Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Umenikumbusha ishu ya Fei, Hahaha. Mpira raha sana.Huu msimamo wa Yanga ila Kolo FC wamejaa kibao, kila timu iendelea na ilicho kiamua. Nyie mmechagua mgomo, sisi tumechagua kendelea na ligi .
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umenikumbusha ishu ya Fei, Hahaha. Mpira raha sana.Huu msimamo wa Yanga ila Kolo FC wamejaa kibao, kila timu iendelea na ilicho kiamua. Nyie mmechagua mgomo, sisi tumechagua kendelea na ligi .
Nimejiuliza pia Yaan kuna kipande wameruka,wameelezea Simba walikuja na magari kadhaa, ehee baada ya kuja mlifanyaje nyie Au mliogopa mabasi mawili 😂😂Makomandoo uchwara ndo waliozuia Simba wasiingie Uwanjani, mbona utopolo hawajaandika hapo kuhusu hao migambo uchwara
View: https://www.instagram.com/reel/DG-B8NUsBKg/?igsh=eXJ1cjhycWx0MmQ0
Ndipo mtajua nani najitoa ufahamu.
Kuna sehemu nimesema huyu ni mtoa maamuzi au amewazungumzia wenye mpira wao Afrika CAF wanavyo fanya inapotokea situation kama ya jana na kaongea kwa vipengele.Ngoja kwanza, huyu ndo atatoa maamuzi kwamba mechi itarudiwa au la?
Mh unasifia ujinga,hiyo barua mmeuandikia UMMA sio Bodi ya ya ligi kudai Point 3Nice
Eti huyu nae ni Mhandisi daah kweli elimu ya Bongo ni jau,Kamati ya Utendaji ya Yanga, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said, imefanya kikao cha dharura kujadili sintofahamu ya kuahirishwa kwa mechi yao dhidi ya Simba iliyopaswa kuchezwa tarehe 8 Machi 2025.
View attachment 3265070
Katika taarifa yao, Yanga imetoa pole kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza kushuhudia mchezo huo na kueleza kuwa walifuata taratibu zote za maandalizi. Klabu hiyo imeeleza kuwa Simba ilishindwa kufuata utaratibu wa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa, jambo lililopelekea mgogoro uliosababisha wao kugomea mechi.
View attachment 3265071
Kutokana na hali hiyo, Yanga imedai kupewa ushindi kwa mujibu wa kanuni, ikakataa kushiriki mechi hiyo kwa tarehe yoyote mpya itakayopangwa, na kutangaza kukosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu chini ya Steven Mnguto.
View attachment 3265065
Klabu hiyo imeiomba TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wapya.
Soma: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
==
TAARIFA KWA UMMA
MACHI 09, 2025
Kamati ya Utendaji ya YANGA, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said imefanya Kikao cha dharura leo tarehe 9 Machi 2025 kwa njia ya mtandao kujadiliana na kukubaliana mambo yafuatayo;
Kwanza, Uongozi wa YANGA unatoa pole kwa Wanachama, Mashabiki, Wapenzi na wadau wamchezo wa mpira wa miguu waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na kushindwa kushuhudia mechi yetu dhidi ya Klabu ya Simba iliyokuwa ifanyike jana tarehe 8 Machi 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Klabu ya YANGA ilifanya maandalizi yote ya mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni ikiwemo kushiriki kwenye kikao cha maandalizi ya mechi [MCM] kilichofanyika tarehe 7 Machi 2025, saa 8 mchana kwenye Hoteli ya Spice, Jijini Dar es Salaam.
Kwenye kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Klabu ya YANGA na Simba, wasimamizi wa mchezo ikiwemo Mratibu wa mchezo, Afisa Usalama wa mchezo, Mtathimini Waamuzi, Kamishna wa mchezo na watendaji wa Bodi ya Ligi, Klabu ya Simba haikutoa taarifa ya kutaka kuutumia uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mchezo husika kwa ajili ya kufanya mazoezi kama kanuni inavyoruhusu.
Katika hali ya kushangaza, Usiku wa tarehe 7 Machi, 2025, Klabu ya Simba iliwasili katika uwanja wa Mkapa ikiwa na magari kadhaa, kwa ajili ya kufanya mazoezi huku wakifahamu hawakuwa wamefuata taratibu za kupata haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye taarifa ya Bodi ya Ligi, ikiwemo kuleta ombi hilo kwenye MCM, kuwasiliana na Msimamizi wa mchezo, Meneja wa Uwanja wala timu mwenyeji ambayo ni YANGA.
