Duuuh! Koffie Olomide hajui muziki?? Ngoja nisikilize vibao vya Papa Plus, Julia na Petit na London kwanza.
Nikiri wazi na najua wengi hapa wananijua kuwa GENTAMYCINE ni Team JB Mpiana na Bendi yangu pendwa ya Wenge BCBG.
Ila kuacha Unafiki na Chuki napingana na wale wote ambao wanasema kuwa Koffi Olomide hana lolote.
Kuna Mtu ( Member ) nimeona mahala amesema kuwa Koffi Olomide hana lolote zaidi tu ya Kuimba kidogo kwa Kuchomokea ila Kazi kubwa wanafanya wengine.
Jamani mbona hiki anachokifanya Koffi Olomide mnachomponda nacho hata Kipenzi changu JB Mpiana nae anakifanya na hata pia Wanamuziki wengi tu wa Congo DR wanafanya hivyo?
Zamani wakati Koffi Olomide alipokuwa akitunga na Kuimba Nyimbo zote Mwenyewe mlisema kuwa alikuwa ni Mbinafsi akaamua kubadilika na kuwapa nafasi Wanamuziki wake na Yeye kuinba kidogo leo hii mnasema haimbi na hajui Kuimba. Mnataka nini nyie?
Labda kwa Faida ya wengi nitoe Elimu kidogo tu ya Mfumo wa Uimbaji wa hawa Wanamuziki wa Congo DR.
Ni kwamba mara nyingi wale wenye Bendi ( Marais akina Koffi, JB Mpiana, Werrason na wengineo ) katika Nyimbo nyingi Kazi yao kubwa nje ya Kutunga pia huwa ni Kuchomokea 'vionjo' vya maneno huku wakiwapa sana nafasi Wanamuziki wengine Kuimba ili Kuwatambulisha zaidi.
Na hata yale majina mbalimbali ambayo huwa mnasikia yakitajwa ( Mtindo unaoitwa Makanga ) katika Nyimbo zao yana maana zaidi Kibiashara kwakuwa Matajiri wengi wa Congo DR hupenda mno Kutajwa katika Nyimbo ili Kuwaongezea Umaarufu.
Ukisikia Wimbo unaanza halafu jina la Mtu linatajwa jua ameshalipa Dola 1000 na ukisikia Jina la Mtu linatajwa katikati jua amelipa Dola 500 na likitajwa mwishoni jua amelipa Dola 250 huku majina mengine mnayosikia katikati ya Wimbo yale huwa yamelipiwa Dola 100.
Na hivi ndiyo Bendi nyingi Kubwa za Congo DR zinavyojipatia Pesa zaidi achilia mbali zile za Viingilio katika Matamasha yao na ndiyo maana Wanamuziki wengi wa Congo DR ni Matajiri wakubwa sana.
Huku ( hapa ) Kwetu Tanzania ukisikia Watu wanatajwa katika Nyimbo nyingi na mbalimbali jua hawatoi ( hawalipi ) chochote kile sana sana hutoa tu Ofa za Bia kwa Wanamuziki hao au Kuwatafutia Mademu ( Mashuga Mami ) ya Mjini yawape UKIMWI na waamze Kuuana katika Bendi zao.
Koffi Olomide ni Habari nyingine na namuheshimu mno kwani nje tu ya kuwa Mwanamuziki ila pia ni Msomi mkubwa sana mwenye Masters Degree yake ya Biashara achilia mbali Degree yake ya Uchumi na pia ni Mjasiriamali mkubwa mno si tu Congo DR bali duniani.
Cc:
Expected Value,
Bila bila