Yanga yatoa msimamo mkali: Yadai pointi 3 kwa Simba, yakataa mechi ya marudio na kutaka Kamati ya Ligi Kuvunjwa!

Yanga yatoa msimamo mkali: Yadai pointi 3 kwa Simba, yakataa mechi ya marudio na kutaka Kamati ya Ligi Kuvunjwa!

Umeona wapi timu inasusia mechi baada ya kutofanya mazoezi siku moja kabla ya mechi. Au kun kanuni yoyote inayosema kama umezuiwa kufanya mazoezi ruksa kususa.

View: https://www.instagram.com/reel/DG-B8NUsBKg/?igsh=eXJ1cjhycWx0MmQ0
CAF huko Uarabuni kila msimu timu zinafanyiwa figisu mpaka wanazuiwa kutumia uwanja,ila mechi inapigwa maamuzi yanakuja kutolewa baada ya CAF kupokea ripoti ya mechi.

Kama kitu hujui ni bora ukanyamaza

Kumbuka uhuni waliofanyiwa Rs Berkane walipoenda Algeria
Kumbuka uhuni waliofanyiwa Nigeria na viongozi wa Libya

Huu mpira msidhani mnauangalia pekee yenu tu mnaweza kutuambia chochote tukawasikiliza tu
 
Ingeanza kuvunjwa TifuTifu kwanza naona Yanga wamepepesa macho nashangaa hadi leo Kasongo anaenda kwenye ofisi kama katibu wa kamati na Mwenyekiti wake wakati watu wenyewe wanafanya mambo kihuni tu.
 
Kama kitu hujui ni bora ukanyamaza

Kumbuka uhuni waliofanyiwa Rs Berkane walipoenda Algeria
Kumbuka uhuni waliofanyiwa Nigeria na viongozi wa Libya

Huu mpira msidhani mnauangalia pekee yenu tu mnaweza kutuambia chochote tukawasikiliza tu
Sasa hivyo vipengele alivyo zungumza vipo au havipo? Ina maana CAF waliviweka kama urembo?
 
Sababu TFF mnawamudu maana hamna kanuni inayosema timu isuse baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi.
Hakukuwa na mechi, ilifutwa na TFF. Simba haiwezi cheza mechi imefutwa na TFF.

Tafsiri ya kususa ni kutokuingiza timu uwanjani, pamoja ya kwamba Simba ilisema haichezi ila misimamo huwa inabadilika kutegemeana na mazingira, ushawishi na mambo mengine, sasa TFF wakafuta.

Lazima mkumbike ya Fei sababu mnachotegemea hapa ni HEKIMA NA BUSARA.
Kanuni mzee baba, Kanuni. HEKIMA NA BUSARA zinafata.
 
Si mnaongea kwa kanuni, mwaduke anaongea kwa kanuni,unasema atakuwa shahidi nyie mnavyo ongea kwa kanuni mnampango wa kuwa mashahidi?

Haya tuzungumze kanuni kaka
Ulileta Team uwanjani ✅
Refa aliekua uwanjani ni nani?
Kamisaa wa mchezo?
Je Team ilikaguliwa na filimbi kumaliza mchezo ilipulizwa?
Hivi kama vilifanyika vyote point 3 haki yako.

Nijibu mzee
 
Kuna sehemu nimesema huyu ni mtoa maamuzi au amewazungumzia wenye mpira wao Afrika CAF wanavyo fanya inapotokea situation kama ya jana na kaongea kwa vipengele.
Msibishane mechi itapigwa tena mbele ya SSH baada ya Simba kukutana na Al masry
 
We unaamini uamuzi wowote wa bodi ya ligi ni sawa? Unaamini hakuna chombo,taratibu,miongozo,kanuni zinazoiongoza bodi ya ligi! Yani hata bodi ya ligi ikisema bingwa wa nbc ni kengold utaona ni sawa kisa ni bold ya ligi imesema
Bodi ya ligi ipo kisheria sio kiimani. Imani yangu juu ya maamuzi ya bodi haina maana kwenye ligi, ishu ni maamuzi yaliyotolewa yanaruhusiwa kisheria?
 
Si mnaongea kwa kanuni, mwaduke anaongea kwa kanuni,unasema atakuwa shahidi nyie mnavyo ongea kwa kanuni mnampango wa kuwa mashahidi?
Unatupostia maandiko ya mtu mwingine, tena mchambuzi tu bila maelezo yoyote unategemea tukuelewe vipi? Sasa Mbwaduke na wewe mna tofauti gani mbele ya vyombo vya usuluhishi?
 
Hakukuwa na mechi, ilifutwa na TFF. Simba haiwezi cheza mechi imefutwa na TFF.

Tafsiri ya kususa ni kutokuingiza timu uwanjani, pamoja ya kwamba Simba ilisema haichezi ila misimamo huwa inabadilika kutegemeana na mazingira, ushawishi na mambo mengine, sasa TFF wakafuta.

Kanuni mzee baba, Kanuni. HEKIMA NA BUSARA zinafata.
Kikanuni hutoboi, sema TFF mnaimudu.Kila timu iendelee na msimamo wako,wewe goma kama alivyo sema Magoli.Yanga itaendelea na mechi zake zilizobaki.
 
Haya tuzungumze kanuni kaka
Ulileta Team uwanjani ✅
Refa aliekua uwanjani ni nani?
Kamisaa wa mchezo?
Je Team ilikaguliwa na filimbi kumaliza mchezo ilipulizwa?
Hivi kama vilifanyika vyote point 3 haki yako.

Nijibu mzee
Kwani wewe kuna kanuni inayo zuia kususia mechi baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi?
 
Kikanuni hutoboi,
Embu tupe mfano halisi wa huu ubaya ubwela uliofanyika hapa umevunja kanuni ipi?
sema TFF mnaimudu.Kila timu iendelee na msimamo wako,wewe goma kama alivyo sema Magoli.Yanga itaendelea na mechi zake zilizobaki.
TFF ina nguvu kiaheria kuhairisha mechi na kuipanga siku nyingine. Kanuni joseph, kanuni na kaakili kidogo.
 
Sasa hivyo vipengele alivyo zungumza vipo au havipo? Ina maana CAF waliviweka kama urembo?
Rs Berkane alienda kucheza final bila kucheza nusu final kwa upumbavu huo huo unaotaka kufanana na wa uto fc
Nigeria wamepewa ushindi bila hata kucheza mechi na Libya kwa ujinga ujinga

Labda kama mnasema Cuf ya buguruni kwa profesa Lipumba
 
Unatupostia maandiko ya mtu mwingine, tena mchambuzi tu bila maelezo yoyote unategemea tukuelewe vipi? Sasa Mbwaduke na wewe mna tofauti gani mbele ya vyombo vya usuluhishi?
Vipi kiziwi wewe?

Mwaduke yale sio maandiko yake binafsi ni maandiko yaliopo kwenye kanuni za CAF.
 
Back
Top Bottom