Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kamati ya Utendaji ya Yanga, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said, imefanya kikao cha dharura kujadili sintofahamu ya kuahirishwa kwa mechi yao dhidi ya Simba iliyopaswa kuchezwa tarehe 8 Machi 2025.
Katika taarifa yao, Yanga imetoa pole kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza kushuhudia mchezo huo na kueleza kuwa walifuata taratibu zote za maandalizi. Klabu hiyo imeeleza kuwa Simba ilishindwa kufuata utaratibu wa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa, jambo lililopelekea mgogoro uliosababisha wao kugomea mechi.
Kutokana na hali hiyo, Yanga imedai kupewa ushindi kwa mujibu wa kanuni, ikakataa kushiriki mechi hiyo kwa tarehe yoyote mpya itakayopangwa, na kutangaza kukosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu chini ya Steven Mnguto.
Klabu hiyo imeiomba TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wapya.
Soma: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
==
TAARIFA KWA UMMA
MACHI 09, 2025
Kamati ya Utendaji ya YANGA, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said imefanya Kikao cha dharura leo tarehe 9 Machi 2025 kwa njia ya mtandao kujadiliana na kukubaliana mambo yafuatayo;
Kwanza, Uongozi wa YANGA unatoa pole kwa Wanachama, Mashabiki, Wapenzi na wadau wamchezo wa mpira wa miguu waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na kushindwa kushuhudia mechi yetu dhidi ya Klabu ya Simba iliyokuwa ifanyike jana tarehe 8 Machi 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Klabu ya YANGA ilifanya maandalizi yote ya mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni ikiwemo kushiriki kwenye kikao cha maandalizi ya mechi [MCM] kilichofanyika tarehe 7 Machi 2025, saa 8 mchana kwenye Hoteli ya Spice, Jijini Dar es Salaam.
Kwenye kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Klabu ya YANGA na Simba, wasimamizi wa mchezo ikiwemo Mratibu wa mchezo, Afisa Usalama wa mchezo, Mtathimini Waamuzi, Kamishna wa mchezo na watendaji wa Bodi ya Ligi, Klabu ya Simba haikutoa taarifa ya kutaka kuutumia uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mchezo husika kwa ajili ya kufanya mazoezi kama kanuni inavyoruhusu.
Katika hali ya kushangaza, Usiku wa tarehe 7 Machi, 2025, Klabu ya Simba iliwasili katika uwanja wa Mkapa ikiwa na magari kadhaa, kwa ajili ya kufanya mazoezi huku wakifahamu hawakuwa wamefuata taratibu za kupata haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye taarifa ya Bodi ya Ligi, ikiwemo kuleta ombi hilo kwenye MCM, kuwasiliana na Msimamizi wa mchezo, Meneja wa Uwanja wala timu mwenyeji ambayo ni YANGA.
Mamlaka ya Uwanja ilikataa kuwaruhusu kuingia ndani ya Uwanja kwa sababu hakuku- wa na taarifa wala maandalizi yoyote yaliyofanywa kwa ajili yao, na baada ya kuwepo kwa sintofahamu hiyo, Klabu ya Simba iliamua kuondoka uwanjani hapo.
Usiku wa kuamkia siku ya mchezo, tarehe 8, Machi 2025, Klabu ya Simba ilitoa tamko rasmi la kugomea mchezo huo kwa kigezo cha kutopata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi, huku wakielewa dhahiri kwamba hawakuwa wamefata taratibu.
Huku kukiwa na taharuki kwa wapenzi wengi wa soka kuhusu uwepo wa mchezo huo baada ya tamko hilo la Klabu ya Simba, asubuhi ya tarehe 8 Machi 2025 Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Steven Mnguto alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa wasiwasi na kuwahakikisha mashabiki waende uwanjani kwa sababu ratiba ya mchezo huu namba 184, iko palepale hakuna kilichobadilika.
Lakini licha ya tamko hilo la Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, mchana wa siku hiyo hiyo, tarehe 8 Machi 2025, Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu ambayo Mwenyekiti wake ni Steven Mnguto ilitoa taarifa ya kuahirisha mechi namba 184, kinyume na taratibu na Kanuni zinazoendesha Ligi Kuu.
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, ufuatao ndio msimamo wa Kamati ya Utendaji wa YANGA;
1: Klabu ya YANGA kupewa haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi.
2: Kamati ya Utendaji ya YANGA imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa.
3. Kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya YANGA imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo tunaliomba Shirikisho la Mpira wa miguu - TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.
Mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga kote duniani kuendelea kuwa watulivu wakati Uongozi ukiendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na harakati za kudai haki yetu zikiendelea.
Imetolewa na Kamati Ya Utendaji
Young Africans Sports Club
09.03.2025