Kuagiza Toothpick za meno toka China, hivi inamaana alieturoga amekufa au?

Kuagiza Toothpick za meno toka China, hivi inamaana alieturoga amekufa au?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Nimeshtuka sana leo baada ya kuona toothpick nilizonunua kwa mangi eti zime-andikwa made in China..!! sasa magari tunaagiza.., mafuta tunaagiza.., hata gesi ambayo tunayo tunaagiza.., sasa ndio hadi vijiti vya kuchokonolea meno tu tuagize....???!!!!!, jamani jamani..., hivi alieturoga amefariki kwani..???!
 
ccm is cannibal tribe
an animal that feeds on the fresh of its own special.Watatula watatumaliza
 
Hautakiwi kulalamika ndugu! tumia fulsa kwa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza hizo toothstick uondokana na umaskini.Kuna vitu vingi hapa bongo hatuna kama mtaji unao kanunua machine china uje kututengenezea tena kwa bei rahisi upige pesa.
 
Umesahau kuna kuku wanatoka Brazil na USA
 
Kuna matunda mengi tu nimewahi kununua mall yanatoka S.A.
 
Hautakiwi kulalamika ndugu! tumia fulsa kwa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza hizo toothstick uondokana na umaskini.Kuna vitu vingi hapa bongo hatuna kama mtaji unao kanunua machine china uje kututengenezea tena kwa bei rahisi upige pesa.

Haya ndo majibu mepesi ambayo yanapatikana kwa wingi pale mjengoni.. Kama kuna viwanda vya hapa nyumbani vinauliwa kwa kuwa bidhaa wanazozizalisha zinakosa soko kwa vile kuna bidhaa toka nje ambazo zinaingizwa na kuuzwa bila ya kulipiwa kodi kwa bei rahisi zaidi unategemea utengeneze kiwanda cha kutengeneza hizo toothpick zipambane na hizo za china..? Leo kiwanda cha kutengeneza kibiriti cha Kibo match kinatembelea dripu kwa kuwa kwenye soko kuna vibiriti vingi toka nje na ambavyo havikulipiwa kodi..!
 
minaona bora hizo toothpicks zitoke china ili tusiharibu miti yetu ! maana kuni tu zinateketeza misitu sembuse hizo toothpicks tena hazina umuhimu kivile !
 
hata samaki tunaagiza japani na south afrika .angali tuna bahari kubwa tu tanga to mtwara na maziwa makubwa yote afrika tunayo na mito isiyohesabika.
 
Jameni toothpick zinatengenzwa kutokana na bamboo siyo miti

Mie naomba kuuliza kwa mwenye kufahami policy ya Tz kwenye cortage industry ikoje, maana bibadhaa nyingi toka China inatoka kwenye hizi cortage industry
 
Kwani ulizokuwa watumia zamani ni za nchi gani
 
mbona kuna kiwanda cha toothpick hapa bongo! btw, hata us kuna viwembe imported, ina maana wao wanashindwa kutengeneza viwembe vya kunyolea ndevu? hayo ndiyo mambo ya soko huria! hizi nazo ni fursa, kiwanda kidogo cha kutengeza toothpicks ni around milioni kumi, fursa hizo!
 
tutunge sera ambazo hazituumizi sisi wenyewe,imagine wawekezaji wakubwa wapewa msamaha wa kodi kwa miaka kadhaa ila wewe ukifungua kaduka unalipa kodi ya mwaka hata hujaanza.

serikali itafute vyanzo vingine vya mapato badala ya hali ya sasa ya kutegemea kodi,misaada n.k.mfano serikali ya Australia wana kipindi cha kwenye tv kinaitwa border security,wakikiuza kwenye tv station ni mapato mazuri tu.

kodi ni nyingi mno matokeo yake ni ukisema uzalishe vitu utauza bei ya juu mno ili kupata faida.

mashine zilitakiwa ziwe na misamaha ya kodi ili kuencourage uzalishaji.

viwanda vya majumbani vingesimamiwa vizuri na project managers chini ya udhamini wa serikali ili kusaidia wenye elimu waitumie kuwasaidia wenye nia ya maendeleo ila hawana profession zinazotakiwa.

tuwe pia tunashare vitu vidogodogo vya kujitengenezea mwenyewe kwa matumizi ya nyumbani katika muda wa ziada,sio lazima kila kitu ununue.mfano wazungu wao wanapeana maarifa mitandaoni eg you tube,pinterest n.k
 
minaona bora hizo toothpicks zitoke china ili tusiharibu miti yetu ! maana kuni tu zinateketeza misitu sembuse hizo toothpicks tena hazina umuhimu kivile !

Ndugu yangu ..... asilimia kubwa ya toothpick zinatengenezwa kwa kutumia bamboo (mianzi) na bamboo is one of the plants ambazo ni environmental friendly material .... Bamboo huota na kutoa watoto maoteo kama migomba hivyo haiharibu mazingira, ..... mikoa ya iringa na mbeya ina potential kubwa ya kuwa na viwanda vya toothpicks, chopsticks, ice cream sticks, spatulas etc
 
Jameni toothpick zinatengenzwa kutokana na bamboo siyo miti

Mie naomba kuuliza kwa mwenye kufahami policy ya Tz kwenye cortage industry ikoje, maana bibadhaa nyingi toka China inatoka kwenye hizi cortage industry
Duhh kweli kizungu kizunguzungu.
Bamboo si Mwanzi,sasa mwanzi sio mti?
 
Nimeshtuka sana leo baada ya kuona toothpick nilizonunua kwa mangi eti zime-andikwa made in China..!! sasa magari tunaagiza.., mafuta tunaagiza.., hata gesi ambayo tunayo tunaagiza.., sasa ndio hadi vijiti vya kuchokonolea meno tu tuagize....???!!!!!, jamani jamani..., hivi alieturoga amefariki kwani..???!

Kibo Match Group imefingwa kwa kushindwa kumudu ushindani
 
Back
Top Bottom