The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kwa mtazamo wangu maendeleo yanaweza kupatikana ikiwa rasilimali za nchi zikapata usimamizi mzuri na mipango ya maendeleo ikapangiliwa vizuri lkn pia wananchi wakatimiza wajibu wao.
Kwa upande wa vyama, naamini ni kama madaraja tu ya kuwasaidia watu kupata sifa ya kuwa wagombea na kukidhi vigezo vya kuchagulika.
Ni kwa mantiki hiyo naamini kwamba suala la uadilifu halihusiani sana na chama alichopo mtu kama ilivyo kwa uwezo wa kuongoza .
Niwaase watanzania tuachane na siasa za kushabikia watu kwa kuangalia rangi ya chama bali tupime uwezo vigezo na uadilifu binafsi wa mtu.
Kudhani kwamba maendeleo yatapatikana tu upinzani ukiingia madarakani sio kweli wala sio kweli kwamba ccm wakitawala basi kuna maendeleo tutapata kwa sababu ni ccm sio kweli.