Kuachiwa huru kwa Freeman Mbowe na wenzake hakuna sababu nyingine isipokuwa ushahidi wa Jamhuri kutothibitisha mashitaka

ASIKUDANGANYE MTU, kwa propaganda yoyote kuwa DPP kutangaza kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka ya tuhuma za ugaidi na uhujumu uchumi dhidi ya M/Kiti wa CHADEMA - Taifa ndugu Freeman A. Mbowe na wenzake eti ni kwa sababu zingine zozote zile bali ilikuwa ni suala la muda tu siku hii ifike.

ASIKUDANGANYE MTU, kuwa ule ugeni wa wanaoitwa "viongozi wa dini" ikulu na kauli ya Zito Kabwe siku chache zilizopita kule Dodoma wakati wa kilichoitwa "mkutano wa Mutungi - Msajili wa vyama vya siasa kwa mwavuli wa TCD" iliyozua tafrani ya kumwombea msamaha zina influence yoyote kwa maamuzi ya DPP leo kuiondoa kesi hii mahakamani.

Yote na kote huko ilikuwa ni harakati za serikali kutafuta mlango wa kutokea tu ili kuliondoa jambo hilo mahakamani kwa sababu kila mtu aliona kwa macho na kusikia kwa masikio yake kutoka day one kuwa hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha mashitaka hayo.

ASIKUDANGANYE MTU, kuwa kesi hii ilikuwa ni jinai kweli kwa maana ya jinai. Huu ulikuwa mchezo na mkakati wa kisiasa wa CCM kwa mgongo wa SERIKALI dhidi CHADEMA chama kinachotishia uhai na uwepo wa CCM madarakani.

Kilichofanyika ni CHADEMA kukutwa wamejiandaa vyema kukabiliana na mkakati huu mwovu wa CCM na serikali yao.

ASIKUDANGANYE MTU bwana, kwa mchezo huu ambao waasisi ni CCM mwenyewe, CHADEMA ni washindi na wamewachapa goli za kutosha CCM na kwa aibu wakawa wametafuta mbinu ya kuumaliza mchezo apema kuepuka kushindiliwa magoli zaidi.

NARUDIA TENA, ASIKUDANGANYE MTU, kuwa kule kuwaona kina Zitto Kabwe na hawa wanaoitwa "viongozi wa dini" wakiokotezwa na kisha wakatengenezewa mazingira na kukaribishw Ikulu ili wajifanye kumsihi Rais kumsamehe Freeman Mbowe ili hili lililofanyika leo ionekana ni kwa sababu "Rais Samia kawasikia viongozi hao".

USIDANGANYIKE na hayo maigizo. Ni uongo mtupu wa kufuta aibu ya malkia na serikali yake.

ASIKUDANGANYE MTU, wote tunaelewa serikali yoyote ikiwemo hii yetu ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu [CCM] huwa madarakani kwa mlango wa siasa na hu - mantain uwepo wake madarakani kwa mbinu za kisiasa zozote zile iwe halali ama haramu.

Katika hili la kesi ya Freeman A. Mbowe ilikuwa mbinu haramu na pengine ya kijinga na kipumbavu sana ya serikali hii chini ya CCM kujaribu kuji - maintain lakini bahati wameshindwa spectacularly.

Kwa kuwa ilikuwa mbinu haramu matokeo yake hata mikakati [strategies] zao zikawa za kijinga na kipumbavu kabisa.

Mathalani, kitendo cha Rais Samia kwenda kufyatuka uongo wa mchana kweupe akihojiwa na kituo cha TV cha BBC Swahili kuwa baadhi ya wahalifu wenzake na Freeman Mbowe walishahukumiwa na kufungwa gerezani ilikuwa uthibitisho wa kwanza wa wanamikakati (strategists) wa CCM kushindwa kabla ya mkakati kufikia hata robo tu.

