Premij canoon
JF-Expert Member
- May 27, 2018
- 1,203
- 2,771
Habari wakuu. Bila shaka nyote ni wazima na mishe mishe zinaendelea kama kawaida. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu uagizaji wa magari.
Internet imerahisisha sana shughuli za binadamu, leo hii mtu unaweza kuagiza chochote kupitia mtandao tu. Kumekuwa wimbi kubwa la madalali wanaojihusisha na biashara ya uagizaji magari na wameweka utaratibu wa kulipa kwa awamu na wao wanatumia mtandao huo huo ambao yeyote anaweza kuutumia na ukaagiza gari yako (wameona fursa na wanaitumia vizuri, pongezi kwao)
Shida au changamoto ambayo inatukwamisha wengi ikiwemo na mimi ni zile hesabu za TRA kama ushuru na tozo za bandari ambazo kwa fununu kadhaa nilizopata ni kuwa tozo zote za gari husika zimewekwa mwenye site ya TRA, ambapo yeyote anaweza kukamilisha na akaitoa gari yake bila kupitia mtu wa katikati.
Naomba kwa yeyote mwenye ufahamu juu ya haya basi atupe ABC's za kufanya ili kukamilisha zoezi lote kuanzia kuagiza hadi ushuru na kulitoa gari lako bandarini ili wengi ambao hatufahamu nasi tuweze kufahamu. Nafahamu JF ni jukwaa kubwa lenye wataalamu wa fani za kila aina na natumaini watajitokeza watu wenye uzoefu wa hili. Natanguliza shukraan.
Nawasilisha.