Kuachiwa Ndege Canada: Lissu, Fatma Karume na Membe muombeni radhi Profesa Kabudi

Kuachiwa Ndege Canada: Lissu, Fatma Karume na Membe muombeni radhi Profesa Kabudi

Leteni hati ya hukumu na cost za kesi acheni polojo.

Hati za hukumu za south africa na za canada ziko wapi? kwanini iwe siri?

Mkulima kalipa garama za kesi? za kulala hotel za nyota 5 ujumbe wa kabudi South Na Canada!

Watanzania sio wajinga kiivyo.
Mnatanua goli, pole kwa maumivu unayopitia.Ile hukumu ya SA mliiona?
 
Pesa imelipwa ila kwa sababu serikali hii inaficha sana mambo watajifanya wameichukua kiubabe! haa wapi! uzuri ukweli ni kama mimba utauificha mwanzoni lakini watu wataanza kuona unatema mate na kula limao. Mzungu atatwambia tu. Lakini ninachojiuliza kwa nini serikali hii inaogopa ukweli na uwazi.
 
hao watu watatu kwakweli nafikiri hata ikija mvua ya kuua watanzania wote watasema bora ije kuliko kuiombea nchi mema yaani ni wanafiki haijawahi tokea ni walafi wa madaraka tu utafikiri wakipewa mdaraka kuna kitu cha maana sana watakachokifanya tuwajue tuwaogope kama ukimwi hawafai nchi hii hasa lissu abaki hukohuko aliko
 
  • Thanks
Reactions: Oii
emalau,
hivi huyo mzungu tangu ameanza kushindwa hizo kesi alishagawaambia nyie kama ameshindwa au amelipwa? kaeni hivyo tu kupiga kelele mitandaoni ccm hoyeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Kamanda, hata SA mlisema hivyo hivyo, tumewazoea kwa kujifariji
Ma'mdogo, Kika kitu kinachofanyika nje ya Gamba la dunia kiakuwa documented! Fanya hivi; weka nakala za hukumu za mahakama za SA na Canada hapa nizisome! Ni hivyo tu utakuwa umeshinda but kinyume chake hayo ni matokeo ya matumizi ya marejesho kutoka mashirika na makampuni ya umma! Hongereni kwa ubunifu wa kuchangisha!
 
Lakini zilikua nyingi hivyo? Basi wengine waweza kuanza kusafiri ili kumufuata atoe mgao mapema!!!
Wanasheria wake makini akina Kimaro &co watazisunda za kutosha natumaini maghorofa yataibuka kama uyoga huko Kilimanjaro haswa maeneo ya milimani
 
Ndugu zangu,

Takribani majuma mawili yaliyopita Waziri wa Mambo ya nje Prof.Palamaganda Kabudi aliutaarifu Umma kutokea Dodoma siku ambayo Rais Magufuli alikuwa na kazi ya kikatiba kuwaapisha mabalozi wetu.

Prof.Kabudi alimuelezea rais huku akieleza jinsi ambavyo wananchi wa Tanzania watauchukua ushindi dhidi ya kaburu Stein kwa mara nyingine baada ya ''kumcharaza'' katika mahakama ya Gauteng kule bondeni (Afrika ya kusini).

Aliyekuwa wa kwanza kubeza ni Ndugu Membe huku akiaminisha umma kuwa Prof.Kabudi hatafanikiwa, akishauri kuwa njia pekee ni kumuita mkulima Stein kwenye meza na ''kumlipa chake. Ajizi nyumba ya njaa naye Tundu Lissu na Fatuma Karume wakauvagaa mkenge huku akiwa hawana uzoefu wowote na mashauri katika korti ya kimataifa, walijaribu kuwaapooza wafuasi wao ambao walikuwa wenye hasira nyingi baada ya kushauriwa vibaya kujitoa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Bila kuchelewa, wafuasi wa CHADEMA na wanasiasa hao wakaivagaa mitandao huku wakionesha dharau kwa Prof.Kabudi na Watanzania, wakisema Mkulima Stein ni ''kiboko'' wakiowanukuu Lissu,Fatuma na Membe.

Wanasheria wetu wazalendo walinyamaza kimya huku wakiandaa hoja za kumshinda ''Mkulima Stein'' kortini. Kwa hoja zilizotolewa kortini hatimaye siku mbili zilizopita Mahakama ya Canada iliipa Tanzania ushindi kwa mara nyingine tena huku ikiweka ''precedence'' kwa siku zijazo.

Nimalize tu kwa kusema, Hongereni wananchi wazalendo wa Tanzania, Mmeshinda tena!
Huyu ndiye mkuu. Weka Hukumu hapa! Vinginevyo tutakudharau!
 
Wanasheria wake makini akina Kimaro &co watazisunda za kutosha natumaini maghorofa yataibuka kama uyoga huko Kilimanjaro haswa maeneo ya milimani
mnaota ndoto za mchana
hana hoja ya kufanya alipwe huyo
 
Pesa imelipwa ila kwa sababu serikali hii inaficha sana mambo watajifanya wameichukua kiubabe! haa wapi! uzuri ukweli ni kama mimba utauificha mwanzoni lakini watu wataanza kuona unatema mate na kula limao. Mzungu atatwambia tu. Lakini ninachojiuliza kwa nini serikali hii inaogopa ukweli na uwazi.
Tunaharaka ya nini, tunasubiri taarifa ya mapato na matumizi ya Serikali tutaziona tu hela zetu kutoka kwa CAG na Zitto 😂 😂
 
Back
Top Bottom