CHADEMA hongereni. You are the winners. I see the light at the end of the tunnel. Keep on going. Harakati za kudai katiba bora na mpya, demokrasia na haki ziendelee.
sasa mlikuwa mnalialia nini kumuombea aachiwe wakati mnajuwa atashinda kwanini msingemuacha mpaka amalize na kwanini DPP alipoleta kusudio la kumuachia kwanini msimwambie jaji kuwa hamkubali mnataka iende mpaka mwisho ili ijulikane maana mpaka sasa mbowe anajulikana kuwa ni gaidi maana alishakutwa na kesi ya kujibu
 
Mama kamwita mbowe ikulu kumuomba msamaha kiutu uzima,
Naona yale mahafidhina yamenuna
 
CHADEMA hongereni. You are the winners. I see the light at the end of the tunnel. Keep on going. Harakati za kudai katiba bora na mpya, demokrasia na haki ziendelee...[emoji1534]
Mbowe hawezi kudai Katiba mpya tena, tayari toka Jana alivyotoka Sero ameshakua Mwana Ikulu ya Samia!!
 
sasa mlikuwa mnalialia nini kumuombea aachiwe wakati mnajuwa atashinda kwanini msingemuacha mpaka amalize na kwanini DPP alipoleta kusudio la kumuachia kwanini msimwambie jaji kuwa hamkubali mnataka iende mpaka mwisho ili ijulikane maana mpaka sasa mbowe anajulikana kuwa ni gaidi maana alishakutwa na kesi ya kujibu
Muda ni mali dogo
 
ila linapokuja suala la kuchukua dola mnabaki mnashangaa kama mjusi aliyebanwa na mlango vile
Punguza hasira Dogo, kunywa maji mengi, hata zenji CUF hushinda lakini wahafidhina hugangania
 
ASIKUDANYE MTU. Hii ni Kama Kuruka Mkojo halafu Kukanyaga 'Mavi'...ashakum.
Zito Alimuomba Mama Amsamehe Mbowe.

Watu Tukaja juu huku tukimlaumu Zito kwanini Kamuombea Msamaha Mbowe. Ajabu Sasa Ombi Lile lile limetolewa Na Viongozi Wa Dini.

Sasa 'Eti' tunashangilia Kabisa huko 'Haya au Soni' Usoni Zimetutoka. Very Funny!
Watu wanajitoa ufahamu kirahisi mno, au labda wanataka kujidanganya kinachotokea hawakioni. Mahakama Kuu imesema baada ya kuusikiliza ushahidi wa serikali kuwa washtakiwa wana kesi ya kujibu. Sasa ushahidi dhaifu uko wapi hapo? Watu wote waliomwona rais Samia Suluhu walimwomba aifute kesi, kwa kawaida wangemwomba aiamuru serikali imalize ushahidi mapema ili haki itendeke mapema. Lakini wanamwomba aifute kesi. Kweli shehe mkuu ananyenyekea kwa rais kuMWOMBA na wala sio kushauri Mbowe na wenzake wafutiwe mashtaka ulitarajia nini rais mwislamu tena mwanamke asisikilize ombi la shehe wake mkuu? Ninajiuliza ingekuwa DPP angeifuta kesi kabla mahakama haijatamka kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa washtakiwa wana kesi ya kujibu hao wanajivua ufahamu wangeimba nyimbo zipi huku kwenye social media.
 
Mbowe hawezi kudai Katiba mpya tena, tayari toka Jana alivyotoka Sero ameshakua Mwana Ikulu ya Samia!!

Now ni zamu yenu mdai katiba mpya mfungwe na nyie sio kila kitu afanye yy Tu
 
Tanzania hatuna Wapinzani ambao wako serious na Mabadiliko,njaa tu ndiyo inawasumbua, ndiyo maana wakiitwa Ikulu wakipewa Mkate na chai ya Maziwa basi wanasahau shida za Wananchi kabisa!!
 
Pia hatuna wanainchi ambao wanaweza kwenda front wao kazi ambayo wanajua ni kukaa jamii forums na kupiga kelele Tu,

Mkitwaaa kwenda front wote mnakimbia

Sehem pekee ambako mnaweza kufanya kitu ni jf basi
 
ASIKUDANYE MTU. Hii ni Kama Kuruka Mkojo halafu Kukanyaga 'Mavi'...ashakum.
Zito Alimuomba Mama Amsamehe Mbowe.

Watu Tukaja juu huku tukimlaumu Zito kwanini Kamuombea Msamaha Mbowe. Ajabu Sasa Ombi Lile lile limetolewa Na Viongozi Wa Dini.

