Kuagiza chakula online Hapa Dar

Kuagiza chakula online Hapa Dar

Kuna wajasiriamali Wengi Sana siku online wanatangaza kupika vyakula mbali mbali na kutangaza unaweza agiza chakula online ...kinakufikia...

Nna watu wengi waliowahi agiza vyakula kutoka restaurants mbalimbali wanakutana na changamoto nyingi Sana...
Kwanza ..kinachotangazwa na kinachofika kunakuwa na tofauti Sana ya quality na quantity...
Watu wengi wanaona Bora kwenda sehemu husika ule uondoke....

Nimeona ni share hili labda kuna wenye experience tofauti....
Inaonekana wabongo Wengi uaminifu wa huduma Bora ni mpaka mteja amuone amekuja...kuliko online...
Wengine uzoefu wenu ikoje?
Umewahi agiza chochote...iwe Biriani au chochote ukajutia?
Huwa unaagiza wapi? Mimi huwa natumia duka direct au piki na ninachokipata ni kile nikichoagiza. Ila siwezi kusema sana maana mostly huwa naagiza orchid, patio,chinese dragon,epi'dor na kfc dependa na mood ya siku, kuna baadhi ya restaurants ukiagiza unaenjoy vinalingana na gharama na kile unachotegemea kukipata
 
Aisee bongo uaminifu ni zero kabisa niliwahi kuagiza mbuzi mahali kiasi nilicholetewa hakiendani kabisa na nilichoagiza alafu nilikua na wageni, sema mwenye kiki namjua nikampigia simu nikagoma kabisa kulipa wala kutumia kile chakula, ikabidi jamaa awashe gari aje, kuja kufika alishangaa sana maana anadai alinifungia chakula mwenyewe, kumbe boda alifungua chakula sijui ndo alikula portion kadhaa za mbuzi au alipeleka kwake😀😀😀, jamaa nusu amuue
Mkuu lakini sisi wote tumelelewa kwenye maadili ya dini mbili nzuri ya kikristo na kiislamu inakuwaje hatuwi waaminifu???
 
Bongo unaeza agiza Biriani online ukaisubiri mpaka ifike tayari njaa imepoa au ushajilia vitu vingine ushashiba zako.. Yani Kuna muda unasubiri msosi hadi unaamua upige simu ucancel order na huo ndo muda wanaokwambia boda ameshatoka yuko road msubiri anafika saivi tu ila mpaka afike sasa….. Doooh 🙌🙌🙌
 
Umeandika nini mkuu?

Hapa jamaa anataka kufahamu kama watu wengine wanaonunua/agiza chakula kupitia apps au page za hao wafanyabiashara ya chakula nao wanapitia changamoto alizozitaja.

Wewe unaanza kulaumu single mother?

Hiyo mbona haina mantiki? Umelewa?
Nimejumuisha single mother coz walio wengi hawana malezi mazuri kwa watoto wao na kukosa malezi bora ndo kumepelekea watu kukosa uwaminifu na tabia za hovyo ktk jamii kipi nimekosea apo ?
 
Huwa unaagiza wapi? Mimi huwa natumia duka direct au piki na ninachokipata ni kile nikichoagiza. Ila siwezi kusema sana maana mostly huwa naagiza orchid, patio,chinese dragon,epi'dor na kfc dependa na mood ya siku, kuna baadhi ya restaurants ukiagiza unaenjoy vinalingana na gharama na kile unachotegemea kukipata
Location pia ...unakaa wapi? Kwa Dar wanaokaa upanga,posta kinondoni Wana nafuu...
Ukikaa Kimara, Kigamboni na kongowe hizo restaurants zina deliver?
 
Location pia ...unakaa wapi? Kwa Dar wanaokaa upanga,posta kinondoni Wana nafuu...
Ukikaa Kimara, Kigamboni na kongowe hizo restaurants zina deliver?
Huwa naagiza nikiwa ofisini, nikiwa nyumbani napendelea kupika kama ni cha nje huwa nakifata huko huko unless nikitaka kuwaagizia watoto KFC au marry brown huwa wanafanya delivery.
 
Tumia QUICKDROP hii inatumika ukiwa maeneo ya post ,Upanga ina search restaurants zilizopo karibu na ww
 
Bodaboda akisikia harufu la biriyani anaamua kupaki aanze kula.
Uamunifu Bado ni kitu adimu sana hapa
 
Back
Top Bottom