Kuahirishwa kwa show za Ipupa: Muziki wake hauvutii japo ana kipaji

Acha kudanganya umma
 
Mzee una miaka mingapi?..itoshe kusema tu hujui muziki wa Congo Drc na tena ukae kimya kabisa..hivi unamjua Jb Mpiana kweli wewe hata mashabiki wa koffi na Fally ipupa pale Kinshasa wanampigia salute huyu mwamba,nakup assignment kasikilize ngoma hizi tamu kabisa ambazo ingekuwa Marekani zingekuwa hadhi sawa na Soul za George Benson au hata Lionel Richie nenda kasikilize Omba,48 Heures Gecoco,Feux de l amour,Jeannette malizia na Masuwa anza na hizo tu kwanza halafu rudi hapa tukuongezee magoma ya JB ambayo sisi tuliruka nayo enzi hizo
 
Unasemaje? Koffi Olomide?
Umezaliwa jana wewe....

Kwa sasa Congo hakuna kama Koffi...Le mopao.
Koffi huwezi kumlinganisha na JB ama mwanamuziki yeyote kwa sasa Congo

Nimeanza kumsikiliza Mopao 1994 natoka msingi, picha mjongeo ya kwanza kuiona kwenye fideo na video yenyewe nilimuona Mopao. Japo sasa simkubali ki mavazi yake na Umri wetu mie na yeye ila anayesema Mopao si mwanamziki atakuwa kaanza kufuatilia muziki kipindi cha Innos B!.
 
Watoto wanaonyoa viduku na surual za kubana hawawez kuelewa
 
Kuongozi nilikuwa nasubiri Comment akoo tuu kiongoziii
 
Wewe umezaliwa majuzi kipindi cha mziki wa bongo fleva, ladha ya bolingo huwezi kuijua....tuachie wakongwe ambao mziki wa kikongo umetukuza....
Hamnaa lolote,wala sioni ladha ya bolingo zaid ya kuruka ruka tu!bora hata R&B atleast zilinibamba
 
Fally Ipupa ni level nyingine kwenye muziki/
Fally Ipupa hana ubora huo mnaomsifia Kutwa isipokuwa anabebwa zaidi na kuwa Kwake 'very handsome' na kujua Kukata Viuno ambapo huwavutia Mashabiki zake wengi ambao 85% ni Wanawake.

Kama ungeniambia kuwa kwa sasa Congo DR Mwanamuziki 'tishio' na 'mahiri' kabisa kwa Utunzi, Uimbaji, Uchezaji na upangiliaji wa Mziki ni Ferre Gola ningekukubalia 100%

Na hata Ugomvi mkubwa baina ya 'Magwiji' Wawili JB Mpiana na Koffi Olomide ulitokana na Kitendo cha Koffi Olomide kuwachukua 'Kimafia' na kwa Bei mbaya Mwanamuziki Ferre Gola na Mpiga Drums Titina Alcapone kutoka Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana.

Na hili Kulithibitisha hilo ndiyo maana Wanamuziki akina Fally Ipupa na Ferre Gola walivyotoka Bendi ya Quarter Latin yake Koffi Olomide kwenda kuanzisha Bendi zao Mtu aliyemuumiza mno Koffi alikuwa ni Ferre Gola na siyo Fally Ipupa kwakuwa tayari katika Bendi kulikuwa na Mtu mwenye Sauti kama ya Fally Ipupa na anacheza kama Yeye aitwae Cardinale Gento.

Baada ya Ferre Gola kuondoka ( kwa Kunyakuliwa Kimafia ) na Koffi Olomide JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG aliwapata wabadala wake Wawili ambao ni akina ni Rio Biku a.k.a De Jeneiro na pia ana Mtu ana Watu Wawili wenye Sauti inayokaribia Kimfanano kama ya Fally Ipupa waitwao Shai Ngenge ( Mtoto pekee wa Mama Tajiri mwenye Migodi Congo DR ) na mwingine anaitwa Djino Equalizer ambapo huyu Djino hata Fally Ipupa alishawahi Kumvulia Kofia na Kumpigia Saluti kwa Uwezo wake na Kipaji chake Kikubwa alichonacho.
 
Pole sana ila fally wacha awe fally
 
Hamnaa lolote,wala sioni ladha ya bolingo zaid ya kuruka ruka tu!bora hata R&B atleast zilinibamba
Kuna Watu wengine nawashauri ni bora tu mfiche Upumbavu wenu mliorithishwa kuliko kutuboa tu hapa.

Jamani Muziki ni 'Interest' na 'Passion' ya Mtu hivyo ni Upumbavu usiovumilika kwa Mtu ambaye anajua anapenda R&B halafu anaukandia Muziki wa Dansi ambao hana 'Passion' wala 'Interest' nao.

Unasema kuwa wanarukaruka tu hivi hujui kuwa Muziki ni 'Culture' ya eneo husika? Mbona Wamaasai Nyimbo zao nyingi nao huwa wanarukaruka na huwashangai?

Kwahiyo ulikuwa unataka Wanamuziki wa Congo DR nao waimbe na wacheze kama Wanamuziki unaowapenda wa R&B ndiyo uwasifie na uwakubali? You must be very Foolish indeed.

Tokea enzi na enzi 'Identity' ya Muziki wa Congo DR una mpangilio wa mambo makuu Matatu 1. Kuanza Kuimba kisha Sebene linafuta, 2. Kuimba kwa Rhumba tupu ( mziki wa taratibu ) na 3. Sebene mwanzo mwisho ila liwe fupi la Kutambulisha Album husika.

