unatokea ila usijisumbue kutamka laana za kila namna bali acha tu uhalisia uje kuongea kama kweli atastahili kulipwa kwa mabaya yake basi atalipwa iwe umetamka ama hukumtamkia.
Mwanasayansi Saul kalivubha
Instagram @fikia ndoto zako