Yanga yatoa msimamo mkali: Yadai pointi 3 kwa Simba, yakataa mechi ya marudio na kutaka Kamati ya Ligi Kuvunjwa!

Yanga yatoa msimamo mkali: Yadai pointi 3 kwa Simba, yakataa mechi ya marudio na kutaka Kamati ya Ligi Kuvunjwa!

Kwa nini sasa usipost kutoka chanzo asili cha CAF badala yake unapost maneno ya mchambuzi? Ndiyo maana nakuuliza huyo Mbwaduke ndiyo atakuwa shahidi wenu namba moja? Bando langu halafu unanipostia viclip visivyo na maelezo unategemea nini?
Yale sio maneno ya mchambuzi, bali alicho ongea ni maandishi ya CAF yy kafanya reference? Au hujui maana ya kurefer...... maana kama hujui maana ya kurefer nitakuona mtu wa ajabu ukizungumzia kanuni,maana huwezi kuzungumzia kanuni bila kufanya reference ndicho alichofanya Mwaduke.

Nimekuuliza wewe Kiziwi? Maana inawezekana nimempigia Mbuzi Gitaa.
 
Kwa hiyo ile barua haikuandikwa na nyie au Magoli aliongea kuchamsha baraza la kahawa?Hivi unasoma ulicho kiandika, kwa hiyo ile barua haikuandikwa na nyie........
Mambo mepesi huelewi, nimekuambia hivi, Simba kuandika barua kuwa haitocheza haitoshi kuipa Yanga p3 kuwa imesusa mechi, ile ni barua, Tafsiri ya kususa ni kutopeleka timu uwanjani. Mbona huwa huelewi boss? Hahaha
 
Kutokucheza na kususia tofauti yake nini?

Ndio maana nimekuambia hata unacho kiandika wewe mwenyewe hukielewi.
 
Yanga ilivunja kanuni ipi inayosema ikivunjwa basi match ighairishwe?
Yanga hakuvunja kanuni inayosema mattch iahirishwe.Hili nakubali,sasa naimba nijibu na mimi swali hili,

Je nani alithibitisha kuwa Yanga ulifika uwanjani?
Kamisaa wa mchezo aliandika report ipi?

Nani alikua Refa akaheshabu dakika na kumaliza mchezo kama kanuni inavuotakiwa ili upate point 3?
 
Yale sio maneno ya mchambuzi, bali alicho ongea ni maandishi ya CAF yy kafanya reference? Au hujui maana ya kurefer...... maana kama hujui maana ya kurefer nitakuona mtu wa ajabu ukizungumzia kanuni,maana huwezi kuzungumzia kanuni bila kufanya reference ndicho alichofanya Mwaduke.

Nimekuuliza wewe Kiziwi? Maana inawezekana nimempigia Mbuzi Gitaa.
Ngoja nikufundishe kama hakuna mtu aliwahi kukufundisha hili. Ukiwa unatoa reference, hauendi kwa source nyingine iliyotumia reference hiyo na kuinukuhu bali unatakiwa uende kwenye source yenyewe halisi ya hiyo reference. Hivyo ndiyo reference zinafanyika.

Ulichofanya hapa in maana reference yako ni Mbwaduke na siyo CAF.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kutokucheza na kususia tofauti yake nini?
Kutokuingiza timu uwanjani ndo kususa. Sasa TFF waliifuta hiyo mechi kabla ya muda wa kuingia uwanjani. Huwezi susa mechi isiyokuwepo. Tumeelewana boss?

Yaani mpaka hapa, hoja si Simba kususa mechi, ni TFF kufuta mechi.
 
Kamati ya Utendaji ya Yanga, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said, imefanya kikao cha dharura kujadili sintofahamu ya kuahirishwa kwa mechi yao dhidi ya Simba iliyopaswa kuchezwa tarehe 8 Machi 2025.

Katika taarifa yao, Yanga imetoa pole kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza kushuhudia mchezo huo na kueleza kuwa walifuata taratibu zote za maandalizi. Klabu hiyo imeeleza kuwa Simba ilishindwa kufuata utaratibu wa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa, jambo lililopelekea mgogoro uliosababisha wao kugomea mechi.