Sasa 'Eti' tunashangilia Kabisa huko 'Haya au Soni' Usoni Zimetutoka. Very Funny!
Usiwe Mjinga,au umesahau kuwa mtoto wa Mbowe alizungumza na akasema Baba Yao hajaomba msamaha na Wala hahitaji kuombewa msamaha kwani anaamini mwomba msamaha ni mkosaji na yeye atapigania haki yake mahakamani!
Hata hao viongozi wa dini hawakutumwa na Mbowe!Mbowe alikuwa kajiandaa kujitetea,siku imefika magereza wakadanganya kuwa Mbowe anaumwa!Baadaye DPP akafuta kesi!Hebu angalia hiyo timeline ya viongozi wa dini,halafu angalia wanafanya hivyo siku Moja kabla ya Mbowe kuanza kujitetea!
DPP kamuachia Mbowe bila masharti yeyote,hivyo Mbowe hajaomba msamaha!
 
ni msamaha wa Rais Samia usidanganywe
Rais hatowi msamaha Kwa watuhumiwa,hakuna sheria hiyo!
DPP kaona hawezi kushinda kesi,pia kina Kibatala walimtia hofu baada ya kuficha identity za mashahidi wao!Maana walikuwa na mashahidi zaidi ya 20 na wengine ni watumishi!
Tumia akili,yaani wamesubiri mpaka siku Mwamba ndio anaanza kujitetea ndio wanafuta kesi!
 
Hata Kama Rais hatowi msamaha,lakini kumbuka kua DPP huyo huyo aliye msamehee Mbowe ni Mteule wa Rais, ndiyo maana ukaona watu wote waliokuwa wanamuwombea msamahaa Mbowe hawakwenda kwa DPP,bali walikwenda kwa Rais, na Rais alichofanya ni kutoa Memo tu kwa Mteule wake,na Mteule wake nae akamaliza game Mahakamani! Na ndiyo maana Mbowe kutoka kwake anamshukuru sana Mama, wala sijamsikia akiwashukulu Mawakili wake!! Jiongeze ndg, haya mambo ya siasa za Africa ni Magumu mno!!
 
Mbowe amewaahukuru watu wote na akasema Kwa wakati huo anaomba asiongee chochote!Ndipo akaitwa Ikulu!Halafu amemshukuru Rais Kwa kukutana naye na Wala sio kumuachia!
Wakati Zitto anamuombea msamaha Kwa Rais,Mbowe kupitia mtoto wake alisema hahitaji msamaha kwani anaamini hana hatia!
Ukipewa msamaha na DPP basi unaambatana na masharti ya kuachiwa!Mfano kabendera alivyoomba msamaha na kupewa masharti ya msamaha!Mbowe kaachiwa bila masharti yeyote!Hata kama Samia alioenyeza memo Kwa DPP basi si kwasababu Mbowe alimpigia magoti Samia!
Mbowe tayari alikuwa amejiandaa na mawakili wake kujitetea!
Jiulize,kwanini wamesubiri mpaka siku Mwamba anaanza kujitetea ndio wafute kesi?
Tukiona Mbowe ameacha kabisa suala la Katiba mpya,basi hapo tutajua kasalimu amri!
 
Hutomsikia tena anaongea Jambo la katiba mpya
 
ASIKUDANYE MTU. Hii ni Kama Kuruka Mkojo halafu Kukanyaga 'Mavi'...ashakum.
Zito Alimuomba Mama Amsamehe Mbowe.

Watu Tukaja juu huku tukimlaumu Zito kwanini Kamuombea Msamaha Mbowe. Ajabu Sasa Ombi Lile lile limetolewa Na Viongozi Wa Dini.

Sasa 'Eti' tunashangilia Kabisa huko 'Haya au Soni' Usoni Zimetutoka. Very Funny!

Nani alishangalia viongozi wa dini kumuombea Mbowe msamaha, acha upotoshaji wa kijinga. Tulisema kabisa Mbowe hana kosa lolote la kuombewa msamaha. Na kama ni kuachiwa sio kwa sababu ya maombi ya viongozi wa dini maana hawakutumwa na cdm bali wao waliamua kivyao baada ya kuona ushahidi wa kihanithi wa serikali huko mahakamani, ama kwa kupangwa na serikali. Mtu anayeijua haki yake hawezi kuiomba Boss, wala kutuma mtu yoyote akamuombee msamaha. Sasa hivi tunaangalia kwanini Mbowe ameenda ikulu haraka hivyo, na tunataka kuona mwelekeo wake baada ya kukutana na rais, akilegeza msimamo tu ajue hatuko naye tena.
 
Back
Top Bottom