Kuagiza mabasi ya mwendokasi ya dizeli baada ya kukamilika kwa Bwawa la Nyerere itakuwa ni kipimo cha ujinga kwa Watanzania

Yeye anajisemea mwenyewe , uhalisia ni kwamba 99% hawana majiko ya umeme, na nikaongezea, hata kwa walionayo, bado umeme ni ghali kuliko gesi. Na nikaeleza utofauti uliopo kwenye Mabasi ambayo ni mradi wa serikali na bwawa ni la serikali, hivyo wanaweza kuweka bei maalum ya umeme kwa ajili ya mabasi kumpa nafuu msafiri, kuliko kufungulia maji yamwagike bure
Sasa tuongelee majiko niliyoyanukuu au manasi na mabwawa ambayo mimi sijakataa.
 
Sababu zipo wazi,
1.) watu tayari wameshatumia pesa nyingi kununua mitungi na majiko ya gesi, hivyo hakuna mwenye pesa ya mchezo kununua tena majiko ya umeme.

2.) Umeme bado ni ghali ukilinganisha na gesi.

- Ila kwa mradi wa mwendokasi ni tofauti, mabasi ndio tunanunua sasa hivi , hivyo tuna nafasi ya kuchagua aina ya mabasi tunayohitaji.

- Mradi ni wa serikali na bwawa la umeme ni la serikali, na kwakuwa kwa sasa umeme ni mwingi kuliko mahitaji, serikali inaweza kupeleka umeme wa special tarrif kwa mabus ya umeme ili kuleta unafuu kwa wananchi kuliko kufungulia mabwawa kama walivyofanya rufiji na kuacha umeme upoteee bure na kuleta mafuriko..
Ongezea pia umeme ni bei rahisi kuliko diesel.
Kwa mchajo mmoja wa lisaa unaweza kupata km 400,500 na kuendelea, umeme hapo sidhani kama umemaliza wa elfu 10, tufanye wa 20 kabisa, sasa elfu 20 inakupa kilometa 500, je kilometa hizo kwa diesel si ni mafuta ya laki na ushehe huko.
 
Hapo umefafanua vizuri.., itashangaza sana kama tutaacha umeme wa Rufiji umwagikie chini na kuleta mafuriko..
 
Na uzuri magari ya kuchaji hayana makorokoro mengi. Hayana vitu vingi vya kutengeneza kama haya ya Mafuta.. Ni mepesi kungundua tatizo la gari liloharibika.

Tena ndugu zetu Uganda wanayazalisha hata sio mbali ..

Sema Wanajua vifaa vya mabasi ya umeme sio vingi hivyo zile hela wanazipata kwa kuagiza kitu flani kwa milioni 50 wakati ni milion 3 watakosa
 
Utaahira upo wa aina nyingi, pia upo utaahira binafsi na utaahira jumuishi (Communal insanity).

Sifahamu bado kama mabasi yaliyoagizwa kwa ajili ya kutumika kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka wa Mbagala kwamba ni ya Diesel au ya umeme (Rechargeable); ila kama kweli tutakuwa tumeagiza mabasi ya kutumia mafuta ya diesel yanayo tugharimu pesa nyingi za kigeni kuyaagiza, yanayosababisha gharama za usafirishaji kuwa kubwa na kuchafua maazingira, ilihali mitambo mingi ya kufua umeme imezimwa kwa sababu ya umeme kuzidi mahitaji, na hii ni baada ya mtambo mmoja tu kati ya 9 ya bwawa la Nyerere kuwashwa, basi itakuwa ni kipimo cha kutosha cha utaahira jumuishi cha waTanganyika.

Ni hayo tu.

Kutokuwa ya umeme wala siyo shida, kwa sababu itahitaji maandalizi mapya ya hayo magari ya kutumia umeme na labda itachukua muda kulingana na mahitaji ya usafiri.

Lakini, jambo linalonishangaza ni hali ya serikali na mashirika yake pamoja na Watanzania kutobadili magari yao kuwa ya mfumo wa gesi asilia yenye ufanuu zaidi kuliko hata umeme.

Kwenda na kurudi kwa safari ya Dar - Moro kwa kutumia kati ya shilingi 35,000 hadi 40,000 inashangaza mno kuona bado yuko Mtanzania ambaye gari lake halitumii mfumo wa gesi.

Hata makusanyo ya siku moja ya taksi inayotumia gesi ni zaidi ya daladala kadhaa. Hivyo, kabla hatujaiwazia serikali tujiulize na raia kwanini gari zetu hazijawekwa mfumo wa gesi?