Kutokana na hali hiyo, Yanga imedai kupewa ushindi kwa mujibu wa kanuni, ikakataa kushiriki mechi hiyo kwa tarehe yoyote mpya itakayopangwa, na kutangaza kukosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu chini ya Steven Mnguto.

Klabu hiyo imeiomba TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wapya.

Soma: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

==

TAARIFA KWA UMMA
MACHI 09, 2025

Kamati ya Utendaji ya YANGA, chini ya Rais Mhandisi Hersi Said imefanya Kikao cha dharura leo tarehe 9 Machi 2025 kwa njia ya mtandao kujadiliana na kukubaliana mambo yafuatayo;

Kwanza, Uongozi wa YANGA unatoa pole kwa Wanachama, Mashabiki, Wapenzi na wadau wamchezo wa mpira wa miguu waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na kushindwa kushuhudia mechi yetu dhidi ya Klabu ya Simba iliyokuwa ifanyike jana tarehe 8 Machi 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Klabu ya YANGA ilifanya maandalizi yote ya mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni ikiwemo kushiriki kwenye kikao cha maandalizi ya mechi [MCM] kilichofanyika tarehe 7 Machi 2025, saa 8 mchana kwenye Hoteli ya Spice, Jijini Dar es Salaam.

Kwenye kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Klabu ya YANGA na Simba, wasimamizi wa mchezo ikiwemo Mratibu wa mchezo, Afisa Usalama wa mchezo, Mtathimini Waamuzi, Kamishna wa mchezo na watendaji wa Bodi ya Ligi, Klabu ya Simba haikutoa taarifa ya kutaka kuutumia uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mchezo husika kwa ajili ya kufanya mazoezi kama kanuni inavyoruhusu.

Katika hali ya kushangaza, Usiku wa tarehe 7 Machi, 2025, Klabu ya Simba iliwasili katika uwanja wa Mkapa ikiwa na magari kadhaa, kwa ajili ya kufanya mazoezi huku wakifahamu hawakuwa wamefuata taratibu za kupata haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye taarifa ya Bodi ya Ligi, ikiwemo kuleta ombi hilo kwenye MCM, kuwasiliana na Msimamizi wa mchezo, Meneja wa Uwanja wala timu mwenyeji ambayo ni YANGA.

Mamlaka ya Uwanja ilikataa kuwaruhusu kuingia ndani ya Uwanja kwa sababu hakuku- wa na taarifa wala maandalizi yoyote yaliyofanywa kwa ajili yao, na baada ya kuwepo kwa sintofahamu hiyo, Klabu ya Simba iliamua kuondoka uwanjani hapo.

Usiku wa kuamkia siku ya mchezo, tarehe 8, Machi 2025, Klabu ya Simba ilitoa tamko rasmi la kugomea mchezo huo kwa kigezo cha kutopata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi, huku wakielewa dhahiri kwamba hawakuwa wamefata taratibu.

Huku kukiwa na taharuki kwa wapenzi wengi wa soka kuhusu uwepo wa mchezo huo baada ya tamko hilo la Klabu ya Simba, asubuhi ya tarehe 8 Machi 2025 Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Steven Mnguto alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa wasiwasi na kuwahakikisha mashabiki waende uwanjani kwa sababu ratiba ya mchezo huu namba 184, iko palepale hakuna kilichobadilika.

Lakini licha ya tamko hilo la Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, mchana wa siku hiyo hiyo, tarehe 8 Machi 2025, Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu ambayo Mwenyekiti wake ni Steven Mnguto ilitoa taarifa ya kuahirisha mechi namba 184, kinyume na taratibu na Kanuni zinazoendesha Ligi Kuu.

Kutokana na maelezo hayo hapo juu, ufuatao ndio msimamo wa Kamati ya Utendaji wa YANGA;

1: Klabu ya YANGA kupewa haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi.

2: Kamati ya Utendaji ya YANGA imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa.

3. Kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya YANGA imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo tunaliomba Shirikisho la Mpira wa miguu - TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.

Mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga kote duniani kuendelea kuwa watulivu wakati Uongozi ukiendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na harakati za kudai haki yetu zikiendelea.

Imetolewa na Kamati Ya Utendaji
Young Africans Sports Club
09.03.2025

Naomba hayo maneno ya msimamo mkali ya futwe,
 
Kifupi bodi ya ligi hawakutumia busara kuahirisha mchezo wao wangetulia hadi mwisho watoe adhabu kwa aliyeonekana kuvunja sheria

Mimi niungane na utopolo kwamba bodi ya ligi inaviongozi wasiofaa waachie ngazi
 
Ngoja nikufundishe kama hakuna mtu aliwahi kukufundisha hili. Ukiwa unatoa reference, hauendi kwa source nyingine iliyotumia reference hiyo na kuinukuhu bali unatakiwa uende kwenye source yenyewe halisi ya hiyo reference. Hivyo ndiyo reference zinafanyika.

Ulichofanya hapa in maana reference yako ni Mbwaduke na siyo CAF.
Mhhh kwani Mwaduke si amefanya reference kutoka CAF?

Mwaduke=Amerefer CAF.
The Nilicho kileta=Reference from Mwaduke.
Hence.
Nilicho kileta=Reference from CAF .

Algebra ya kawaida tu tena O-Level sio ya Advance.
 
Yanga hakuvunja kanuni inayosema mattch iahirishwe.Hili nakubali,sasa naimba nijibu na mimi swali hili,

Je nani alithibitisha kuwa Yanga ulifika uwanjani?
Kamisaa wa mchezo aliandika report ipi?

Nani alikua Refa akaheshabu dakika na kumaliza mchezo kama kanuni inavuotakiwa ili upate point 3?
Hilo swala la bodi ya ligi kwanini awakuwepo uwanjani siku ya mchezo namba husika,Yanga wao walifika,na wana vielelezo vya pre match meeting siku 1 nyuma kabla ya match,so bodi ya ligi wao ndio watakuja na kipengele cha kuahirisha kupitia kanuni za vyama soka
 
Team ya Yanga ilifika uwanjani? Mbona hunijibu
 
Kutokuingiza timu uwanjani ndo kususa. Sasa TFF waliifuta hiyo mechi kabla ya muda wa kuingia uwanjani. Huwezi susa mechi isiyokuwepo. Tumeelewana boss?

Yaani mpaka hapa, hoja si Simba kususa mechi, ni TFF kufuta mechi.
Nikuelewe vip wakati hata unacho kiandika ww mwenyewe hukielewi.Kwa hiyo TFF wamefuta mechi bila sababu ? Kwa hiyo kile mlicho fanya juzi cha kususa sio hoja kabisa? Sasa kama sio hoja ile barua mliiandika ya nini?
 
Mhhh kwani Mwaduke si amefanya reference kutoka CAF?

Mwaduke=Amerefer CAF.
The Nilicho kileta=Reference from Mwaduke.
Hence.
Nilicho kileta=Reference from CAF .

Algebra ya kawaida tu tena O-Level sio ya Advance.
Kwani hapa tunaongelea Principles of Mathematics au Principles of Referencing mbona unachanganya mafaili?
 
Nikuelewe vip wakati hata unacho kiandika ww mwenyewe hukielewi.Kwa hiyo TFF wamefuta mechi bila sababu ?
Sababu ipo kwenye barua yao, hujaisoma? Hiyo hapo mwisho nimekuwekea.
Screenshot_20250309-110318_Chrome.jpg

Kwa hiyo kile mlicho fanya juzi cha kususa sio hoja kabisa? Sasa kama sio hoja ile barua mliiandika ya nini?
Sio hoja, huwezi kuitumia kupewa point tatu maana haikidhi tafsiri ya kususa.

Mkuu, mambo mepesi haya. Mambo ya Ubaya Ubwela.
 
Kwani hapa tunaongelea Principles of Mathematics au Principles of Referencing mbona unachanganya mafaili?
Ni kitu kile kile sema kimekuwe represented into variable kwa kutumia Algebra. Hamna sehemu nilipo changanya mafaili labda kama ulikimbia hesabu.
 
Back
Top Bottom