Ndugu;
Sekeseke na ukaidi kidogo na pengine hata kujaribu kugoma kukabidhi nchi kwa mshindi, hilo linatarajiwa bila shaka
Lakini jambo moja la uhakika ni hili; NI LAZIMA ALIYESHINDWA AKABIDHI UONGOZI WA NCHI KWA MSHINDI!
Haijalishi ni njia gani zitatumika lakini, lazima CCM na JIWE wakabidhi nchi kwa mshindi kwa sababu mpaka sasa iko wazi sana, kabisa kuwa CCM na Magufuli a.k.a JIWE hawatashinda kwa mbinu za wizi wao
Hofu ya kushughulikiwa?
Yes, sharti na lazima wawe na hofu. Na kwa upande mwingine sheria ni lazima ichukue mkondo wake
Kwa hili hakuna cha kuoneana haya hata kidogo maana Mungu si binadamu hata aseme uongo ama awe kigeugeu. Alilosema atalitenda, basi atalitenda kweli kweli
Mfano, imeandikwa mahali fulani kwenye biblia takatifu kuwa;
"......KILA ATENDAYE DHAMBI AMEKWISHA KUHUKUMIWA....."
Hii maana yake ni kuwa, kama kuna yeyote aliyetenda dhambi kwa kutumia vibaya madaraka yake, huyo AMEKWISHA KUHUKUMIWA TAYARI na Mungu
Tundu Lissu au CHADEMA hawana hatia yoyote dhidi ya mtu huyu maana matendo yake maovu ndiyo yanayomshuhudia na kumhukumu!!
Hii ni natural principle
Na kamwe hapa hakuna kisasi chochote. Alipaye kisasi ni Mungu mwenyewe. Matendo yao yatafuatana nayo. Salama yao, ni kupatana na matendo yao sasa kabla ya kiama kuwafika!!