Nimeona tangazo la kuahirishwa kwa show za Fally Ipupa Dar na Mwanza.Sikusitushwa hasa kwa sababu ana miziki mingi ya kubahatisha isiyo vutia kama ambavyo ukilinganisha na mkongwe Koffi Olomide.
Fally Ipupa zaidi ya urembo na kukata mauno,ana kipaji cha sauti nzuri.
Hata hivyo sauti nzuri,urembo,na kukata mauno vinaweza tu kuwa vivutio kwa wadada na sio wanaume wapenda muziki.
Huyu jamaa niliona kama vile alipata kiki sana kwenye media za nje kama anavyopata kiki Diamond ingawa hana muziki unaovutia.
Kama mtu angetoa laki moja kwenda kwenye show,ni kwa vile tabia ya matajiri kupenda kutafuta sababu ya kukutana na hasa wakisukumwa na ushawishi wa warembo wanaoweza kuhudhuria show.
Wakati huyo Fally Ipupa akifanya show stejini,wengine waliohudhuria wako kwa ajili ya show off tu.
Huyo jamaa angeweza kuwa bora kama angekuwa kwenye kundi la Quarter Latin la Koffi Olomide.Ni sawa tu na ambavyo JB Mpiana hawezi kuwa bora bila wakali wenzie waliokuwa nao Wenge BCBG.
Kumfananisha JB Mpiana na Fally Ipupa Kiumaarufu ni Upumbavu mkubwa na usiovumilika.
Ni vyema Watu kabla hamjakurupuka kuja kutuonyesha Upumbavu wenu hapa muwe mnajiridhisha hasa Kitaarifa.
JB Mpiana kaanza kuwa maarufu tokea mwaka 1993 tena akiwa ni Kiongozi Mkuu wa Bendi ( Mareshale Mukulu ) wakati Fally Ipupa kaanza kujulikana mwaka 2004 tena akiwa ni Dansa na Muimbaji wa Kawaida mno ndani ya Bendi ya Quarter Latin yake Koffi Olomide.
Ingia YoiTube uone jinsi Wanamuziki wa Kizazi cha sasa akina Fally Ipupa na Mwenzake Ferre Gola wanavyomsifia sana JB Mpiana na kwamba amewafunza Mziki na kila mara Wenge BCBG yake JB Mpiana ikifanya Tamasha Congo DR ( hasa Kinshasa ) Wanamuziki hawa Fally na Ferre huomba kwenda Kuimba nae kama afanyavyo pia aliyekuwa mpiga Gitaa la Bass Didier Masela.
Katika interviews zote azifanyazo Hasimu mkubwa wa JB Mpiana Mkongwe Koffi Olomide amekuwa akisema kuwa Mtu ambaye anamuogopa na kasababisha awe Mbunifu zaidi Kimuziki ni JB Mpiana ambaye kwa msiojua Nyumba zao za Kifahari zipo Jirani kabisa tu.
La mwisho kaa ukijua kuwa Wanamuziki wote wa iliyokuwa Bendi ya Wenge Musica 4 X 4 iliyowajumuisha Wanamuziki wote akina JB Mpiana, Werrason, Blaise Bula ( ambaye Kitaaluma ni Injinia wa Ndege ), Adolphe Dominguez, Alain Makaba 'Prense', Didier Masela, Alain Mpela 'Afande', Ficarre Mwamba 'Mitre' na Rapa ( Atalaku ) Mwanzilishi Roberto Wunda Enkokota wametoka katika Familia za Kitajiri tupu ambapo wengi wao Baba zao walikuwa ni Mabalozi na wengine ni Wakuu wa Vikosi vya Jeshi katika Utawala wa Hayati Rais wao Mobutu Seseseko Kuku wa Zabanga huku Mfadhili wao mkuu Kiserikali akiwa ni aliyekuwa Mtoto Kipenzi wa Rais Mobutu aitwae Jose Kongolo Mibeko Lalwaa ambaye alijiua kwa Kujipiga Risasi baada ya Kujigundua alikuwa ameathirika na VVU.
Dada yake huyu Jose Kongolo aitwae Ngawali ndiyo Yule wakati Baba yao Mobutu akiwa Rais ndiyo alikuwa akisafiri na Ndege aina ya Concorde kutoka Kinshasa hadi Brussels kwenda Kusoma na Kumrudisha ila hivi sasa huyu ( huyo ) Ngawali ni 'Baamedi' katika moja ya Hotel Kubwa Jijini Paris nchini Ufaransa baada ya Kufilisika kutokana na Mali zote za Marehemu Baba yao Kutaifishwa na aliyekuwa Rais wa Congo DR Mzee Laurent Desire Kabila ( ambaye alipokuwa Ukimbizini ) hapa Tanzania alikuwa akijiita ( akiitwa ) Mzee Simwale.
Jikite sana katika kutafuta kujua mengi.