Ova
 
Ukitaka kujua km serikali ya Tz inaongozwa na viongozi wajinga angalia barabara za mwendokasi za Mwenge - Tegeta na K'koo - Mbagala,, tyr tuna umeme wa kutosha,,why hawakuwaza kujenga reli tuwe na SGR ya Town Trip km ilivyo Dubai na Metro or Abu Dhami walivyo na Emirates? Ukiifatilia serikali yetu utaumia kichwa na kutoboa moyo wako
 
Ni mdogo?, sasa kwanini ulipowashwa mtambo mmoja tu kati ya 9 ilibidi wazime mitambo mingine sababu uzalishaji umezidi? Pia kwakuwa kuna watu hawana umeme basi ndio tuache kununua mabasi ya umeme? Kwamba haya mabasi yanazuia nini hao wasio na umeme kupewa umeme?
Kwa nini wengine wapate anasa ya mabasi ya umeme wakati wenzao wanatumia vibatari?
 
Sababu zipo wazi,
1.) watu tayari wameshatumia pesa nyingi kununua mitungi na majiko ya gesi, hivyo hakuna mwenye pesa ya mchezo kununua tena majiko ya umeme.
Watu wana majiko ya umeme ambayo walikuwa wanayatumia na sasa hivi yamebakia kuwa kama mapambo na unavyosema kwamba watu wameshanunua majiko ya gesi na mitungi ni sawasawa na kusema sababu watu wameshapata ukimwi waendeleze ngono.....
2.) Umeme bado ni ghali ukilinganisha na gesi.
Ni ghali sababu inabidi uwe ghali au ni ghali sababu ya walamba asali ? Na je ukiingiza dollar tunazotumia kuagiaza hio LPG huoni kwamba in the long run Gesi ni gharama..., na je vipi katika efficiency ya kupika keki (oven) kuchemsha maji (jug kettle) kuwarm chakula (microwave) food processing, blender n.k. je umeme bado ni ghali (sababu hapo naongelea ufanisi)
- Ila kwa mradi wa mwendokasi ni tofauti, mabasi ndio tunanunua sasa hivi , hivyo tuna nafasi ya kuchagua aina ya mabasi tunayohitaji.
Hakuna aliyesema tutumie diesel tunaweza kutumia hata CNG yaani kutofanya kule au kufanya huku haimaanishi tusifanye hapa
- Mradi ni wa serikali na bwawa la umeme ni la serikali, na kwakuwa kwa sasa umeme ni mwingi kuliko mahitaji, serikali inaweza kupeleka umeme wa special tarrif kwa mabus ya umeme ili kuleta unafuu kwa wananchi kuliko kufungulia mabwawa kama walivyofanya rufiji na kuacha umeme upoteee bure na kuleta mafuriko..
Hata Tanesco ni ya Serikali na Serikali ni ya wenye nchi ambao ni wananchi kwahio inapaswa wala sio ombi kuhakikisha gharama ya nishati ni nafuu..., na ni upuuzi kutumia pesa za misaada na kodi kupigia chapuo wasambazaji wa gesi ya watu wa ughaibuni...
 
Kutokuwa ya umeme wala siyo shida, kwa sababu itahitaji maandalizi mapya ya hayo magari ya kutumia umeme na labda itachukua muda kulingana na mahitaji ya usafiri.

Lakini, jambo linalonishangaza ni hali ya serikali na mashirika yake pamoja na Watanzania kutobadili magari yao kuwa ya mfumo wa gesi asilia yenye ufanuu zaidi kuliko hata umeme.

Kwenda na kurudi kwa safari ya Dar - Moro kwa kutumia kati ya shilingi 35,000 hadi 40,000 inashangaza mno kuona bado yuko Mtanzania ambaye gari lake halitumii mfumo wa gesi.

Hata makusanyo ya siku moja ya taksi inayotumia gesi ni zaidi ya daladala kadhaa. Hivyo, kabla hatujaiwazia serikali tujiulize na raia kwanini gari zetu hazijawekwa mfumo wa gesi?