Waingereza wameuza duniani 'Culture' yao ya Lugha ya Kiingereza duniani, Wabrazili wameuza duniani 'Culture' yao ya Mpira wa Samba na Wakongo ( zamani Wazaire ) wameuza duniani 'Culture' yao ya Muziki ambayo hata 99% ya Bendi za Tanzania zinauiga pamoja na Wanamuziki wa Mataifa mbalimbali mfano huko Nigeria, France, Belgium, Ivory Coast, Benin, Uganda, Rwanda, Burundi na Canada.

Cc: Expected Value
 
Umemaliza kila Kitu kuhusu Kipenzi changu 'tukuka' JB Mpiana a.k.a Mareshale Mukulu a.k.a Mukulu ya Bamukulu a.k.a Bin Adam a.k.a Souverain Premiere a.k.a Moto Pamba a.k.a De la Patria a.k.a Papa Cherie a.k.a Le Grand Leadere na a.k.a Lonkia Milo Dankokoo.

Ukiona Kitu chochote kinapendwa au Mtu yoyote anapendwa na GENTAMYCINE jua kwa 99.9999% ni Kizuri na nimeshakipima na Kujiridhisha nacho kwani sina desturi ya Kupenda vilivyo 'vibovu vibovu' tupu.
 
Ongeeni yote lakin mimi nikiwa nakunywa bia zangu fere golaa ni nyokoooo...

Fala yule anabembeleza bia inashukaa kama maji..fundi sana mbwa yulle
Naona Bia bado ziko 'Mbichwani' Kwako au?
 
Mm na mamizik ya bolingo mbali mbal maana sionagi wanachofanya zaid ya kunengua tu mauno na kuvaa minguo kama mitubali
Sasa kama you're this Foolish utaonaje mazuri ya Muziki wa Bolingo wa Congo DR? Hebu kampikie Chai Mumeo awahi Kazini urejee Kitandani kulala na hilo Dela lako kama Puto.
 
Duuuh! Koffie Olomide hajui muziki?? Ngoja nisikilize vibao vya Papa Plus, Julia na Petit na London kwanza.
Nikiri wazi na najua wengi hapa wananijua kuwa GENTAMYCINE ni Team JB Mpiana na Bendi yangu pendwa ya Wenge BCBG.

Ila kuacha Unafiki na Chuki napingana na wale wote ambao wanasema kuwa Koffi Olomide hana lolote.

Kuna Mtu ( Member ) nimeona mahala amesema kuwa Koffi Olomide hana lolote zaidi tu ya Kuimba kidogo kwa Kuchomokea ila Kazi kubwa wanafanya wengine.

Jamani mbona hiki anachokifanya Koffi Olomide mnachomponda nacho hata Kipenzi changu JB Mpiana nae anakifanya na hata pia Wanamuziki wengi tu wa Congo DR wanafanya hivyo?

Zamani wakati Koffi Olomide alipokuwa akitunga na Kuimba Nyimbo zote Mwenyewe mlisema kuwa alikuwa ni Mbinafsi akaamua kubadilika na kuwapa nafasi Wanamuziki wake na Yeye kuinba kidogo leo hii mnasema haimbi na hajui Kuimba. Mnataka nini nyie?

Labda kwa Faida ya wengi nitoe Elimu kidogo tu ya Mfumo wa Uimbaji wa hawa Wanamuziki wa Congo DR.

Ni kwamba mara nyingi wale wenye Bendi ( Marais akina Koffi, JB Mpiana, Werrason na wengineo ) katika Nyimbo nyingi Kazi yao kubwa nje ya Kutunga pia huwa ni Kuchomokea 'vionjo' vya maneno huku wakiwapa sana nafasi Wanamuziki wengine Kuimba ili Kuwatambulisha zaidi.

Na hata yale majina mbalimbali ambayo huwa mnasikia yakitajwa ( Mtindo unaoitwa Makanga ) katika Nyimbo zao yana maana zaidi Kibiashara kwakuwa Matajiri wengi wa Congo DR hupenda mno Kutajwa katika Nyimbo ili Kuwaongezea Umaarufu.

Ukisikia Wimbo unaanza halafu jina la Mtu linatajwa jua ameshalipa Dola 1000 na ukisikia Jina la Mtu linatajwa katikati jua amelipa Dola 500 na likitajwa mwishoni jua amelipa Dola 250 huku majina mengine mnayosikia katikati ya Wimbo yale huwa yamelipiwa Dola 100.

Na hivi ndiyo Bendi nyingi Kubwa za Congo DR zinavyojipatia Pesa zaidi achilia mbali zile za Viingilio katika Matamasha yao na ndiyo maana Wanamuziki wengi wa Congo DR ni Matajiri wakubwa sana.

Huku ( hapa ) Kwetu Tanzania ukisikia Watu wanatajwa katika Nyimbo nyingi na mbalimbali jua hawatoi ( hawalipi ) chochote kile sana sana hutoa tu Ofa za Bia kwa Wanamuziki hao au Kuwatafutia Mademu ( Mashuga Mami ) ya Mjini yawape UKIMWI na waamze Kuuana katika Bendi zao.

Koffi Olomide ni Habari nyingine na namuheshimu mno kwani nje tu ya kuwa Mwanamuziki ila pia ni Msomi mkubwa sana mwenye Masters Degree yake ya Biashara achilia mbali Degree yake ya Uchumi na pia ni Mjasiriamali mkubwa mno si tu Congo DR bali duniani.

Cc: Expected Value, Bila bila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…