Kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu. Upi ni uamuzi sahihi na wenye manufaa (tija) zaidi?

Kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu. Upi ni uamuzi sahihi na wenye manufaa (tija) zaidi?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu. Upi ni uamuzi sahihi na wenye manufaa (tija) zaidi?

images (3).jpg

WANAOUNGA MKONO HOJA ya kuajiri ndugu wa karibu katika biashara zenu wanadai ya kwamba, ndugu yako akikuibia basi ile pesa inakuwa inazunguka mulemule katika ukoo wenu tofauti na kuajiri mtu wa mbali kisha akaiba na kupeleka pesa katika ukoo mwingine.

WANAOPINGANA NA HOJA ya kuajiri ndugu wa karibu katika biashara wanasema kwamba usipoajiri ndugu ndio kuna manufaa zaidi kwa maana ata akikuibia inakuwa ni rahisi zaidi kumfikisha katika vyombo vya sheria tofauti na ndugu wa karibu ambaye utamuonea aibu na vile vile ukoo mzima utakuweka kikao na kuanza kukusimanga kwanini unataka ndugu yako akaozee jela.

Upi ni uamuzi sahihi kati ya kuajiri ama kutoajiri ndugu wa karibu katika biashara? Na kwanini?

images (4).jpg

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Aisee, nadhani inategemea na ukubwa wa mtaji. Kwa mitaji midogo bora ndugu, hata kweny malipo inakua kisela au anawez hata akawa anakaa kwako ikaisha unampa tu za matumizi.

Mtaji ukiwa mkubwa ni rahisi hta kuweka mikataba, hivyo huwazi kuajiri ndugu. Mfano, mauzo kwa siku ikiwa chini ya laki 5 naona ni hasara kuwa na mtu baki.

Mtu baki ni vizuri ukiwa umeandikishana nae malipo na hasara atakazo sababisha, japo kwa ndugu nawew uwe serious kweny kufunga hesabu, ikiwezkana hata kila siku jioni. Ila vizuri zaidi hiyo biashara pia uwe na abc zake, ikiwa mpya hujui challenges zake na ukaweka mtu tu, mtaishia kugombana.
 
Ndugu kikawaidaa huwa tunarudishana nyuma.

Mfano mimi kondakta wa daladala huku kwetu nikiwapakiza ndugu zangu watatu hawatoi hata mia ila sku wakikuta sipo hiyo sku wanalipa daladala zingine ..na hapo sio mia 4 mia 4 kama huko mjini, kitu kuanzia buku 3.
 
WANAOUNGA MKONO HOJA ya kuajiri ndugu wa karibu katika biashara zetu wanadai ya kwamba, ndugu yako akikuibia basi ile pesa inakuwa inazunguka mulemule katika ukoo wenu tofauti na kuajiri mtu wa mbali kisha akaiba na kupeleka pesa katika ukoo mwingine.

Akikuibiaaa akaonga ? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kaka yangu first born aliibiwa na mtu baki aliyemuajiri kama cashier wake.
 
Kaka yangu first born aliibiwa na mtu baki aliyemuajiri kama cashier wake.
Mimi ndugu ntamsupport ata kumtafutia pengine ila kwangu hapana, mambo ya kuitana njoo tusaidianee ni changamoto.

Kwa level ya kampuni ata kama mm ndo share holder mkubwa lazima nikupitishee kwa hr na ufate masharti ili akizengua wamalizane.
 
Kuajiri mtu baki kuna ahueni sana katika biashara, ndugu akizingua kumwajibisha mtihani lakini mtu baki unamwajibisha vizuri, niliwahi mweka ndugu duka la spear tena shughuli yenyewe ina maslahi makubwa nje ya mshahara wake, mfano kitu cha 50k ukikiuza 55k or 60k hiyo ziada ni yake bt cha ajabu kila tukipiga hesabu mzigo umepungua pesa hazionekani nikamtoa

NB:Ndugu huifanya biashara yako kama mali ya nyumbani hivo huiba kwa kuchukua bt mtu baki huiba kwa akili sana
 
Back
Top Bottom