Ova
Serikali inafanya kila iwezalo kuzuia matumizi ya gesi sababu waliopo seriakalino wananufaika na uagizaji mafuta. Omba kuanzisha vitu vya kubadili mitungi ya hesi kwenye magari uone balaa lake
 
Ukitaka kujua km serikali ya Tz inaongozwa na viongozi wajinga angalia barabara za mwendokasi za Mwenge - Tegeta na K'koo - Mbagala,, tyr tuna umeme wa kutosha,,why hawakuwaza kujenga reli tuwe na SGR ya Town Trip km ilivyo Dubai na Metro or Abu Dhami walivyo na Emirates? Ukiifatilia serikali yetu utaumia kichwa na kutoboa moyo wako
Hata hizi njia za sasa zinaweza kuwekewa overhead powelines kwa baadae ili tusitumie mabasi ya kucharge, hivyo hakijaharibika kitu..
 
Kenya hapo wana bodaboda za umeme na daladala za umeme, ni sisj tu tumezembea.

Hizo boda boda huchukua battery kwa station za Total kwa Kes 120 ambapo anatembea nayo 90km
Ambapo mafuta hapo ni 4lts kwa Tsh 800
 
Nimejaribu na kuona kuwa mapishi kwa umeme ni bei rahisi kuliko mkaa na gesi, tatizo umeme hautabiriki
 
Serikali inafanya kila iwezalo kuzuia matumizi ya gesi sababu waliopo seriakalino wananufaika na uagizaji mafuta. Omba kuanzisha vitu vya kubadili mitungi ya hesi kwenye magari uone balaa lake

Ni kweli, lakini ni gari ngapi binafsi zina mfumo huo? Na sisi wananchi shida yetu iko wapi? Labda kama taifa tuna tatizo la kuishi kimazoea?

Kwamba serikali na taasisi zake na raia tumeshazoea hali hivyo ilivyo na tunaogopa kubadilisha? Kwanini sisi raia hatuchangamkii hii nafuu?

Mtu kutoa 2mil. kwa pamoja kufunga mfumo wa gesi ni mtihani mzito..
 
kabisa, mie nilishauri wakati ndo tunaanza kujenga brt za mkapa tukashauri zitandikwe njia za umeme kama zile za sgr ili bus hizo zitumie umeme, pili tulishauri zijengwe reli mjini maarufu kama trum hizi treni zingesafiri sambamba na mabus, lakini ndo kwanza yakaagizwa ma irus hata hayaeleweki bodi youtong engene cummin break wabco, tukasema yakizeeka hawatajua spea wapate wapi, ikumbukwe tuliambiwa tenda ya kusupply mabasi ilipewa kampuni ya MAN ya ujerumani, sasa huko kwa mchina hatujui tulifikaje
 
Watu wana majiko ya umeme ambayo walikuwa wanayatumia na sasa hivi yamebakia kuwa kama mapambo na unavyosema kwamba watu wameshanunua majiko ya gesi na mitungi ni sawasawa na kusema sababu watu wameshapata ukimwi waendeleze ngono.....

Ni ghali sababu inabidi uwe ghali au ni ghali sababu ya walamba asali ? Na je ukiingiza dollar tunazotumia kuagiaza hio LPG huoni kwamba in the long run Gesi ni gharama..., na je vipi katika efficiency ya kupika keki (oven) kuchemsha maji (jug kettle) kuwarm chakula (microwave) food processing, blender n.k. je umeme bado ni ghali (sababu hapo naongelea ufanisi)

Hakuna aliyesema tutumie diesel tunaweza kutumia hata CNG yaani kutofanya kule au kufanya huku haimaanishi tusifanye hapa

Hata Tanesco ni ya Serikali na Serikali ni ya wenye nchi ambao ni wananchi kwahio inapaswa wala sio ombi kuhakikisha gharama ya nishati ni nafuu..., na ni upuuzi kutumia pesa za misaada na kodi kupigia chapuo wasambazaji wa gesi ya watu wa ughaibuni...
Turahisishe mazungumzo. Gesi na Umeme vyote ni mbadala mzuri wa diesel, ila napendekkea zaidi umeme sababu utumikaji wake kwenye vyombo vya usafiri ni rahisi zaidi, ndio maana SGR imefungwa motor za umeme, pia kwa sasa umeme tunao wa kutosha na wa bei nafuu.
 
Mtu kutoa 2mil. kwa pamoja kufunga mfumo wa gesi ni mtihani mzito..
Unajua watu wanatoa shilingi ngapi kufunga sound za akina Dick Sound? Au wanatoa shilingi ngapi kwa garage za Wachina ili kuunda mwonekano wa mbele wa gari zao ili ziwe kama toleo la sasa?

Kuna tabia tU za mazoea, gharama huwa kisingizio tu.

Sasa sio wote wanatumia pesa nyingi kwenye hizo anasa
 
Back
Top Bottom