Mamlaka ya Uwanja ilikataa kuwaruhusu kuingia ndani ya Uwanja kwa sababu hakuku- wa na taarifa wala maandalizi yoyote yaliyofanywa kwa ajili yao, na baada ya kuwepo kwa sintofahamu hiyo, Klabu ya Simba iliamua kuondoka uwanjani hapo.
Usiku wa kuamkia siku ya mchezo, tarehe 8, Machi 2025, Klabu ya Simba ilitoa tamko rasmi la kugomea mchezo huo kwa kigezo cha kutopata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi, huku wakielewa dhahiri kwamba hawakuwa wamefata taratibu.
Huku kukiwa na taharuki kwa wapenzi wengi wa soka kuhusu uwepo wa mchezo huo baada ya tamko hilo la Klabu ya Simba, asubuhi ya tarehe 8 Machi 2025 Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Steven Mnguto alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa wasiwasi na kuwahakikisha mashabiki waende uwanjani kwa sababu ratiba ya mchezo huu namba 184, iko palepale hakuna kilichobadilika.
Lakini licha ya tamko hilo la Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, mchana wa siku hiyo hiyo, tarehe 8 Machi 2025, Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu ambayo Mwenyekiti wake ni Steven Mnguto ilitoa taarifa ya kuahirisha mechi namba 184, kinyume na taratibu na Kanuni zinazoendesha Ligi Kuu.
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, ufuatao ndio msimamo wa Kamati ya Utendaji wa YANGA;
1: Klabu ya YANGA kupewa haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi.
2: Kamati ya Utendaji ya YANGA imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa.
3. Kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya YANGA imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo tunaliomba Shirikisho la Mpira wa miguu - TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.
Mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga kote duniani kuendelea kuwa watulivu wakati Uongozi ukiendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na harakati za kudai haki yetu zikiendelea.
Imetolewa na Kamati Ya Utendaji
Young Africans Sports Club
09.03.2025
View attachment 3265044View attachment 3265046
Sasa hapa kwenye hii ishu CAF haipo mkuu. Labda mkashtaki. Ila mtani huko nje nako una makesi kibao, mengine umeangukia pua.Kuna sehemu nimesema huyu ni mtoa maamuzi au amewazungumzia wenye mpira wao Afrika CAF wanavyo fanya inapotokea situation kama ya jana na kaongea kwa vipengele.
Umesikiliza video CAF wanavyo fanya wenye mpira wao? Endeleeni kudeka na TFF yenu.Sasa unamquote huyo ndiyo mtapeleka maandiko yake kwenye vyombo vya usuluhishi?
Umenikumbusha ishu ya Fei, Hahaha. Mpira raha sana.
Sababu TFF mnawamudu, hamna kanuni inayosema timu isuse baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi.Sasa hapa kwenye hii ishu CAF haipo mkuu.
Mh unasifia ujinga,hiyo barua mmeuandikia UMMA sio Bodi ya ya ligi kudai Point 3
Huyu jamaa ndio anayewapoteza maboya pale Gongowazi.Yaan Kikao mmekaa mmefanya mtandaoni? Mnadai point 3 mkiwa kila mtu yupo kwake😂😂 point 3 na magoli matatu mkitumia zoom meeting Au WebEx?
Haya hii barua mbovu hivi isiyo na mashiko bila shaka ameamdika kamwe?
Mbona hamjaelezea walinzi wenu kuwazuia Simba kuingia uwanjani?
We unaamini uamuzi wowote wa bodi ya ligi ni sawa? Unaamini hakuna chombo,taratibu,miongozo,kanuni zinazoiongoza bodi ya ligi! Yani hata bodi ya ligi ikisema bingwa wa nbc ni kengold utaona ni sawa kisa ni bold ya ligi imesemaSasa point tatu zitatolewa kwa vigezo gani na mechi ilihairishwa? TFF kupitia bodi ya ligi si ilifuta hii mechi?
Hawajasoma hata vigezo vya kutoa point tatu iwapo timu itasusa mchezo?
Halafu hawajasoma kuwa mechi ilihairishwa kwa mamlaka ya kifungu kipi?